Bifu la Eminem na Snoop Dogg

anonymousafrica

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
611
639
Au niite mgongano (maana halijawa bifu 100%, ila nadhani nimeeleweka kwa huo msamiati) Mwaka jana mwishoni kumeibuka msuguano (kutoelewana) kati ya snoop dogg na Eminem.

Kumbuka hawa jamaa wamekuwa karibu kwa mda mrefu bila kusahau wanaunganishwa na Dr Dree (wote ni watu wa karibu na dree na pia wamewahi kufanya baadhi ya kazi pamoja) Nadhani kwa mwaka 2020 kurudi nyuma - ukiulizwa ni watu gani wamekaa pamoja kwenye game mda mrefu bila msuguano ni 50cent, Dr Dree, Eminem na Snoop Dogg.

f4822b8f6aff99a96c998a8cd85b1813.jpg
Nini sababu/chanzo cha bifu la snoop na Eminem (Marshal Mathers) Kwanza inajulikana ukivurugana na Eminem lazma akuchane tu, kama anamchana mama mzazi atakuacha ww?, alipita na Snoop kwenye Zeus ila tuangalie mchezo ulikuaje.

Mwakajana kuna jamaa anaitwa
@NoLifeShaq alipost Twitter na kutaka watu watume best rappers wao. Eminem alicomment na kuwataja Wayne, Pac, Royce, Jay, Redman, Treach, G. Rap, Biggie & King Crook .... Plus Redman, LL, Nas, Joyner, Kendrick, Cole, Andre, Rakim, Kane
EsZuWfSW8AEEZq-.jpg
EsZuXPCXMAEc6J2.jpg

Snoop nae si akalipa akaja na List yake ya wasanii bora 10 kupitia account yake ya instagram na kuwataja .. “Slick Rick / Ice Cube / L. L. Cool J / K. R. S. 1 / Rakim / Run from Run D.M.C. / D from Run D.M.C. / Big Daddy Kane / Ice T / Too Short.”

Hakuishia hapo,
alifanya interview fulani..na alipoambiwa ataje wasanii anaowakubali alianza kwa kusema Hawa marapa wakizungu hawana heshima na huu mziki wa rap.. Unajua Eminem anajiona kama msanii bora sana, ila ajue asingejulikana wala kuskika kipaji chake bila Dr Dree..
amshkuru sana Dree kwa kumnyanyua ila atambue miaka ya 1980 kulikuwa na wasanii wakali zaidi yake na yupo kwenye game mda mrefu, mashabiri wanamkubali kwa mashairi yake ila akae akitambua bila Dre asingefika hapa
EsZuZYpW8AAIeW_.jpg

Povu lilikuwa jingi mno.

Hapo ndipo Zeus ikatoka... na Eminem hakuficha, alimtaja snoop Direct huku akisema, nimezoea sana kurushiwa mawe ila sikutegemea kama mawe haya yangerushwa kutoka kwa watu wa upande wangu
.. na kukubali kwamba mchizi nlikuwa namkubali sana hapo mwanzo
ila ndo nagundua kumbe mchizi ni mbwa........alikuwa snoop God but ni real DOG..tena kwa kumuita ZEUS (Mungu mrefu wa kigiriki ambaye hutokea kwa ishara ya radi). Mpaka sasa maneno yamezidi kuwa mengi..
Na kwa namna hiyo (mashabiki wanadhani watu hawa walikuwa hawapatanitoka zamani ila walikuwa hawajapata site ya kuchanana) Grudges are never end.
EsZu0poXUAAsOAp.jpg
EsZu1BJXEAA-AUX.jpg

Kuna jamaa alipost insta picha ya Eminem na Snoop na kisema hofu yake juu ya bifu hilo mwaka huu, snoop alicomment na kusema "Hakuna shida, tuko poa" akionyesha hana bifu lolote na Eminem.

Kwenye redio Eminem alikiri kupanic kwasababu hakutegemea Snoop kuongea vile,.. alichosema Snoop ni kweli kabisa, mimi sio kitu bila Dr Dre lakini imekuwaje Snoop akayasema yote hayo na kikubwa style (tone) ya snoop kwenye kuelezea hayo ndiyo iliyonikera.
EsZu1o8XIAAXS46.jpg

Nnachofurahi naweza kuishi bila hayo/yeye, jamaa kanivunjia heshima sana Baada ya washkaji wengi kumtaka Snoop ajibu, alicomment kwa mtu mmoja huko insta “Pray I don’t answer that soft ass shit.”
 
Snoop anachikitafuta atakipata tu.

Huenda eminem anamuheshimu tu kama brother lakini kwa namna yoyote ile snoope dog hawezi kumfikia eminem hata robo.

Sheria ya kwanza ukiwa star wa hiphop jitahidi kukaa mbali sana kwenye kuanzisha ugomvi na eminem, Huyu mzungu hakuna mtu anaemweza akianza kukuchana.

Snoop ajaribu kuficha hisia zake, Sio peke yake anaemchukia eminem, wapo wasanii wengi wa hiphop sana sana weusi wanamchukia sana eminem maana anaweza mno lakini wanajisitiri.
 
Snoop ana wivu na ubaguzi tu, ndio maana anang'ang'ania kutaja Rappers Weusi akidai ndio wakali kuliko EM, na ndio wanaingia kwenye top 10 yake..ila Wakongwe wenzake wengi tu wanamkubali.
Kila mmoja na enzi yake, snoop alishalivaa taji la ufalme kwa miaka kama si miongo,ila muda wake ndiyo umeisha hivyo,enzi zake hata marshall angechana vipi bado style ya dog ingemshusha tu,ila sasa dog inabidi tu akubali ukweli,muda umemtupa mkono
 
Sio kwamba Eminem anajiona ni rapa bora sana, HAPANA. Ukweli ni kwamba Eminem ni mwanahip hop/rapa bora kabisa kuwahi kutokea hapa duniani. Sio kwamba yeye anahisi hivyo, bali ndivyo ilivyo. Hata Messi tusingemjua bila Barcelona, lakini hiyo haivui ufalme wa Messi katika kandanda.
 
ila Em naye kazingua na list yake
seriously unamtaja Redman, Wayne na LL
What about Black Thought, TechNine n Scarface?

Snoop must have been high wakati anatoa comment yake cz kaja na list ya rappers wa 80s wakati Em kaja na two generations (old skul and new skul).
 
Snoop anachikitafuta atakipata tu.

Huenda eminem anamuheshimu tu kama brother lakini kwa namna yoyote ile snoope dog hawezi kumfikia eminem hata robo.

Sheria ya kwanza ukiwa star wa hiphop jitahidinkukaa mbali sana kwenye kuanzisha ugomvi na eminem, Huyu mzungu hakuna mtu anaemweza akianza kukuchana.

Snoop apunguze wivu
hahahaaaa kila mmoja hapo anastyle yake na upekee wake... Japo ni kweli, Eminem anaflow sana - snoop mtu wa burudani
 
Kila mmoja na enzi yake, snoop alishalivaa taji la ufalme kwa miaka kama si miongo,ila muda wake ndiyo umeisha hivyo,enzi zake hata marshall angechana vipi bado style ya dog ingemshusha tu,ila sasa dog inabidi tu akubali ukweli,muda umemtupa mkono
wote wamehit kwenye game kwa wakati mmoja... kwa mziki wa wenzetu game haliwatupagi mkono, still watu wanapenda mziki wao. Jay Z amezaliwa 1969 na ni kati ya wasanii wakongwe mno kwenye game na bado tunahitaji kuskia kazi nyingi sana kutoka kwake. Hii notion ya kutupwa mkono ndio chanzo cha kuua mziki wa wazee wetu kina Gurumo, Bichuka, Eddie Sheggy, Momba, Marijan na ma bro kama Juma nature, Hashim, Afande, Prof, Inspecta. Nyimbo zote ni kali, tusizitupe mkono eti kwasababu ni za wakati fulani
 
Back
Top Bottom