Biashara Kumi (10) Unazoweza Kuanzisha na Kufanikiwa Kimaisha

Drop shipping Tanzania

Senior Member
Jun 15, 2020
198
500
Salute wakuu !!
KARIBU kwenye Jukwaa letu la Biashara, Uchumi na Ujasiriliamali. Leo nimekuandalia Biashara 10 ambozo ukizifanya zinaweza kukuleta mafanikio makubwa sana.

Biashara Kumi (10) Unazoweza Kuanzisha na Kufanikiwa Kimaisha.

Mwaka huu 2020 ni mwaka ambao moja ya malengo ambayo kila mtu anapaswa kuwa nayo ni malengo ya kibiashara. Kama bado hujawa na biashara basi unapaswa kuanza biashara yako mwaka huu. Na kama tayari una biashara, basi unapaswa kuikuza zaidi biashara yako mwaka huu 2020.

Nyakati zinapokuwa ngumu, usikazane kuwa na biashara ya kipekee, ambayo unahitaji kuanza kumshawishi mteja kwa nini anapaswa kununua unachouza. Ukishaona biashara unayofanya au unayotaka kufanya inakubidi uanze kumshawishi mteja kwa nini anapaswa kununua, hapo upo njia mbaya. Mteja anapaswa kujua tayari kwa nini anapaswa kununua, na avutiwe kununua kwako kwa huduma nzuri unazotoa.

1. Bidhaa za chakula.

Kwa kuwa watu bado wanakula, na wataendelea kula siku zijazo, kuanza biashara ya kuuza bidhaa za chakula ni hatua sahihi kwako kuchukua. Hapa unaweza kuuza na kusambaza bidhaa za chakula kama nafaka, mafuta na bidhaa nyingine muhimu.

Angalia uhitaji wa bidhaa za vyakula kwa wale wanaokuzunguka au unaoweza kuwafikia kisha wapatie bidhaa hizo kwa kiwango na gharama ambazo wanaweza kumudu huku wewe ukipata faidia ili biashara iweze kuendelea.

Uzuri wa biashara ya bidhaa za chakula unaweza kuanza na mtaji kidogo, ukatafuta bidhaa zilizo bora na kuweza kuwasambazia watu kule walipo. Biashara ya mchele, mahindi, maharagwe na nafaka nyingine zina uhitaji mkubwa kwa watu.

2. Huduma za chakula.

Biashara nyingine unayoweza kuanza kwa mafanikio mwaka huu 2020 ni biashara ya utoaji wa huduma za chakula. Hapa unatengeneza na kuuza chakula bora ambacho watu wanaweza kukimudu.

Uzuri wa biashara hii ni kwamba, watu wengi wanabanwa na kazi au biashara zao na hivyo hawawezi kuandaa vyakula vyao, hasa vya mchana. Hivyo kwa kuwajua watu wa aina hii na namna unavyoweza kuwafikia, unaweza kuwapatia chakula ambacho ni bora kwa gharama wanazoweza kulipia.

Kingine muhimu ni kwamba watu kwa sasa wanajali sana afya zao, hivyo wanakula mlo bora, unaweza kutumia nafasi hii kutoa vyakula bora kiafya badala ya vyakula vya haraka ambavyo siyo bora.

Unaweza pia kutoa huduma ya matunda, juisi na huduma nyingine za chakula kwa wale wenye uhitaji.

3. Bidhaa za mavazi.

Kama ambavyo tumeona, watu wanaendelea kuvaa nguo, bila ya kujali mambo ni magumu au la. Hivyo unaweza kuingia kwenye biashara kwa kutoa bidhaa za mavazi. Hapa unauza mavazi kama nguo, viatu na mengineyo.

Unachohitaji hapa ni kujua uhitaji wa watu kwa wakati mbalimbali. Kwa mfano kipindi cha mwanzo wa mwaka bidhaa nyingi za mavazi zinazotoka ni zile zinazohusiana na mavazi ya shule. Pia katika kipindi cha sikukuu, watu wanajibana wawezavyo ili wavae nguo mpya.

