Bibi kuozesha mjukuu wake wa kike imekaaje!!

Mremaaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
293
Reaction score
325
Ndugu wanajamvi habarini za asubuhi nawasalimu nyote itifaki imezingatiwa, kwa mliopo kwenye majukumu poleni na hongereni kwa majukumu.

Naja mbele zenu tena great thinkers kuomba ushauri , miezi kadhaa nilileta uzii mbili tofauti

"1.Huyu mwanamke nipige chini au nivulie mpaka ndoa?
2.Mama anataka nione Baba hataki nione"

Nashukuruni sana wakuu mlinishauri vizuri sana na hata sasa katika hili nategemea ushauri wenu.

MADA:
Siku chache zilizopita nilikuwa mkoa X kikazi na ndio mkoa anaotokea mchumba (wife to be ) wakati nikiwa huko na yeye alipata likizo na kuja kwao ambapo bado mim nilikwepo, nilipomaliza kazi niliyokuwa nayo kàbla ya kurejea nyumbani tulikutana tukawa pamoja lakini akawa anasisitiza nikasalimiane na bibi yake (ndiye aliyemlea tangu akiwa mdogo na mim nilipata kukutana na huyu bibi yake mara moja alipomtembelea) mim sikuona shida kusalimiana naye maana tulifahamiana kabla, mwanaume nikachukua tax mpaka kwa bibi mtu.

Nilipofika nilimkuta bibi mwenyewe na wazee wengine wawili tulisalimiana baadaye binti akaambiwa tutambulishe huyu nani?, binti akawaambia huyu ni mchumba wangu, bibi mtu akaanza kuuliza tunakuja lini kwa shughuli husika? Nilibaki nimeduwaa sababu hata taratibu kwa wazee wangu hazijaanza na ukizingatia mim nipo kikazi sikwenda kwa ajili ya hilo, nikashindwa kujibu mwisho wale wazee wakaanza kueleza taratibu za kufuata " ukizingatia mim ndo naambiwa taratibu sijawahi kuona" Sikujibu lolote.

Ila binti alijua nimechukia japo sikumwonyesha kuchukizwa au kukerwa na kilichotokea, na wala sikuliongelea kilichotokea mpaka sasa ( Inavyooneka ilikuwa mpango wa bibi na mjukuu wake ili wakamilishe adhama yao haraka iwezekavyo) ndugu zangu naombeni ushauri sababu nashangaa kinachofanya haraka yote hiyo ni nin akati nilishamwambia taratibu hazijaanza kwanin afanye hivyo? (Wazazi wake wote wapo na mama yake mzazi tunawasiliana")

"Naombeni hekima na busara zenu katika kunishauri mwana jamvi mwenzenu naomba kuwasilisha"

Niwatakie majukumu mema!!!!
 
oa tu mkuu, acha kujishauri shauri, usimpotezee muda binti wa watu
 
Wewe unataka kuoa au unataka upewe tu umlee? Acha kujiuliza uliza vuta jiko, bibi anataka akutunuku we unalemba
 
Mi mbona sion cha kukushaur hapo mkuu kwan nan asiopenda ndugu yake mwanae mjukuu asiolewe kwa hiyo we lengo lako ugonge tu na hata sion kilicho kuchukiza hapo
 
Hilo ni jambo la kawaida asa mabibi maana ingelikuwa ni ajabu kama bibi asingeli kuuliza utakuja kuoa lini?, kwa maana nyingine bibi kutokuuliza ni kualalisha zinaa kati yenu.Kumbuka wewe ni Kutoka jamii ya ktanzania na hatuna hiyo tabia ya kwenda kwa familia ya mwanamke huku hujajulikana kama mchumba aliekwisha toa posa.

hakuna baya hapo kama unampenda huyo binti anza taratibu vinginevyo kila mara utakapokwenda kwa huyo bibi utaulizwa swali hilo hilo mpaka pale mtakapo oana.
 
Unaenda kikeni hujawa tayari kuoa, mbona umejitafutia balaa mwenyewe
 
Sasa kilichokukasirisha nini??? Acha ujinga si ungesema nitaoa mwakani. Pwaguzi we
 
Angalia muzee, bora kuchelewa kwenye furaha kuliko kuwahi kwenye kilio
 
Back
Top Bottom