television
Member
- May 1, 2021
- 78
- 69
Fungua tuuu mkubwa nijambo la heri
Mkuu Asante kwa ushauriSorry for late reply.....za dukani utapata ila utapata mzigo mdogo...... Za mtumba zinauzika sana hasa za kina dada tena unaweza anza na za mtumba za laki 3 tu alafu laki 3 nyingine wekea viati vya kina dada.....vingi vinauzika kwa elfu 5 yani kariakoo unanunua 2500 unakuja uza 5000......
Laki 4 ibaki pembeni kama akiba na nguo ufanye pointing kuliko kununua belo, sehemu za kufanyia pointing kwa dar ni ilalaboma na karume huko nguvu yako ya kuchagua ndio itafanya upate nguo nzuri kwa bei ya kuanzia 1000 - 4000 kwa ilalaboma kama ukiwahi alfajiri....
Utaratibu wa kupata meza, unategemeana na mkoa, ila sehemu nyingi ni nguvu ya kuwahi na kujuana na majirani zako kibiashara na tozo wanalipa 2000 kwa siku hiyo ni Moro.....kwa iringa huku ni bure kabisa kwa machinga......
Ukiwa smart utatoka mapema, kupitia nguo zakike na viatu kulaza 50 itakuwa kawaida na ninauhakika katika hili....
nimekushauri upoint ili usipate maronya mengi pia uzoee deals zinaendaje ili ukizoeana na unaeona anapata mabelo mazuri na muaminifu akushike mkono ..... Changamoto zipo ila zinasolvika na ni ndogondogo sana.....
Mfano kipindi cha baridi hiki mikoako ukipeleka trench coats almaarufu kama koti za kikorea utauza sana kwa bei ya 5000 na zile ndefu mzuri 7000 hadi 8000.....
Shukrani mkuu hii ni moja ya biashara niliyowahi ifanya hivyo tarifa zke ninazo mkuiMkuu Asante kwa ushauri
Mpuuze io sio sababuKwa mfano mimi nikiingia Jf jukwaa langu ni humu BUU na Mara moja moja MMU inamaana sifahamiki
Hongera nimependa bosi ,naskia ukiamka mapema hapo ni kugombania vibaya au inakuajePia za mtumba zinauza na kutoka kwa uharaka hasa za akina dada kuliko za dukani......pia nilichosahau ni rika...yani Nguo za mtumba angalia sana unataka uwauzie wa rika gani usiwele nguo nyingi za wanafunzi wa sekondari utakosa pesa...wewe weka nguo za wanachuo na wadada wakubwa kiasi pesa ipo pale mkuu.....
my testimony: kipindi cha corona nilikuwa nyumbani office ilifungwa basi nikaenda dar nikapoint nguo ilala boma nilienda saa 9 usiku wakafungua saa 11 hivi nikapoint nguo nzuri sana za kike kwa 1500, 2000 skin jeans 3000 wanapofungua mabelo zingine hadi 500 blouse nzuri tu......skin jeans nlinunua kama 20 tu sikuwa na uhakika nazo ila ajabu niliuza skin jeans hadi sio vizuri kwa bei ya 6500 nikajilaumu kwanini sikuchukua skin tu....
so Skin kwa wanachuo zinauzika sana na zile track zao kama wanazovaa wasanii kama Nandy wewe ziweke humo utanishukuru badae.....