Unapochagua kuingia kwenye biashara hii ya bidhaa za mavazi, angalia aina ya watu ambao ni wanunuaji wazuri. Mfano mavazi ya wanawake na watoto yanatoka zaidi kibiashara kuliko mavazi ya aina nyingine.

Uzuri wa biashara ya bidhaa za mavazi ni kwamba, unaweza kuianza kwa hatua ndogo sana, huhitaji hata kuwa na eneo la biashara. Unaweza kuchagua wateja unaowalenga, ukachagua bidhaa zao kisha kuwasambazia au kuwatangazia kwa njia ya mtandao.

4. Biashara ya huduma za mavazi
.
Huduma za mavazi ni aina nyingine ya biashara unayoweza kuanza, ambayo itakuwezesha kupiga hatua kubwa. Kama una ubunifu wa mavazi, au unaona uhitaji wa mavazi ya aina fulani, unaweza kutoa huduma ya kuandaa mavazi hayo.

Hapa tunazungumzia kutoa huduma ya kuwaandalia watu mavazi kwa namna wanavyoyataka. Pia kuwasaidia watu kurekebisha mavazi yao. Biashara hii unaweza kuifanya kama unao ufundi wa kutengeneza mavazi. Lakini hata kama huna, unaweza kupata mtu mwenye ufundi ukawa unampa maelekezo na wewe kuwa na kazi ya kutafuta masoko au kusambaza yale mavazi yanayotengenezwa.

Siku hizi zipo mashine ambazo ni rahisi kutumia kushona mavazi ya aina mbalimbali ambazo unaweza kuwa nazo na kuanza kiwanda chako kidogo cha mavazi.

5. Ufugaji wa kibiashara – kuku.

Hakuna familia ya asili ya kiafrika ambayo haijawahi kufuga kuku. Na kuku ni moja ya biashara ambayo soko lake halijawahi kuyumba. Zimekuja biashara za ndege wa aina mbalimbali kama kware lakini zimepita na kuacha biashara ya kuku ikiwa imara. Huhitaji kumshawishi mtu kwamba anahitaji kula nyama ya kuku, au kula mayai, ni kitu ambacho kwa wengine ni ufahari.

Unaweza kuingia kwenye ufugaji wa kibiashara na kufuga kuku ambao utaweza kuuza mayai, kuuza vifaranga na hata kuuza kuku wenyewe. Unaweza kufuga kuku wa kienyeji, kuku chotara na hata kuku wa kisasa kabisa. Unachohitaji kuangalia ni uwezo wako na uhitaji wa soko unalolenga.

Uzuri wa ufugaji wa kuku ni kitu unaweza kuanza kwa hatua ndogo na kukuza. Pia unaweza kufanya huku ukiendelea kufanya vitu vingine. Pia itakuhitaji uwe makini ili ufugaji wako ukue.

6. Ufugaji kibiashara – samaki.

Samaki ni chakula kingine ambacho kina uhitaji mkubwa sana kwenye jamii zetu. Ni mboga ambayo ina uhitaji mkubwa na hivyo ukiweza kuzalisha kwa kiwango kizuri, ni biashara nzuri kwako kufanya.

Ufugaji wa samaki kwa sasa umerahisishwa kutokana na upatikanaji wa huduma muhimu za samaki. Huduma kama vyakula vya samaki, ujenzi bora wa mabwawa ya kufugia samaki zimefanya ufugaji wa kibiashara wa samaki kuwezekana. Japo ufugaji wa samaki unahitaji mtaji mkubwa, inawezekana pia kuanza kidogo na ukafanya vizuri.

7. Kilimo biashara – mbogamboga na matunda ya muda mfupi.

Hata kama uchumi ni mgumu kiasi gani, watu hawatakula chakula bila ya kitunguu, bila ya nyanya, bila ya bamia. Watu wataendelea kula mchicha, matembele na mboga nyingine. Na muhimu zaidi matunda kama matango, matikiti maji na hata ndizi ni vyakula ambavyo kila mtu ana uhitaji navyo.

Hivyo eneo unaloweza kuingia kibiashara mwaka 2020 kulingana na nafasi na uwezo wako ni kilimo biashara cha mbogamboga na matunda ya muda mfupi. Ninaposema kilimo biashara namaanisha ulime kwa lengo la kuuza, hivyo kulima kwa viwango vizuri na ubora ambao unakubalika na soko unalolenga.

Unaweza kulenga wanunuaji wa rejareja au kuuza kwa wanaonunua jumla, kama mahoteli au maduka makubwa.

8. Kilimo biashara – mazao ya chakula.

Mazao ya chakula kama nafaka, mahindi, maharagwe na mpunga ndiyo mazao yanayoongoza kwa kuliwa sana kwenye jamii zetu. Hivyo hili ni eneo ambalo unaweza kuingia kibiashara na ukafanya vizuri kwa mwaka huu 2020. Unaweza kuingia kwenye kilimo moja kwa moja na ukalima kibiashara, kwa njia ambayo utazalisha kwa kiwango kikubwa na kwa ubora wa kuweza kuuza.

Lakini pia kama huwezi kulima, kwa kukosa nafasi au usimamizi mzuri, unaweza kununua mazao hayo kwa wingi kwenye msimu wa mavuno, kuyaongeza thamani na kuyauza kwa wahitaji. Mfano kununua mpunga wakati wa mavuno, kuukoboa, kuuhifadhi kwenye vifungashio vizuri na kuuza kwa watumiaji ni biashara ambayo inaweza kukupeleka kwenye mafanikio makubwa 2020.

9. Biashara ya vyakula vya mifugo na huduma zake.

Watu sasa wanafuga, kuanzia kuku, mbuzi, ng’ombe, sungura, samaki na kadhalika. Unaweza kuingia kwenye biashara kwa kutoa huduma mbalimbali za kuwezesha wafugaji kupata mafanikio kwenye ufugaji wao.

Hapa unaweza kuingia kwenye biashara ya kuuza vyakula vya mifugo, kuuza madawa na virutubisho vya mifugo na hata kutoa huduma za vyakula mbadala kwa wafugaji. Na kama wewe ni mfugaji au una utaalamu kuhusu mifugo, unaweza kutoa ushauri kwa wafugaji kibiashara pia.

10. Huduma za ushauri wa kitaalamu.

Kwa jambo lolote ambalo umesomea, au umeshakuwa na uzoefu nalo, kuna watu ambao wamekwama na hawajui wafanye nini. Hapa unaweza kuingia kwenye biashara ya kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa lile eneo ambalo una utaalamu au uzoefu nalo.

Kama umesomea mambo ya afya unaweza kutoa ushauri wa kiafya kwa watu na wakakulipa. Kama umesomea au una uzoefu kwenye biashara, unaweza kuwashauri watu kuhusu biashara na wakakulipa.
Angalia kipi unajua na watu hawajui, kisha wape ushauri kwa njia ambayo watakulipa.

Asante.
 
swahiba Senior

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
2,285
2,000
HAHAHAHAHAA
HUWEZ kutoka kimaisha kwa biashara hizo zaid ya kupata ela ya kula tu na majitaj mengine madogo madogo.
Nilifkir utazungumzia biashara ya kununua mazao kisha uweke stoku ili uuze pindi bei ikipanda. Hii biashara itakutoa kuliko hiyo ya kwako
Nadhani biashara ya kununua mazao na kuweka stock huifahamu, unaisikia tu. Ni biashara moja ya kipumbavu sana. Unaweza nunua mpunga wa 5M ukaa miezi6 ukauza ukapata faida ya 1M fikiria mtaji wa 5M upate faida ya 1M kwa miezi 6 wakati kuna biashara ukiwa na 5M kila mwezi unatengeneza 1M.
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,440

Mkuu acha uongo , Sasa hivi ifakara wanauza gunia moja la mpunga la kilo 100 kwa shilingi 60,000 ... Kwa hiyo ukiwa na milion 5 unachuua magunia 84 hivi.

Mwezi wa kumi na mbili gunia huuzwa mpaka laki 1 na ishirini.

Gharama yako ni kuweka stoo huko ifakara ambapo ni tsh 2000 kwa gunia moja ambapo Ni lifetime cost.

Ninachojua mpunga unaweza kukurejeshea hela yako almost Mara 2.
 
Drizzle

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
4,884

Kuna watu huandika kwa nadharia ila umeandika kwa vitendo. Safi sana.

Hii ndio hoja hupingwa kwa hoja nzito.
 
LOVE U JF

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
2,100
2,000
Nadhani biashara ya kununua mazao na kuweka stock huifahamu, unaisikia tu. Ni biashara moja ya kipumbavu sana. Unaweza nunua mpunga wa 5M ukaa miezi6 ukauza ukapata faida ya 1M fikiria mtaji wa 5M upate faida ya 1M kwa miezi 6 wakati kuna biashara ukiwa na 5M kila mwezi unatengeneza 1M.
Kweli but ni biashara ipi ?
Itaje ndugu
 
kalisheshe

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
1,105
2,000
IMG_20200621_030522.jpg
 
Bestfredy

Member
Jan 4, 2016
86
125
Mkuu acha uongo , Sasa hivi ifakara wanauza gunia moja la mpunga la kilo 100 kwa shilingi 60,000 ... Kwa hiyo ukiwa na milion 5 unachuua magunia 84 hivi.

Mwezi wa kumi na mbili gunia huuzwa mpaka laki 1 na ishirini.

Gharama yako ni kuweka stoo huko ifakara ambapo ni tsh 2000 kwa gunia moja ambapo Ni lifetime cost.

Ninachojua mpunga unaweza kukurejeshea hela yako almost Mara 2.
Hujui unachoongea.
 
darubin

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,423
2,000
Nadhani biashara ya kununua mazao na kuweka stock huifahamu, unaisikia tu. Ni biashara moja ya kipumbavu sana. Unaweza nunua mpunga wa 5M ukaa miezi6 ukauza ukapata faida ya 1M fikiria mtaji wa 5M upate faida ya 1M kwa miezi 6 wakati kuna biashara ukiwa na 5M kila mwezi unatengeneza 1M.
Well said. Kununua mazao na kusubiri bei ipande kazi bure.

Bora kununua machine ya kuprorocess hayo mazao na kuuza.
In short kuyaongezea samani.

Biashara ya kununua na kusubiri bei ipande Ni ya stock markets tu.
 
Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,099
2,000
Biashara hubadrika unaweza ukaweka stock na ikakulipa vizuri lakini wakati mwingine ikakukata sana.

Biashara za kuuza unga ama mchele nazo zinaelekea kuwa ngumu kwa sababau ya ushindani unaotokana na watu wengi kujiingiza huko.

Nayakumbuka mabasi ya " kuku ni mali"
Mwenye haya mabasi alitajirika kwa biashara ya kuku.

Changamoto ni masoko. Hapo panahitaji uhunifu na ndipo panakukumbusha umuhimu wa kuwa na network nzuri.

Lazima akili yako iwaze ni mahali gani patahitaji nini kwa kipindi kipi na pengine kwa muda gani. Halafu ufikirie namna ya kufikisha bidhaa zako kule.
 
Capital G

JF-Expert Member
Jul 2, 2017
1,631
2,000
Nadhani biashara ya kununua mazao na kuweka stock huifahamu, unaisikia tu. Ni biashara moja ya kipumbavu sana. Unaweza nunua mpunga wa 5M ukaa miezi6 ukauza ukapata faida ya 1M fikiria mtaji wa 5M upate faida ya 1M kwa miezi 6 wakati kuna biashara ukiwa na 5M kila mwezi unatengeneza 1M.
Tutajie basi mkuu hizo biashara tujifunze
 
Capital G

JF-Expert Member
Jul 2, 2017
1,631
2,000
Well said. Kununua mazao na kusubiri bei ipande kazi bure.

Bora kununua machine ya kuprorocess hayo mazao na kuuza.
In short kuyaongezea samani.

Biashara ya kununua na kusubiri bei ipande Ni ya stock markets tu.
Mashine zake ni bei gani mkuu?
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,048
2,000
Salute wakuu !!

KARIBU kwenye Jukwaa letu la Biashara, Uchumi na Ujasiriliamali. Leo nimekuandalia Biashara 10 ambozo ukizifanya zinaweza kukuleta mafanikio makubwa sana.

TUENDELEEE!

Biashara Kumi (10) Unazoweza Kuanzisha na Kufanikiwa Kimaisha.

Mwaka huu 2020 ni mwaka ambao moja ya malengo ambayo kila mtu anapaswa kuwa nayo ni malengo ya kibiashara. Kama bado hujawa na biashara basi unapaswa kuanza biashara yako mwaka huu. Na kama tayari una biashara, basi unapaswa kuikuza zaidi biashara yako mwaka huu 2020.

Nyakati zinapokuwa ngumu, usikazane kuwa na biashara ya kipekee, ambayo unahitaji kuanza kumshawishi mteja kwa nini anapaswa kununua unachouza. Ukishaona biashara unayofanya au unayotaka kufanya inakubidi uanze kumshawishi mteja kwa nini anapaswa kununua, hapo upo njia mbaya. Mteja anapaswa kujua tayari kwa nini anapaswa kununua, na avutiwe kununua kwako kwa huduma nzuri unazotoa.

1. Bidhaa za chakula.

Kwa kuwa watu bado wanakula, na wataendelea kula siku zijazo, kuanza biashara ya kuuza bidhaa za chakula ni hatua sahihi kwako kuchukua. Hapa unaweza kuuza na kusambaza bidhaa za chakula kama nafaka, mafuta na bidhaa nyingine muhimu.

Angalia uhitaji wa bidhaa za vyakula kwa wale wanaokuzunguka au unaoweza kuwafikia kisha wapatie bidhaa hizo kwa kiwango na gharama ambazo wanaweza kumudu huku wewe ukipata faidia ili biashara iweze kuendelea.

Uzuri wa biashara ya bidhaa za chakula unaweza kuanza na mtaji kidogo, ukatafuta bidhaa zilizo bora na kuweza kuwasambazia watu kule walipo.

Biashara ya mchele, mahindi, maharagwe na nafaka nyingine zina uhitaji mkubwa kwa watu.

2. Huduma za chakula.

Biashara nyingine unayoweza kuanza kwa mafanikio mwaka huu 2020 ni biashara ya utoaji wa huduma za chakula. Hapa unatengeneza na kuuza chakula bora ambacho watu wanaweza kukimudu.

Uzuri wa biashara hii ni kwamba, watu wengi wanabanwa na kazi au biashara zao na hivyo hawawezi kuandaa vyakula vyao, hasa vya mchana. Hivyo kwa kuwajua watu wa aina hii na namna unavyoweza kuwafikia, unaweza kuwapatia chakula ambacho ni bora kwa gharama wanazoweza kulipia.

Kingine muhimu ni kwamba watu kwa sasa wanajali sana afya zao, hivyo wanakula mlo bora, unaweza kutumia nafasi hii kutoa vyakula bora kiafya badala ya vyakula vya haraka ambavyo siyo bora.

Unaweza pia kutoa huduma ya matunda, juisi na huduma nyingine za chakula kwa wale wenye uhitaji.

3. Bidhaa za mavazi.

Kama ambavyo tumeona, watu wanaendelea kuvaa nguo, bila ya kujali mambo ni magumu au la. Hivyo unaweza kuingia kwenye biashara kwa kutoa bidhaa za mavazi. Hapa unauza mavazi kama nguo, viatu na mengineyo.

