Bibi Harusi apata ajali akienda kuolewa

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,675
Hii imetokea maeneo ya Korogwe Tanga,bibi harusi akiwa na ndugu na Sheikh wa "shughuli" wamepata ajali ktk gari aina ya NOAH.Katika ajali hiyo Bibi Harusi amepata maumivu ya kifua,wengine wametoka salama na michubuko ya hapa na pale.Sheikh wa shughuli amepata michubuko kidogo na kanzu kuchanika sehemu ya mikononi.Wapambe wengine wa bibi harusi wana michubuko ya hapa na pale.

Shughuli imehairishwa mpaka wakati mwingine utakapoonekana unafaa,Wali na vyote vilivyopikwa maalumu kwa shughuli vimewekwa kando na kugawiwa raia waliokuwepo karibu,shughuli imeingia dimbwini,mpaka wakati mwingine.Dereva wa gari amekimbia na kutokomea porini kusikojulikana.Ni taharuki kwa bibi harusi na bwana harpsichordist
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
 
Doh.... kwa wale wenye imani zao.... huyo mwali ndo kwaheri tena ndoa.

Ataisikia kwa wenzake tu.
 
Pole yao. Ila kila ajali ikitokea dereva kama anajiweza ni lazima akimbie?
 
Doh.... kwa wale wenye imani zao.... huyo mwali ndo kwaheri tena ndoa.

Ataisikia kwa wenzake tu.

Labda alimfanyia mwenzie magirini akaolewa yeye.......sasa yamemkuta.......
 
Back
Top Bottom