Biashara ya Ubia kwa vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya Ubia kwa vijana

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by OGOPASANA, May 21, 2012.

 1. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Heshima mbele wakuu, nimekuwa na wazo kuhusu jinsi ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana hapa nchini kwetu katika nyanja za biashara hasa kuhusu kufanya biashara kama wabia, yaani vijana kama 50 ambao wataaminiana, kufahamiana vizuri na kuwa na vision moja na kuanzisha kampuni kuendesha biashara yoyote watakayokubaliana kwa kuchangia mtaji wa walau Milioni 2 kila mmoja ambapo kwa watu 50 wataweza kupata mtaji wa Milioni 100 ambayo nahisi ni kiasi tosha kuanza kuanzisha kampuni ndogo endelevu kisha wao wakawa shareholders na hapo hapo wakaweza kujipatia ajira. Kwa wenye uzoefu, hili lina ugumu gani, hasara gani, faida gani hapa nchini?
   
 2. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Ngoja Olesaidimu aje hapa atatuambia.
   
 3. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,879
  Likes Received: 2,827
  Trophy Points: 280
  Mkuu wazo hilo zuri sana vijana hatuelewi tu! Mimi nimeanza ushawishi kwa vikundi vya hisa badala ya kugawana fedha tuweke pamoja uwe mtaji mkubwa. Endapo watalikubali wazo langu vikundi hivyo 100 tutakuwa na 400m kwa kuanzia. Lengo litakuwa kuweka viwanda vya kusindika alizeti na kusaga na kufungasha nafaka.
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Njia hii ni nzuri na yaweza kuwa suluhisho la baadhi ya matatizo ya ajira na kipato. Tatizo lipo ktk idadi, kukusanya vijana 50 wa kizazi cha dot com walio na vision moja si kazi nyepesi sana. Pili,faida ni kubwa lakini sio ya haraka haraka,inahitaji uvumilivu, subira na umakini mkubwa, je akina dot com wanaweza kusubiri miaka mitano ili wapate gawio la kwanza?

  Niliwahi kufanya sehemu fulani, ilichukua miaka 4 vijana wenzangu kunielewa. Nashauri kikundi kisizidi vijana 15, vizuri zaidi 10.
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  May 26, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaweza kuwa unalengo zuri sana lakini kama MALILA alivyo sema hapo juu, Kukusanya watu wengi kiasi hicho itakuwa ni VURUGU na si maendeleo, VIKUNDI VYA HISA NINAVYO VIJUA MIMI VINGI VYAO VINAWANACHAMA 30 KILA KIKUNDI, hivyo ukikusanya VIKUNDI 100 MAANA YAKE NI 100 times 30 AMBAPO NI WANACHAMA 3000, Mkuu kuwa na Mradi wa Pamoja wa watu kama hao ni Hatari tupu, Make ahata kama ni kampuni Basi iatakuwa imeipiku TBL au NMB, hata kwenye kugawana Faida mtu anaweza jikuta mwisho wa mwaka anapewa SH 500 kama gawaio na hapo ndo VITA ITAKAPO ANZIA,

  Mkuu Vikundi Vya hisa Mbona vipo vya watu 30 Vyenye pesa? Mimi nimesiha hudhuria sherehe za Kugawana pesa mwisho wa Mzunguko kwa VIKUNDI VINGI SANA ARUSHA MAKE NILIKUWA NAFANYA NAVYO KAZI, utakuta wanagawana MILIONI 80, so haina haja mkusanye watu 3000 ili muunde Kampuni,

  Na sijajua Uko wapi, Ila ni PM nikupe mbinu mbadala za kufanya kwa hivyo vikundi,
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  May 26, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kukusanya watu wengi hao ni kazi ngumu sana, Make hapo unatafuta mapatina wa Biashara so mkuu njia nzuri ya kukusanya watu wa Kufanya nao Biashara ni hizi

  1. Mlio soma nao Darasa moja au shule/chuo kimoja - Hawa utakuwa unawafahamu kitabia

  2. Mnao sali/swali nao- Hapa napo unaweza pata kikundi imara

  3. Mnao ishi nao Jirani/Mataa mmoja na kazalika- Hawa nao unaweza pata likundi make mnafahamiana vyema kwa Tabia ingawa si kwa undani sana

  4. Ndugu/Jamaa/Marafiki- Unaweza pata watu wakufanya nao Biashara kupitia Ndugu zako,jamaa zako na marafiki

  5. Wafanyakazi wenzako- Watu wengi wamejiunga kupata kukundi kwa kupitia njia hii ya kazini

  Na njia nyingine nyingi tu, Ila si kwa kiwango cha hao watu 50 inatakiwa wasizidi kumi, MAKE HAO 50 UNAWEZA PATA MAMBA, KENGE NA MIJUSI,

   
 7. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa upande wangu nashauri wawe 7 kwa kila kikundi.Mwaweza kukusanya capital kwa miaka 2 kila mwaka milioni 2 kila mmoja baada ya miaka 2 milioni 4*7 inakuwa 28m.Mnaanza business huku mkiendelea kuraise capital ili ifike 50m hivyo ndani ya miaka 4 mna m60 kama capital na iko ndani ya mzunguko.