Unachohitaji hapa ni kujua uhitaji wa watu kwa wakati mbalimbali. Kwa mfano kipindi cha mwanzo wa mwaka bidhaa nyingi za mavazi zinazotoka ni zile zinazohusiana na mavazi ya shule. Pia katika kipindi cha sikukuu, watu wanajibana wawezavyo ili wavae nguo mpya.

Unapochagua kuingia kwenye biashara hii ya bidhaa za mavazi, angalia aina ya watu ambao ni wanunuaji wazuri. Mfano mavazi ya wanawake na watoto yanatoka zaidi kibiashara kuliko mavazi ya aina nyingine.

Uzuri wa biashara ya bidhaa za mavazi ni kwamba, unaweza kuianza kwa hatua ndogo sana, huhitaji hata kuwa na eneo la biashara. Unaweza kuchagua wateja unaowalenga, ukachagua bidhaa zao kisha kuwasambazia au kuwatangazia kwa njia ya mtandao.

4. Biashara ya huduma za mavazi.

Huduma za mavazi ni aina nyingine ya biashara unayoweza kuanza, ambayo itakuwezesha kupiga hatua kubwa. Kama una ubunifu wa mavazi, au unaona uhitaji wa mavazi ya aina fulani, unaweza kutoa huduma ya kuandaa mavazi hayo.

Hapa tunazungumzia kutoa huduma ya kuwaandalia watu mavazi kwa namna wanavyoyataka. Pia kuwasaidia watu kurekebisha mavazi yao. Biashara hii unaweza kuifanya kama unao ufundi wa kutengeneza mavazi. Lakini hata kama huna, unaweza kupata mtu mwenye ufundi ukawa unampa maelekezo na wewe kuwa na kazi ya kutafuta masoko au kusambaza yale mavazi yanayotengenezwa.

Siku hizi zipo mashine ambazo ni rahisi kutumia kushona mavazi ya aina mbalimbali ambazo unaweza kuwa nazo na kuanza kiwanda chako kidogo cha mavazi.

5. Ufugaji wa kibiashara – kuku.

Hakuna familia ya asili ya kiafrika ambayo haijawahi kufuga kuku. Na kuku ni moja ya biashara ambayo soko lake halijawahi kuyumba. Zimekuja biashara za ndege wa aina mbalimbali kama kware lakini zimepita na kuacha biashara ya kuku ikiwa imara. Huhitaji kumshawishi mtu kwamba anahitaji kula nyama ya kuku, au kula mayai, ni kitu ambacho kwa wengine ni ufahari.

Unaweza kuingia kwenye ufugaji wa kibiashara na kufuga kuku ambao utaweza kuuza mayai, kuuza vifaranga na hata kuuza kuku wenyewe. Unaweza kufuga kuku wa kienyeji, kuku chotara na hata kuku wa kisasa kabisa. Unachohitaji kuangalia ni uwezo wako na uhitaji wa soko unalolenga.

Uzuri wa ufugaji wa kuku ni kitu unaweza kuanza kwa hatua ndogo na kukuza. Pia unaweza kufanya huku ukiendelea kufanya vitu vingine. Pia itakuhitaji uwe makini ili ufugaji wako ukue.

6. Ufugaji kibiashara – samaki.

Samaki ni chakula kingine ambacho kina uhitaji mkubwa sana kwenye jamii zetu. Ni mboga ambayo ina uhitaji mkubwa na hivyo ukiweza kuzalisha kwa kiwango kizuri, ni biashara nzuri kwako kufanya.

Ufugaji wa samaki kwa sasa umerahisishwa kutokana na upatikanaji wa huduma muhimu za samaki. Huduma kama vyakula vya samaki, ujenzi bora wa mabwawa ya kufugia samaki zimefanya ufugaji wa kibiashara wa samaki kuwezekana.

Japo ufugaji wa samaki unahitaji mtaji mkubwa, inawezekana pia kuanza kidogo na ukafanya vizuri.

7. Kilimo biashara – mbogamboga na matunda ya muda mfupi.

Hata kama uchumi ni mgumu kiasi gani, watu hawatakula chakula bila ya kitunguu, bila ya nyanya, bila ya bamia. Watu wataendelea kula mchicha, matembele na mboga nyingine. Na muhimu zaidi matunda kama matango, matikiti maji na hata ndizi ni vyakula ambavyo kila mtu ana uhitaji navyo.

Hivyo eneo unaloweza kuingia kibiashara mwaka 2020 kulingana na nafasi na uwezo wako ni kilimo biashara cha mbogamboga na matunda ya muda mfupi. Ninaposema kilimo biashara namaanisha ulime kwa lengo la kuuza, hivyo kulima kwa viwango vizuri na ubora ambao unakubalika na soko unalolenga.

Unaweza kulenga wanunuaji wa rejareja au kuuza kwa wanaonunua jumla, kama mahoteli au maduka makubwa.

8. Kilimo biashara – mazao ya chakula.

Mazao ya chakula kama nafaka, mahindi, maharagwe na mpunga ndiyo mazao yanayoongoza kwa kuliwa sana kwenye jamii zetu. Hivyo hili ni eneo ambalo unaweza kuingia kibiashara na ukafanya vizuri kwa mwaka huu 2020. Unaweza kuingia kwenye kilimo moja kwa moja na ukalima kibiashara, kwa njia ambayo utazalisha kwa kiwango kikubwa na kwa ubora wa kuweza kuuza.

Lakini pia kama huwezi kulima, kwa kukosa nafasi au usimamizi mzuri, unaweza kununua mazao hayo kwa wingi kwenye msimu wa mavuno, kuyaongeza thamani na kuyauza kwa wahitaji. Mfano kununua mpunga wakati wa mavuno, kuukoboa, kuuhifadhi kwenye vifungashio vizuri na kuuza kwa watumiaji ni biashara ambayo inaweza kukupeleka kwenye mafanikio makubwa 2020.

9. Biashara ya vyakula vya mifugo na huduma zake.

Watu sasa wanafuga, kuanzia kuku, mbuzi, ng’ombe, sungura, samaki na kadhalika. Unaweza kuingia kwenye biashara kwa kutoa huduma mbalimbali za kuwezesha wafugaji kupata mafanikio kwenye ufugaji wao.

Hapa unaweza kuingia kwenye biashara ya kuuza vyakula vya mifugo, kuuza madawa na virutubisho vya mifugo na hata kutoa huduma za vyakula mbadala kwa wafugaji.

Na kama wewe ni mfugaji au una utaalamu kuhusu mifugo, unaweza kutoa ushauri kwa wafugaji kibiashara pia.

10. Huduma za ushauri wa kitaalamu.

Kwa jambo lolote ambalo umesomea, au umeshakuwa na uzoefu nalo, kuna watu ambao wamekwama na hawajui wafanye nini. Hapa unaweza kuingia kwenye biashara ya kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa lile eneo ambalo una utaalamu au uzoefu nalo.

Kama umesomea mambo ya afya unaweza kutoa ushauri wa kiafya kwa watu na wakakulipa. Kama umesomea au una uzoefu kwenye biashara, unaweza kuwashauri watu kuhusu biashara na wakakulipa.

Angalia kipi unajua na watu hawajui, kisha wape ushauri kwa njia ambayo watakulipa.

Asante.

Katika hizi wewe unaifanya ipi mkuu
 
ngongoti2000

JF-Expert Member
Nov 20, 2017
1,998
2,000
Mkuu acha uongo , Sasa hivi ifakara wanauza gunia moja la mpunga la kilo 100 kwa shilingi 60,000 ... Kwa hiyo ukiwa na milion 5 unachuua magunia 84 hivi.

Mwezi wa kumi na mbili gunia huuzwa mpaka laki 1 na ishirini.

Gharama yako ni kuweka stoo huko ifakara ambapo ni tsh 2000 kwa gunia moja ambapo Ni lifetime cost.

Ninachojua mpunga unaweza kukurejeshea hela yako almost Mara 2.
Wakatii unataka kuuza mchele kwa bei ya juu...kuna watu wanaingiza mchele toka nje halafu kilo 700.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom