Big up kwa SAMAKIBA foundation, Wape tabasamu, saidia wazazi na Mwamnyeto foundation.

carnage21

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
521
1,258
BILA Kujali timu unayoishabikia wala Mchezaji unayemshabikia.....hili SUALA la Wachezaji wanaocheza ndani na wale wanaocheza nje ya Tanzania Kutoa misaada ya kuwagusa Moja kwa Moja jamii inayowazunguka Ni Jambo jema ambalo linapaswa kuungwa mkono na kuigwa wachezaji wengi pamoja na vilabu vingine.
FB_IMG_16882402067281645.jpg


WALIANZA MBWANA SAMATTA NA ALIKIBA kupitia SAMAKIBA FOUNDATION kisha wakaja WAPE TABASAMU ya KIBWANA SHOMARY na DICKSON JOB baadae wakaja SAIDIA WAZAZI ya Feisal Salum na Abdulaziz Makame na sasa MWAMNYETO FOUNDATION ya Bakari Nondo Mwamnyeto pamoja na Zawadi Mauya.

IMEKUWA Kama Desturi yao kwa Mechi zote wanazocheza kile kinachopatikana kinaenda kurudisha fadhila kwa wahitaji.....Inawezekana hawakuwaza kuwa KUPITIA kuandaa hiyo Michezo Rais atachangia chochote,atatoa neno lolote,Mashabiki na wadau mbalimbali wataongezea chochote pia....NINAAMINI kupitia matukio ya namna hiyo hufungua milango ya Baraka nyingi kwao pamoja na kurudisha tabasamu kwa wahitaji.

LAKINI pia hii inaongezea Mashabiki kuwa wengi zaidi na soka kuchukuliwa kwa uzito mkubwa kuanzia kwa wazazi kuelekea kwa watoto wenye ndoto za kuwa wachezaji badala ya kuchukuliwa kama Mchezo wa kihuni na badala yake kuonekana Mchezo wenye thamani na unaoweza kufanya makubwa kwa familia mpaka jamii kwa ujumla.

UPENDO unaosababishwa na muunganiko baina ya Wachezaji na Mashabiki pamoja na wachezaji kwa wachezaji unakuwa ni wa kudumu kutokana na matukio ya aina hii ambayo humgusa kila mmoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom