Bidhaa ambayo inatoa faida ghafi ya laki moja na zaidi kwa kila pc

Sa 7 mchana

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
4,975
9,721
Habari zenu wapambanaji,

Naomba kujuzwa bidhaa ambazo inaweza toa faida ghafi ya laki moja au zaidi kwa pc na huku mimi nikiinunua pamoja na usafirishaji niwe nimetumia laki moja au pungufu ya laki kwa kila pc.

Bidhaa iyo haijalishi iwe inapatikana nchini mwetu au kuagizwa.

Asante
 
Kama ni wakike au jinsia yako inautata. Aaah sijui hata nilitaka kuandika nini.
Uuzaji wa bangi mkuu una faida nzuri
 
Habari zenu wapambanaji,

Naomba kujuzwa bidhaa ambazo inaweza toa faida ghafi ya laki moja au zaidi kwa pc na huku mimi nikiinunua pamoja na usafirishaji niwe nimetumia laki moja au pungufu ya laki kwa kila pc.

Bidhaa iyo haijalishi iwe inapatikana nchini mwetu au kuagizwa.

Asante
Hahaha unapenda sana mtelezo kijana utumie laki upate laki kwa pic? Aloo lbda bangi
 
Hakuna biashara halali inayoweza kukupa faifa kubwa namna hiyo katika entry level..
Labda ufanye biashara za magendo , kwenye biashara anza na items zenye faida kidogo then work your way up kwemye mafaida ya makubwa makubwa .
 
Nimependa hii idea, naomba ufafanuzi zaidi mkuu...
kwaufupi, pita madukani mahali ulipo/tafuta muuza duka mzoefu hakupe list ya bidhaa
Then, ........chunguza bidhaa zipatikanazo ambazo haziozi agiza kwa bei ya jumla weka ndani haina haja ya kufungua duka we wasambazie wauze wenyewe huku ukisubiri marejesho ya wiki
Jamaa kafanya hivyo kwa miezi michache now Mashallah amesimama kiuchumi maradufu
N.B. ni moja yakukimbia kodi hivyo ni hatari kwa afya yako ya akili fanya kwa umakini
 
Habari zenu wapambanaji,

Naomba kujuzwa bidhaa ambazo inaweza toa faida ghafi ya laki moja au zaidi kwa pc na huku mimi nikiinunua pamoja na usafirishaji niwe nimetumia laki moja au pungufu ya laki kwa kila pc.

Bidhaa iyo haijalishi iwe inapatikana nchini mwetu au kuagizwa.

Asante
Maswali mengine bwana khaaaa!!!
Haya! Fanya biashara hii: agiza magari, caterpillar, transformer, ultrasound (medical) na mashine za kisasa za hospital, meri, ndege, n.k. Nadhani hapo utapiga hela ndefu
 
Moja kati ya makosa makubwa ya watu wanaoanza biashara ni kufikiria kwanza faida kabla ya biashara yenyewe..

Mkuu, biashara haiko hivyo.
Ukitaka kufanya biashara kaa chini tathmini mambo yafuatayo;
1.Unapenda kufanya nini?
2.Mahitaji ya jamii inayokuzunguka ni nini? (utafiti)
3.Watu ambao wako kwenye mzunguko wako na wanaweza kukusaidia (connection)
4.Mtaji ulionao ni kiasi gani na unatosha kuanza kwa ukubwa upi?

Faida (either kubwa au ndogo) ni matokeo ya nguvu, juhudi, maarifa, ufanisi, ubunifu na ujuzi uliyoweka kwenye biashara yoyote uliyoamua kufanya baada ya kutafakari kwa kina mambo manne (4) niliyotaja hapo juu.

Natamani ungenielewa!
 
Back
Top Bottom