Bidhaa mpya kwenye soko la filamu tz zenye maudhui ya utalii tu(siyo Bongo movie na wala hazifanani)

Apr 11, 2017
21
2
Bidhaa ya kwanza(filamu yenye maudhui ya utalii kwa 100%) yenye lugha ya kiswahili ( siyo ya kutafsili) inatambulishwa sokoni ikiwa imerekodiwa na mzawa kutoka katika mbuga mbalimbali zilizopo hapa nchini.

Itaanza kupatikana sokoni mnamo tarehe 15/5/2017 kwenye maduka yanayouza filamu au kwa watembeza filamu mtaani kwa bei ya sh 2000 tu.

Utalii entertainment ina lengo la kufikia hatua ya kila unapoizungumzia sekta ya utalii hapa nchini basi unalazimika kuitaja na utalii entertainment kama mdau namba moja.

Kwa sapoti yako tunaweza kulifikia lengo hili na kuikuza sekta ya utalii wa ndani zaidi ya ilivyo sasa.

Tunapokea maoni ushauri,ushilikiano wa aina yeyote na hata kuwekeza pamoja pia( ila suala hili litahitaji mazungumzo ya kina kwanza) ili wote tusonge mbele.MUNGU AWABALIKI WOTE.
 

Attachments

  • IMG_20170430_203337.jpg
    IMG_20170430_203337.jpg
    144.2 KB · Views: 25
Tunaisubiri, kama poa tutashiriki kuisambaza mtandaoni wazungu na waarabu walete "the greens"...
 
Hamna vichekesho vya Bongo movie huko kweli??
Hiki ndicho kiwango cha kufikili cha vijana wa kitanzania,siku zote wanawaza kwenye mabaya tu,kabla hatuwasaidia watu kama hawa jamno lolote kwanza inabidi tubadilishe uwezo wao wa kufikili ikibidi hata kuwashikia akili zao mpaka pale watakapo jielewa ndo tuendelee mbele .
 
Hiki ndicho kiwango cha kufikili cha vijana wa kitanzania,siku zote wanawaza kwenye mabaya tu,kabla hatuwasaidia watu kama hawa jamno lolote kwanza inabidi tubadilishe uwezo wao wa kufikili ikibidi hata kuwashikia akili zao mpaka pale watakapo jielewa ndo tuendelee mbele .

Jibu swali sio unaleta hoja zisizo na mashiko..nimekuuliza swali simple sana unazunguka...sasa usiponijibu vyema utanishawishije kununua bidhaa yako?? au ndivyo ulivyofundishwa kujibu wateja wako hivyo......??
 
Back
Top Bottom