Bidhaa unazoweza kuuza Ulaya zisizohitaji mtaji mkubwa sana

Fuga Kisasa

Senior Member
Jan 16, 2016
165
91
Habari zenu,

Naomba kuuliza ni aina ipi ya bidhaa ambazo hazihitaji uwe na mtaji mkubwa sana ili uweze kuziuza nchi za Ulaya.

Mimi nilikuwa na idea ya kuuza sandal za kimasai maana nahisi ni unique hivyo naweza kupata wateja msimu wa summer na pia nilikuwa nafikiria kuuza asali. Mwingine mwenye mawazo mbadala anaweza kuchangia.

Karibu sana kwa mjadala.
 
Mtaji mdogo !!!!!!!!! hebu fafanua ( maana kibongo bongo ukiwa na mtaji wa pesa ya kuweza kujenga nyumba ya 30milion - 50m si mtaji mdog )
 
Nadhani nchi za ulaya hawatumii ugali, hiyo sembe itakuwa na soko kweli?
Wapo waafrika wengi wanaotamani sembe ya nyumbani believe me kuna jamaa alileta container liliisha kwa siku mbili tu na hakuleta tena sijui kwa nini
 
Naomba nikuulize. Kwa nini unataka kuuza ulaya?
Exportation siku zote inalipa zaidi kwakuwa unaleta pesa za kigeni nchini pia ina mchango mkubwa katika kukabiliana na upandaji wa dollar dhidi ya shilingi. Maoni yako mkuu?
 
Exportation siku zote inalipa zaidi kwakuwa unaleta pesa za kigeni nchini pia ina mchango mkubwa katika kukabiliana na upandaji wa dollar dhidi ya shilingi. Maoni yako mkuu?

Una experience ya ku run biashara yoyote ndani au ya nchi au ni biashara ya kwanza unayotaka kuanza?
 
Prolem iliyokuwepo na kufanya business nje ya nchi (na wewe ukiwa umo ndani) ni kuwa utapata mitihani kwenye
  1. Market research (ni ngumu kufanya)
  2. Marketing (ni ngumu)
  3. Complication ya kusafirisha mizigo
Biashara nyingi zinazouza bidhaa nje ya nchi, zimeanza kuuza ndani ya nchi ikisha ndio ikatoka nje. Sijui kama ushawahi kusikia msema unaosema "Act Local. Think Global".

Labda bidhaa zako ziwe za ki dijitali ambayo haihitaji wao kusubiri na kupokea mzigo.

Hilo ni wazo langu. I might be wrong.
 
Pata maelezo toka bodi ya Biashara za nje ili ujue walaji wanahitaji nini huko. Kuhusu mtaji waza vema mtaji mkubwa ni faida kubwa. Kopa ukishakuwa na hakika ya aina ya biashara usiwaze mambo ya mtaji mdogo.
 
Back
Top Bottom