Biashara ya vitenge ni black Diamond!?

Biashara ya vitenge ni black Diamond!?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,102
Reaction score
828,970
Kuna mikondo ya pesa wengi wetu hapa tunaisotea kwa udi na kwa uvumba! Wengine wanaroga kabisa ili waweze kuikamata. Kuna mitandao haramu ya biashara yenye faida za kufuru madini yanasubiri!

Vitenge biashara iliyohitaji elimu kubwa na uwekezaji wa wataalam ni biashara kubwa yenye mitandao ya kutisha inaguka kuwa biashara haramu sasa.. Maana watu wameshanogewa lakini mamlaka nazo sasa ndio zinakumbuka shuka asubuhi kukiwa kumeshapambazuka

Kuna nguvu ya kimamlaka inajaribu kuuvunja huu mtandao lakini bila kujitoa na kuongeza nguvu kubwa hawatafika popote. Watakamata vidagaa tuu na pumzi itakata
Ona hii magazijuto Kisha jiongeze!

Mwanamama kakamatwa Dodoma na mamlaka ya mapato kwa kosa la kutodai risiti ya mzigo wa vitenge alivyonunua .. Anashtakiwa kwa makosa mawili
1. Kutodai risiti
2. Kutotoa ushirikiano kwa maofisa alipotakiwa kuonesha mahali aliponunua mzigo

Huyu ni mbuzi wa kafara tuu... Hiyo mizigo wanaipata kimagumashi.. Mitandao ndio inafanya kazi..hakuna vituo rasmi ni kupeana juu kwa ju!

Siku mbili nyuma zimekamatwa gari na mzigo mkubwa wa vitenge mkoani lindi.. Mzigo haukuwa na nyaraka na ikasadikika ni mzigo wa magendo.. Mikwara mingi sana ikapigwa!

Mwezi uliopita zilikamwata container zenye mzigo wa kutosha wa vitenge .. Mzigo uliandikwa ni mashuka yako transit kumbe ni vitenge vinaenda kushushwa Tabata na wakahusishwa wazito hasa wakubwa

Tengeneza hilo picha la pyramid kuanzia Dar, Lindi mpaka Dom uone namna huo mtandao ulivyo mkubwa!

Je vijana wenye uchungu na nchi yao wanaojaribu kujitolea mustakali wao wauvunje huu mtandao wa biashara haramu ya vitenge watafanikiwa?
 
Kama Issue ni TRA biashara nyingi tu kubwa kubwa zinafanyika bila receipt

Waseme wanataka kiwanda chao kiingie sokoni kwa nguvu
Kama kuna kiwanda cha wazawa cha vitenge ni jambo jema sana. Haiingii akilini kila mwanamke wa Africa anavaa vitenge. Na karibu wote wananunua vitenge vipya halafu tuwe tunaagizq toka China NK.
 
Vitenge ni pasua kichwa hasa pale kariakoo kuna mtandao mkubwa sana unahusisha mpaka viongozi ndo importer wakubwa. Hawa TRA ni watoto wadogo sana wakitaka tuwape info na taarifa sahihi waache tabia zao za unyanyapaa. Sio vitenge tu mpaka nguo, mashuka na mapazia kodi hazilipwi kuanzia kule bandarini. Karikaoo ishakua ni black market tayari embu imagine TRA kariakoo kwa mwezi makusanyo ya kodi hayazidi billion 15 ni aibu ukizingatia KARIAKOO ndiyo kitovu cha biashara Africa mashariki kwa mwezi pekee Makusanyo ilibidi yawe hata bill100 na zaidi.
 
Natamani nianze kufanya biashara ya vitenge . age is just a numbers.

Niliona mzigo ulikamatwa somewhere kama Tanga hivi, niliwaza sana.

Mwanamama kuwa na mzigo mkubwa vile, japo yawezekana pia kuwa wapo wa huko mbele ndo wenye mzigo.

Let's do that japo nitaanza kidogo kidogo tu
 
Natamani nianze kufanya biashara ya vitenge . age is just a numbers.

Niliona mzigo ulikamatwa somewhere kama Tanga hivi, niliwaza sana.

Mwanamama kuwa na mzigo mkubwa vile, japo yawezekana pia kuwa wapo wa huko mbele ndo wenye mzigo.

Let's do that japo nitaanza kidogo kidogo tu
Mama bonge! Mtani vingine viache tu vipite maana vina kina kirefu kama utupu wa mwembamba
 
Tanzania ukitaka watu walipe kodi kwa moyo we weka magari ya kubebea wanafunzi ya bure! yapite kila mtaa haijalishi ni wapi halafuu yaandike lipa kodi tusome!

ukijenga barabara ziandike hii no kodi yetu! ukienda hospitali kusiwe na ubaguz tena na dawa ziwepo,! utakuja kunishukuru

Watu hawawezi lipa kodi wakati kodi zinatafunwa hadharani na wachache na kila mtu anaona
 
Back
Top Bottom