Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,096
- 22,627
Kweli kabisa.. me kama hizi kampuni za simu natamani watokee wawekezaji kutoka nje zije kampuni hata 10 zaidi, hawa waliopo washike adabu.....Ishu sio uwezo wa kutengeneza tu ishu ipo kwenye bei.
Saruji inatengezwa TZ ila Saruji inayotoka nje inauzwa kwa bei rahisi au sawa na inayozalishwa hapa TZ au Sukari. Kwanini iwe hivyo?
Halafu TZ kuna ufa.la flani unafanyika, leo ukisema saruji zisiingie kutoka nje kwa sababu tunayzalisha ya kutosha, huchelewi kuona saruji imepanda, tena kampuni zote wanapandisha pamoja, ushindani wa biashara hamna ila kuna janja janja tu.
Kama mitandao ya simu, utakuta yote yanakupa 1GB kwa buku 2. Makampuni ya ndani hayashindani bali yanakaa kitako na kuamua kuumiza wananchi tu. Bora kama nje kipo rahisi kije tu nchini mpaka na wao watakapoamua kushindana