Bifu la walioolewa na mama mkwe chanzo nini?

Kuna mtu halewi sio mzinzi kiufupi hana uchafu Wala mambo ya kipuuziiiiiii ila mkeo mamaake na ndugu zake wote wanampenda mke wake kweli kweli sasa nayo vipi?
Ila yupo wa kiume pekeake au ndo sababu!?
Au ni wee ndo unaejuzungumzia?
 
Mkuu mahusiano ya mkeo na ndugu zako yanajengwa na wewe mwenyewe,, inategemea na ulivo mtambulisha kwenu na unavyo mzungumzia kwa ndugu zako..

Jitahidi upunguze mazoea baina ya mkeo na familia yako,, hili litasaidia sana coz KUZOEANA SANA NDIO KUNAPUNGUZA HESHIMA,, make sure wanakutana kwenye mambo ya msingi tu.

Thank me later
 
Au mara nyingi mchumba anaweza kupatikana lakini ndugu wasimpende, kama ndugu yao alivyompenda mpaka akakubali kufunga ndoa naye. Yaani mara nyingi kukosea kuoa ndiyo kunaanzia hapo kwa ujumla.
Kwa hiyo wao ndio wanapaswa kutafuta mke au?
 
Mimi suala la kuoa naona bado ni jambo la muhimu sana, kwa sababu bila mwanamke maisha ya mwanaume kama yanakuwa hayana maana vizuri. Lakini nawaza kuja kuoa halafu changamoto zisizo na msingi kama hizi zikawa zinaendelea katika familia yangu. Negativity mbaya sana inaharibu kwa utaratibu mzima wa maisha kwa ujumla.
Kwa hiyo ili kuleta positivity nimwache huyu mwanamke?
 
Wanawake vichokochoko huwa havituishi ikiwemo kununiana na maneno ya hapa na pale wewe Cha msingi usi side na pande yoyote au kumtetea yoyote hapo. Pia mamako vile umeoa anaona attention humpi uko na mkewe sasa hyo case tu.
 
Sababu ya kwanza wivu, hasa unapokuwa na uwezo kidogo wa kiuchumi na familia ilisaport kwa hayo mafanikio kidogo uliyonayo.

Jambo la pili ni kuishi nao pamoja, kunawakati wanashindwa kuvumiliana Kwa mapungufu yao, maana kila mmoja anamapungufu yake ya kibinadamu.

Jambo la mwisho ni tabia tu ya kibinaadam katika kuamua mtu wa kumpenda au kumchukia bila hata sababu, au sababu zisizo na mashiko.
Maana unachokipenda wewe si lazima na wengine wakipende hatakama ni kizuri au chema.

Mke anaweza kuwa mwema anahuruma anajali lakini akaonekana anajipendekeza. Unaweza kuwa na mke kauzu mtata kwelikweli lakini mama yako akampenda tu bila kujali mapungufu yake.
 
Kwa hiyo wao ndio wanapaswa kutafuta mke au?
Sina maana hiyo mkuu, wao ndiyo lakini vitu kama hivi hutokea, ndugu wanakwambia hawajampenda mke wako, au kwa ufasaha zaidi wanakuwa na mashaka na mke.
Mara nyingi hii hutokana na kuongozwa na instinct au hisia kuwa mtu fulani siyo mtu sahihi, hii inaweza kuwa sawa ama si sawa kutokana na experience ya ndugu wa muoaji.
Si unafahamu mkuu at first sight na mtu yoyote unayekutana naye kuna ile hisia inakuja kama huyu mtu unaweza ukaelewana naye ama mkapitia wakati mgumu. Kupitia observation katika mazungumzo ya kwanza kuna first impressions.
 
Kwa hiyo ili kuleta positivity nimwache huyu mwanamke?
Hapana mzee, kiimani wanasema Mungu hakupi jaribu usiloweza kulishinda. Kama vitu hivyo vinatokea kwenye ndoa inakupasa kupambana ipasavyo kuondoa tofauti zitakazokuwepo kati ya mke wako na ndugu zako.
Kwa mfano ndugu wapo nyumbani kwako, na wewe unafahamu kuwa hakuna maelewano, kutakuwa na ile amani ya kujumuika pamoja, ukifahamu fika kwamba mke wako na ndugu zako wana tofauti zao za mara kwa mara?
Ukiona maelewano hakuna means kwamba moja kati ya wapinzani wawili ana negativity au wote wana negativity. Lakini inabidi uombe Mungu changamoto zisiwe nyingi katika maelewano ikasababisha ndoa kuyumba ama kuvunjika.

Kuna mhindi anaitwa Dandapani aliwahi kusema kuwa where energy goes awareness flows, so if its negative energy, you know what the outcomes will be.
 
Mkuu mahusiano ya mkeo na ndugu zako yanajengwa na wewe mwenyewe,, inategemea na ulivo mtambulisha kwenu na unavyo mzungumzia kwa ndugu zako..

Jitahidi upunguze mazoea baina ya mkeo na familia yako,, hili litasaidia sana coz KUZOEANA SANA NDIO KUNAPUNGUZA HESHIMA,, make sure wanakutana kwenye mambo ya msingi tu.

Thank me later

 
Mara nyingi nimeshuhudia mabifu kati ya mwali na mama mkwe na mawifi,ukiangalia hakuna sababu za msingi za mabifu haya.Yamenikuta ndo mana nasema hivyo.Ukiangalia nampenda wife na mama nampenda pia.Kuoa ndio chanzo cha kuchukiana na mama sasa.Dah kua uyaone
Dah
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom