Biashara ya mtandaoni

poposindege

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
453
175
Habari wanaJF,

Kwa muda mrefu nimetamani kununua bidhaa mbalimbali toka nje ya nchi na hasa kupitia njia ya mtandao.najua ipo mitandao mingi inauza bidhaa mbalimbali,lakini nimeingia woga baada ya kusikia wapo matapeli wanaowaibia watu kupitia njia hii ya mtandao.Sasa wakuu naomba mnielekeze kupitia uzoefu au ufahamu wenu kunijuza mitandao inayouza bidhaa mbalimbali tena ni waaminifu na si matapeli. Kama ikiwekana na njia inayotuka kuwatumia pesa pamajo na kupokea mzigo. Natumai wana jamvi mtanisaidia.
 
Ni rahisi sana from ebay, amazon etc tatizo zina ibiwa zote hapo posta so bure uende kko
 
SHARO:
Weka wazi kiongozi mi sijakuelewa!

Biashara ya nini?
Ebay ni nini?
Amazoni nini?
Biashara hiyo itafanyikaje kwenye mtandao?

Siwote wanajua unachojua wewe,unapotaka kuelimisha au kufahamisha jambo lolote yakupasa kutoacha maswali mengi kuliko majibu!

Hima lisha watu kwa uwazi mkuu!!!
 
Oh!! kumbe hujui kabisa

Hivi jiunge na Paypal fungua pay pal fata maelekezo fungua akount nenda bank kajaze pesa account yako..ni kama mpesa vile. Ukiona account inapesa fanya manunuzi online payment bonya paypal jaza detail tayari ushanunua kama ni free shiping watakutumia kwa adress uliyowapa..standard airmail ni common na cheapest way!!

Yote tisa niliagiza laptop kwa njia hiyo...nimeenda posta kucheki loh!!!! mara haijafika mara haionekani nika tuma email tena kuuliza kwa muuzaji akasema imefika hadi tarehe kanipa baaada ya hapo nikaanza safari za posta njoo kesho njoo keshokutwa zaidi ya 20 aha!! nikakaa chini nikapiga mahesabu gharama ya mafuta imepanda safari za posta na foreni aha!! bora ningenunua Bongo.

So labda uwe na mtu nje au utumie DHL kama muuzaji anatakubali ila dhl ni expensive kidogo. kila la heri bro.
 
Back
Top Bottom