  Mkuu ukiwa tayari kwa hili ni PM ili nami niwe member wako.
   
 8. K

  KISWAHILI Member

  #8
  May 26, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah!hivi kumbe watanzania mmeendelea kiasi hiki!mmenipa elimu kubwa sana!
   
 9. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  sawasawa kabisa usemavyo mkuu Malila.. idadi niliyoitoa ni mfano tu ila wadau tunaoelewa vyema kuhusu njia hii hatuna budi kuzidi kutoa taarifa, elimu na kuwaelewesha wengine especially vijana kwani naona ni njia rahisi ya umoja zaidi na ina faida nyingi kuliko kijana mmoja au wawili wakianzisha biashara hasa kwa level ya buiashara zilizokaa kiofisi. Ifikie wakati sasa jukwaa hili lile la kipekee katika kutoa nini cha kufanya na si kujadili taarifa ambazo hazimsaidii mtanzania. uwezo tunao, mitaji tunayo na tunaweza kuitafuta ingawa ni kidogo (fuatilia watanzania wanavyoweza kuchangia michango ya shughuli na sherehe za siku moja), hivyo tukiwa serious tunaweza kuendelea bila misaada ya wazungu kuanzia ngazi za juu hadi chini.
   
 10. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  A partnership is a business where there are two or more owners of the enterprise. Most partnerships are between two and twenty members though there are examples like John Lewis and some of the major world accountancy firms where there are hundreds of partners.

  A partner is normally set up using a Deed of Partnership. This contains:

  • Amount of capital each partner should provide (i.e. starting cash).
  • How profits or losses should be divided.
  • How many votes each partner has (usually based on proportion of capital provided).
  • Rules on how to take on new partners.
  • How the partnership is brought to an end, or how a partner leaves.

  The advantages of a sole trader becoming a partnership are:

  • Spreads the risk across more people, so if the business gets into difficulty then there are more people to share the burden of debt
  • Partner may bring money and resources to the business (e.g. better premises to work from)
  • Partner may bring other skills and ideas to the business, complementing the work already done by the original partner
  • Increased credibility with potential customers and suppliers – who may see dealing with the business as less risky than trading with just a sole trader

  For example, a builder, working originally as a sole trader, may team up with an architect or carpenter to form a partnership. Either would bring added expertise, but also might bring added capital and/or contacts. Of course the builder could team up with another builder as well – sharing the risk, and potentially the workload.

  The main disadvantages of becoming a partnership are:

  • Have to share the profits.
  • Less control of the business for the individual.
  • Disputes over workload.
  • Problems if partners disagree over of direction of business.
  The next step for a partnership is to move towards becoming a private limited company. However some partnerships do not want to move to this stage.

  The advantages of remaining a partnership rather than becoming a private limited company are:

  • Costs money to set up limited company (may need to employ a solicitor to set up the paper work).
  • Company accounts are filed so the public can view them (and competitors).
  • May need to spend money on an auditor to check the accounts before they are filed.
  When a partnership finishes then, depending on how the Deed of Partnership is set up, each partner has an agreed slice of the business.

  source: www.tutor2u.net
   
 11. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  mkuu Chasha...hizo ni njia nzuri za kupata partners lakini kwa asilimia kubwa naweza kusema kuwa si nzuri kwa sisi watanzania kutokana na mila, desturi, taratibu, mazoea na maisha yetu kwani watu wa karibu katika maisha yetu kama vile, majirani, marafiki, ndugu na jamaa hawana upendo wa kweli na kutakiana maendeleo baina yao, pia hata usiriasi hautakuwepo katika biashara kwa kuwa na idadi kubwa ya watu aina hiyo. Kuaminiana katika biashara si lazima hadi muwe mmefahamiana kwa miaka mingi au kuwa karibu sana, unaweza kutafuta watu usiofahamiana nao kwa muda mrefu au wasio ndugu zako, marafiki, wazazi au wafanyakazi wenzako wenye nia, uelewa, uwezo, uvumilivu, heshima, busara, ujuzi, uzoefu na utayari na wakawa wabia wazuri sana, ndo maana hata SACCOSS na vikundi na vyama kama hivyo huundwa na watu tofauti na vinaendelea vizuri. 'kikulacho kinguoni mwako'.
   
Loading...