Bibi aangua kilio

oba

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
310
65
Leo nilipoenda mhimbili hospitali kumwona ngugu yangu mgonjwa nilikutana na bibi mmoja akitokwa machozi na mama mmoja alipotaka kujua kulikoni alionesha cheti cha msamaha wa matibabu na kulalamika kuwa pamoja na cheti hicho hajapata matibabu ya dawa alizoandikiwa na daktari eti kwa kuwa hazipatikani katika pharmacy ya hapo hospitali ya taifa. Nilipomtazama kwa makini nikamfananisha na bibi mmoja aliyekuwa akishangilia hotuba ya JK juzi akifurahia na kumshangilia Raisi kwa kuwafanya madaktari kusitisha mgomo bila kujali kama madai yao ya kuboreshwa mazingira ya kazi na uwepo wa vifaa tiba yametekelezwa au la.
My take.
Tusifurahi madaktari kusitisha mgomo ila twapaswa kufurahi kuwa madai yao yametekelezwa vinginevyo sisi wananchi ndio tutakaoumia!!
 
Hata mie huyo bibi nilimwona; si alivaa t-shirt na kanga vya kijani vimeandikwa 'chagua ccm, chagua kikwete'?
 
Siku ile walipokuwa wanapewa hadithi za Hospitali za India walikuwa wamelewa shibe (pilau na soda). Sasa waache wapambane na uhalisia kwani walijisahau wakadhania wanamkataba na Mungu kuwa hawataugua wala kuuguza wapendwa wao.
 
safi sana madaktari huu ni muda wa kuwaambia wagonjwa ukweli ambao wao ungeliwapa ahueni katika matibabu yao
 
Madaktar na wafamasia huwa wanajisevia.Pengine dawa zimefichwa ndio mgomo baridi umeanza ili tuwa support wataalam wetu. Lakini ndugu mtoa mada inaonesha umefurahishwa na hilo tukio la huyo mama mtu mzima kutoa machozi...
 
Mimi naogopa sana endapo madr wameamua kurudi kazini huku wana vinyongo moyoni. Unajua mgomo baridi wa walimu madhara yake tutayaona baadaye wakati wa matokeo ya fm iv ambapo zaidi ya 50% division 0, lakini mgomo baridi wa matabibu usiombe. :scared:
 
Madaktar na wafamasia huwa wanajisevia.Pengine dawa zimefichwa ndio mgomo baridi umeanza ili tuwa support wataalam wetu. Lakini ndugu mtoa mada inaonesha umefurahishwa na hilo tukio la huyo mama mtu mzima kutoa machozi...

Mlinzi wa kwanza wa maslahi yako ni wewe mwenyewe, sasa ukichagua kuyatelekeza maslahi yako mwenyewe huku ukibeza juhudi za wanaotaka kukusaidia ufanyweje yakikukuta ya kukukuta? Mimi ningekuwa na uhakika ni yeye wala nisingemcheka tu, na kumzodoa ningemzodoa tena wazi wazi hadharani.

Na wewe aliekwambia wafamasia na madaktari wanatunza store za madawa hadi "wajisevie" ni nani? Au hospitali hazina maboharia siku hizi?
 
Leo nilipoenda mhimbili hospitali kumwona ngugu yangu mgonjwa nilikutana na bibi mmoja akitokwa machozi na mama mmoja alipotaka kujua kulikoni alionesha cheti cha msamaha wa matibabu na kulalamika kuwa pamoja na cheti hicho hajapata matibabu ya dawa alizoandikiwa na daktari eti kwa kuwa hazipatikani katika pharmacy ya hapo hospitali ya taifa. Nilipomtazama kwa makini nikamfananisha na bibi mmoja aliyekuwa akishangilia hotuba ya JK juzi akifurahia na kumshangilia Raisi kwa kuwafanya madaktari kusitisha mgomo bila kujali kama madai yao ya kuboreshwa mazingira ya kazi na uwepo wa vifaa tiba yametekelezwa au la.
My take.
Tusifurahi madaktari kusitisha mgomo ila twapaswa kufurahi kuwa madai yao yametekelezwa vinginevyo sisi wananchi ndio tutakaoumia!!

acha uongo. kwani uliwashika sura wale wote waliohudhuria kwa baba liz
 
Back
Top Bottom