Bidhaa gani ambayo Serikali inaweza kukataza isiingizwe nchini, ambayo Watanzania wanaweza tengeneza?

Ishu sio uwezo wa kutengeneza tu ishu ipo kwenye bei.

Saruji inatengezwa TZ ila Saruji inayotoka nje inauzwa kwa bei rahisi au sawa na inayozalishwa hapa TZ au Sukari. Kwanini iwe hivyo?

Halafu TZ kuna ufa.la flani unafanyika, leo ukisema saruji zisiingie kutoka nje kwa sababu tunayzalisha ya kutosha, huchelewi kuona saruji imepanda, tena kampuni zote wanapandisha pamoja, ushindani wa biashara hamna ila kuna janja janja tu.

Kama mitandao ya simu, utakuta yote yanakupa 1GB kwa buku 2. Makampuni ya ndani hayashindani bali yanakaa kitako na kuamua kuumiza wananchi tu. Bora kama nje kipo rahisi kije tu nchini mpaka na wao watakapoamua kushindana
Kweli kabisa.. me kama hizi kampuni za simu natamani watokee wawekezaji kutoka nje zije kampuni hata 10 zaidi, hawa waliopo washike adabu.....
 
Zipo bidhaa zinazotengenezwa na kupatikana nchini lkn bado aina hio hio ya bidhaa inaingia kutoka nje.
kwanini?
Kwa sababu serikali haimpi mfanyabiashara favourable conditions za kudeal na bidhaa za ndani.

Ikumbukwe kuwa mfanyabiashara ni mtu anayeangalia urahisi wa yy kupata faida. Hivyo anapowekewa conditions ngumu za kufanya biashara yake kwa bidhaa zilizopo nchini, huangalia namna nyingine ya kumpa urahisi wa kupata faida.

Mfano Sukari. Bidhaa hii huzalishwa kwa wingi sana nchini, lkn bado inaingizwa kutoka malawi.

Ni ngumu sana kwa mfanyabiashara kuchukua mzigo wa sukari kutoka morogoro na kuisafirisha hadi Kyela then auze kwa bei elekezi.
Hapo atachezea hasara. Hii hupelekea sukari kutoka malawi ijulikanayo kama Tseketseke kuingia na kuuzika sana kwa maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom