Bidhaa zapanda bei, wanyonge walia kila kona

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Tumezoea kusikia neno wanyonge katika serikali ya awamu ya sita kuwa ni kejeli iliyopitiliza kwa watanzania ! Katika pitapita zangu mikoa mbalimbali hususan kagera kigoma mwanza na mara na shinyanga walalamikia vifaa vya ujenzi bei zake kuwa juu mfano cement kwa mkoa wa shinyanga tsh 21000/= tofauti na awali ilikuwa tsh 16000/= mwanza kwa sasa bei ya cement sh 23000/= mara msoma tsh 25,000/= , kagera na kigoma tsh 25000/=!

Nishat mafta petrol lita @1 mwanza tsh 2720/=; shinyanga tsh 2640/= kagera na kigoma 2820/= awali mafta yalitapatikana kwa kila lita tsh 1810/= kwa sasa mambo yamebadilika sukar mafta ya kupikia hvohvo bei ipo juu!

Baadhi ya vijana wamesema kwa sasa ni vigumu sana kuwekeza pesa kwenye ujenzi kwan vifaa vya ujenzi vipo juu na maisha kwa ujumla yamekuwa magumu.

Kwa vile MHESHIMIWA RAISI SAMIA SULUHU HASSAN tunaomba tupia jicho kwenye wizara husika hali ni ngumu huku mitaan jua kali pesa hamna

. NAWASALIMU KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KAZI IENDELEEE!
 
Huku katavi saruji 25000,
Unga wa ngano 42,000
Mafuta ya kula Lita 10 sh. 50000.
HALI NI TETE KILA UCHAO
 
Waziri wa biashara na viwanda ni mzee wa ngwini, mambo ya biashara atayajulia wapi? Bei zikipanda ni neema kwa serikali vat na kodi ya mapato inaongezeka
 
Acha CCM watumie dola tu kubaki madarakani , maana kwa hali ilivyo mtaani , atakayeipigia kura CCM labda awe ameteuliwa sehemu ya uongozi anakula hela
 
Ingekuwa nchi nyingine bidhaa moja tu ipae bei hovyo hovyo watu wangekuwa mtaani tayari na viongozi wanaweza kujiuzuru,
Tanzania kuna watu wajinga tu na huko wanakozindika viongozi wetu wanajua kabisa waganga walioturoga kina mtabiri maarufu Afrikanmashariki na kati na kina deepwaters wameshakufa wakutuagua hayupo, ndio maana viongozi wanajiamini kutuburuza hovyo namna hiyo.
 
Bei ya kg 1 ya mchele kwa sasa bei ya chini ni 1600.

Sembe nayo ndo hivyo kg 25 kwa 20000.
Mliopo mijini kwenye mfumuko wa bei mtashaaa.😉😉😉😉😉😉
 
Nchi hii imekuwa ngumu kuishi ccm wenye madaraka wanachekelea wapiga kura wakilia na kusaga meno
 
Ingekuwa nchi nyingine bidhaa moja tu ipae bei hovyo hovyo watu wangekuwa mtaani tayari na viongozi wanaweza kujiuzuru,
Tanzania kuna watu wajinga tu na huko wanakozindika viongozi wetu wanajua kabisa waganga walioturoga kina mtabiri maarufu Afrikanmashariki na kati na kina deepwaters wameshakufa wakutuagua hayupo, ndio maana viongozi wanajiamini kutuburuza hovyo namna hiyo.
Hata weee ni mtanzania unaweza kusaidia kuanza kuwa mtaani ili wengine wafuatie
 
Unahitaji PhD kujua ya kwamba Rais ambae siyo chaguo la wananchi na ambae hana kibali cha wananchi hawezi kuhangaika na matatizo ya wananchi?

Hata kama ni mimi nilipora chaguzi na kuchukua dola wala nisingehangaika na majitu ambayo ni mazembe katika kutetea demokrasia yao.Ningekuwa nazurura tu kula bata.

Hayo unayopitia ya bei ya vitu kuwa juu ndiyo gharama ya kuruhusu vibaka ambao hawana ujuzi wa kuendesha nchi kupora chaguzi na kuchukua dola.

 
Suku

Sukuma gang. Magufuli amekufa na hatarudi.
Tunaongelea maswala ya msingi wewe unaingiza mambo ya SUKUMA GANG hivi ni lini tutabadilika na kujadili mambo ya msingi na kuwa kitu kimoja au wewe unasema hayo umeshiba
 
Back
Top Bottom