Matokeo ya jana Kiboko;
Ni kama Binti kukimbia na shela Ukumbuni;
Kurudi kwa wazazi wake.
Hii inaweza kuwa ni uzembe wa Mwanaume aliyetaka kuoa
Au ni ushujaa wa BInti kuweza kumtoroka Nyamaume.
Family ya Mr &Mrs y.manji inawaomba radhi kwa wanachama,wapenzi na mashabiki wote wa dar young African kwa tafrija iliyoshindwa kufanyika baada ya bibi harusi mtarajiwa KUKIMBIA UKUMBUNI MUDA MFUPI BAADA YA IBADA TAKATIFU ILIYOONGOZWA NA I.NKONGO MAJIRA YA SAA 11JIONI.MAELFU YA WATU WALIKUWA WAKIFUATILIA KWA UMAKIN KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI.MAONGEZ BADO YANAENDELEA KWA MWAKAN ILI TUWEZE KUENDELEA NA TAFRIJA YETU KWAN BIBI HARUSI(SIMBA)AMEOMBA RADHI KWA DHARAU ALIYOTUFANYIA NA AMEOMBA TUMUACHE AMALIZIE MASOMO YAKE.SHUKRANI KWA WOTE WALIOJITOKEZA.
Matokeo ya jana Kiboko;
Ni kama Binti kukimbia na shela Ukumbuni;
Kurudi kwa wazazi wake.
Hii inaweza kuwa ni uzembe wa Mwanaume aliyetaka kuoa
Au ni ushujaa wa BInti kuweza kumtoroka Nyamaume.
Ngassa alichofanya alinogesha utani wa Simba na Yanga. Na kama Simba wangekuwa wajinga basi wangejifanya kumkaba Ngassa ili asifunge kitu ambacho kingewaghalimu zaidi, maana inawezekana baada ya kuwa chini ya ulinzi Ngassa asingefunga lakini kuna watu kama Kiiza na Kavumbagu wangeweza kusababisha madhara makubwa maana wangeweza kutoka na hat trick hata mbilimbili endapo Simba wangeingia kwenye mtego wa Ngassa. Hii ndiyo ambayo imewatokea Yanga kwa mtego wa Mzee Akilimali. Mzee Akilimali si Kocha ila nashawishika kuamini kuwa ni Mganga Mjanja Mjanja wa Kienyeji ambaye aliyatamka maneno ya bao tatu na ikatokea timu ikapata mabao hayo na wachezaji wakatumbukia katika trick yake wakiamini kuwa magoli yale ni ya Mzee Akilimali hivyo hakuna haja ya kuongeza mengine. Mimi naamini kuwa kama Yanga wangekuwa makini na kupata bao la nne ndani ya dakika tano za kipindi cha pili, Simba wangeishiwa nguvu na wasingeweza kusawazisha.
Lakini kitendo cha wachezaji wake nyota (Yanga) kuacha kucheza mpira na kutukana benchi la ufundi la Simba, kuliwatoa mchezoni. Ni mechi ambayo kama Simba ingepata pia bao la nne basi ingeleta madhara na mtafaruku mkubwa sana Jangwani. Mchezo ule umetufundisha mengi na nafikiri ni makosa ambayo hayatakuja kurudiwa kwa pande zote mbili. Lakini yote kwa yote Simba wana haki kwa asilimia mia moja kusherehekea ushindi ule hata kwa wiki moja na mdundiko ukikesha! Ni jambo la nadra sana kutokea katika soka la Bongo. Imenikumbusha Manchester United na Liverpool pale mjini Liverpool mahasimu hawa walipotoka 3-3 enzi zile za kina Bruce Globelar na Gavana Paul Ince! Au kwenye kombe la Mataifa ya Afrika mechi ya mshindi wa tatu nafikiri kati ya wenyeji Burkina Faso na Congo DRC 1998. Wenyeji walikuwa wanaongoza 4-1 hadi dakika ya 81 na Wakongomani walikuja juu na kurejesha bao tatu zilizo baki na ngoma kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti na Simba wa Kabila kuibuka washindi. Mtangazaji aliyekuwa anatangaza mechi ya Bayern Munchen na Man U pale Camp Nou 1999, wakati Super Sub Ole Gunner Sosha akisawazisha na kisha baada ya muda kidogo Teddy Sherringham akimliza Sammy Osei Kuffor,
namkumbuka Mtangazaji wa mechi ile akisema namnukuu: FOOTBALL SOMETIMES IS A VERY, VERY, VERY CRUEL GAME! FEW MINUTES REMAINING TO THE ADDED TIME, MANCHESTER UNITED TWO, BUYERN MUNICH ONE, THIS IS UNBELIEVABLE! So mpira siku zote ni dakika tisini na hata zile za nyongeza nazo zinapaswa kuheshimiwa, ndiyo maana Simba waliziheshimu kwa kuzitumia kumuingiza Zahoro Pazi maana pale hata wao japo Yanga walichanganyikiwa lakini wangeweza kupata bao la nne!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.