Njia moja ya uhakika ya kufanya wateja wakuamini na wakupe pesa!

Seif Mselem

JF-Expert Member
Oct 16, 2023
257
441
Kama umekuwa Kwenye Biashara kwa Muda mrefu na umekuwa Ukitafuta ni...

Jinsi gani ya Kuwafanya Wateja wako Wakuamini na wakupe HELA Zao bila Kipingamizi chochote Basi Makala hii kwako ni Zaidi ya Biriani Kuku.

Kwasababu...

Naenda kukuonesha SENTENSI Moja tu ambayo Itakupa...

Uaminifu Sokoni na Hauta waza tena Kuhusu Washindani wako!

...Ungana na Mimi humu ili Nikuonyesha hatua kwa hatua Jinsi Inavokuwa...

Ukweli ni Kwamba...

Kwenye SOKO la Sasahivi kumekuwa na Shida kubwa ya Wateja kutokuamini Wauzaji wa bidhaa au huduma Mbalimbali hasa Wajasiliamali wadogo wadogo wanaoingia sokoni.

Na...

Hii imetokana na baadhi ya Wauzaji wachche kutokuwa Waaminifu kwa Wateja wao na nikutoka na Biashara nyingi kuwa zinafanyikia Mtandaoni (Online)

ILA...

Leo hapa Nitaenda kukupa Sentensi moja Iliyobeba NGUVU yote ya Imani kwa Wateja wako

Sentensi hiyo Moja ni hii Hapa chini

Inasema Hivi...

"If I Can Make them that [My New Opportunity] is the Key [What they Desire Most] and...

Is only Attainable through [My Specific Vehicle] then all other Objections and...

Concerns becomes Irrelevant and they have to give me Money"

Usihangaike... Nimekuwekea Kila kitu Hapa chini

Inakuwa Hivi...

"Ikiwa Naweza Kuwafanya kuwa [My New Opportunity] ndio Ufunguo [What they Desire Most] na...

Inaweza Kufikiwa tu kupitia [My Specific Vehicle] kisha Vipingamizi vingine Vyote na...

Wasiwasi utakuwa Hauna maana na Lazima wanipe Pesa"

Najua itakuwa Bado Unajiuliza huyu Mselem anaongea Ma nini Leo!

Usijali angalia Tena hapa Utanielewa Vizuri zaidi...

Sijabadili maana ya Maneno ya kwenye Mabano kwasababu Utaenda kuona maana yake Ndani ya Sekunde moja hapa...

Tunaposema...

My New Opportunity: Ni vile vitu Ambavyo bidhaa au huduma Yako inavitoa kwa Mteja wako.

What they Desire the Most: Ni yale Matokeo ambayo Wateja wako Wanayahitaji Kila siku.

Na...

My Specific Vehicle: Ni ile bidhaa Yako sasa ambayo Unaiuza wewe kama Mjasiliamali.

Ukiweka na Mifano yake kabisa Itaonekana Hivi

My New Opportunity: Inaweza Ikawa...

Kukuza Nywele, Kuondoa Chunusi, Kutoa Harufu, Kupunguza Uzito n.k

Halafu...

What they Desire the Most: Inaweza Ikawa ni...

Kupendwa zaidi, Kuwa Wazuri, Kuwa wenye Furaha, Kuwa na Sex Body n.k

Halafu kwenye Hiyo ya Mwisho ni...

My Specific Vehicle: Inaweza Ikawa...

Mafuta ya kukuza Nywele, Dawa ya Meno, Sabuni, Program flani ya Mazoezi n.k

Sijui Umeona Jinsi Inavyoenda Sasa?..

Yeah...VIZURI!

Kwahiyo sasa kama Utaviweka hivo Vitu kwenye ile Sentensi pale juu.

Swala la Wateja wako Kukuamini na Kukupa Pesa unayotaka Litakuwa halipingiki

Kwasababu...

Utakuwa umewapa AHADI Ambayo hakuna mahala wanaweza Kuipata.

Kwahiyo...

Cha kufanya chukua Sasahivi kalamu na karatasi halafu Jaza kama Nilivyofanya

Halafu uangalie Jinsi gani Inakuwa kwenye Biashara yako...

Unaweza kunitumia pia Nikuangalizie kama kuna Mahali utakuwa Unakwama.

Na...

Hivyo Ndivyo Unafanya Wateja wako Wakuamini kwa Kuwapa AHADI Kubwa Kuliko Washindani zako.

I Hope Umejifunza Kitu Japo kwa Uchache.

Uwe na Siku Njema!

Gracias

Seif Mselem
 
Nakunukuu " Utakuwa umewapa AHADI Ambayo hakuna mahala wanaweza Kuipata"

Hapa ndio kwenye changamoto. Yaani bidhaa au huduma yako iwe inahitajika na hakuna mahala pengine inaweza kupatikana. Hapa ukiweza kufika ina maana utakua na 'monopoly' yaani utakua na uwezo mkubwa kwenye soko kuliko wapinzani wako.
 
Hapo nataka unipe Hilo neno la kuaminiwa niwe nawaambia wateja wanipe Hizo Hela
Wape "AHADI" Kubwa kama Mungu Alivyotupa Ahadi kwa Watu watakaotenda Mema Duniani.

Yaani...

Jiulize ni Kitu gani ambacho Bidhaa/Huduma yangu Inatatua kwa Uhakika Zaidi... Hicho Ndicho Unakiahidi kwa Walengwa wako a.k.a Wateja wako.

Wewe Jiulize kwanini Unaendelea Kumpa Vitu ambavyo Unampa Kila Siku Mume/Boyfriend wako?

Hiyo Vitu ni Sawa na PESA kwenye Biashara na Unampa Kwasababu Ametimiza AHADI Aliyokwambia Kipindi Mnakutana.

SIMPLE. LIKE. THAT!

Kama bado Hujanielewa Kabisa Nitumie Meseji WhatsApp yenye Neno "E" Naweza Kukupa Nafasi Nikakuelekeza kwenye Simu.
 
Nakunukuu " Utakuwa umewapa AHADI Ambayo hakuna mahala wanaweza Kuipata"

Hapa ndio kwenye changamoto. Yaani bidhaa au huduma yako iwe inahitajika na hakuna mahala pengine inaweza kupatikana. Hapa ukiweza kufika ina maana utakua na 'monopoly' yaani utakua na uwezo mkubwa kwenye soko kuliko wapinzani wako.
Exactly Percival... I Hope Wewe ni Moja ya Watu Umenielewa Vizuri zaidi.

Safi Sana Brother
 
Wape "AHADI" Kubwa kama Mungu Alivyotupa Ahadi kwa Watu watakaotenda Mema Duniani.

Yaani...

Jiulize ni Kitu gani ambacho Bidhaa/Huduma yangu Inatatua kwa Uhakika Zaidi... Hicho Ndicho Unakiahidi kwa Walengwa wako a.k.a Wateja wako.

Wewe Jiulize kwanini Unaendelea Kumpa Vitu ambavyo Unampa Kila Siku Mume/Boyfriend wako?

Hiyo Vitu ni Sawa na PESA kwenye Biashara na Unampa Kwasababu Ametimiza AHADI Aliyokwambia Kipindi Mnakutana.

SIMPLE. LIKE. THAT!

Kama bado Hujanielewa Kabisa Nitumie Meseji WhatsApp yenye Neno "E" Naweza Kukupa Nafasi Nikakuelekeza kwenye Simu.
Nimekupata fresh.....umeeleweka nadhani na lugha ya malkia ilinichanganya
 
Back
Top Bottom