Nilishindwa endelea sababu ofisi ilifunguliwa na nikashindwa kumanage muda vizuri wa biashara na kazi. Nilitumia mtaji wa laki 330 tu including nauli
Mkuu wewe uko Dar pia?Ok ushaur wang kwann kwa pesa io usingeitumia yote na ukafungua duka online lets say kachukue nguo za watoto na kina dada kwa 200000 then unafanya matangazo unalipia hii inakulipa zaid na mm ndio biashara yangu ...mtu akitaka nguo unampelekea alipo ...na io pesa nyingine unaiweka huku ukiangalia upepo unaendaje ...yan ukiwa na laki 3 ..mbili mzgo na moja matangazo inalipa sana
Asante sana Mkuu kuna swali hapo mdau kauliza huko ilala boma mzigo ni wa kugombania au ipoje?Nilikuwa nauzia iringa mkuu tena kama machinga tu..... Nguo wamazopenda binti wa dar kuanzia crop top had vile viskin vyote vinapatikana ilala boma kwa bei ya 1500-2500 kwa crop top na visweta vya kike vizuri skin ndo hiyo elfu 3-4
hapana eio kugombania kihivyo ni kawaida tu mnaweza kuwa watu 7 belo linakatwa ukiwahi ndio umewahi.....pia kwa uzoefu wangu wanafungua belo saa 11 hivi maana mimi nilifika saa 9 nikasubiri hadi saa 11......ila ukiwahi sana kwenye hiyo saa 11 au 11 kasoro unaweza kuuliza anaefungua nguo unazohitaji alafu unamwambia nguo zote kali unaomba akuwekee utanunua wewe ukiwa pembeni wenzio wanashangaa unaona tu anakurushia nguo.... kama ni skin, vipochi vibegi vyote niliona watu wanafanya hivyo ni njia nzuri zaidi akikuzoea mara 2 raha sana utapata nguo kali sana bila kugombania.....Hongera nimependa bosi ,naskia ukiamka mapema hapo ni kugombania vibaya au inakuaje
Hongera nimependa bosi ,naskia ukiamka mapema hapo ni kugombania vibaya au inakuaje
hapana eio kugombania kihivyo ni kawaida tu mnaweza kuwa watu 7 belo linakatwa ukiwahi ndio umewahi.....pia kwa uzoefu wangu wanafungua belo saa 11 hivi maana mimi nilifika saa 9 nikasubiri hadi saa 11......ila ukiwahi sana kwenye hiyo saa 11 au 11 kasoro unaweza kuuliza anaefungua nguo unazohitaji alafu unamwambia nguo zote kali unaomba akuwekee utanunua wewe ukiwa pembeni wenzio wanashangaa unaona tu anakurushia nguo.... kama ni skin, vipochi vibegi vyote niliona watu wanafanya hivyo ni njia nzuri zaidi akikuzoea mara 2 raha sana utapata nguo kali sana bila kugombania.....
Kaka nimejibuAsante sana Mkuu kuna swali hapo mdau kauliza huko ilala boma mzigo ni wa kugombania au ipoje?
😒Kaka
Kush nikuambie kitu, watu hutofautiana
Kuna akija sisi Karucee ni headache tangu wadogo.... Darasani ni noisemakers tangu nursery school.
Ila kuna wengine who are comfortable in their solitude. Hawajichanganyi not because hawataki but it's because of their nature.
Some are shy, some just can't interact with others.
So please tumuelewe. And sometimes it is better to just read and mute rather than offend people or insult them.
If you can assist her please do... It you can send her a link, go ahead. The good you do will come back to you in one way or the other.
Mtumba ukiingia vizuri na ukiwa na mipango mizuri unatoboa maana kwakila nguo faida inakuwa elfu 5 au 4 kwasiku ukiuza nguo 5 basi unakuwa na 25 kwa mtaji wa laki 2 au 3 sio mbaya......
Pia mkuu unaweza fungua frame karbu na town au ukatengeneza kwa kutumia mbao na zile nailon ndefu (nimesahau jina) ukawa unauza mtumba tu utajaza sana.....kuna jamaa angu amefungua frame karbu na town amejaza nguo za laki 7 tu na ameweka vizuri chumba cha kupimia huwa anaweza laza parefu sana maana pindi nikienda mtembelea kwa masaa 2 anapata wateja 7 hadi 10 hapo 6 wakinunua anakuwa na 30 tayari.Ndio MKUU. naona wapo bize na kulijenga TAIFA.