Biashara ya milioni tatu arusha mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya milioni tatu arusha mjini

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Mtoka Mbali, Sep 17, 2012.

 1. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Habari za wikendi wapendwa?
  Bila kupindisha mada kama ilivyo katika kichwa hapo juu ni kwamba mie ni mkazi wa Arusha mjini mwenye nia ya kufanya biashara angalau yenye mtaji wa shilingi milioni tatu. Hiyo ndoela niliyopanga kuanza nayo katika biashara japo naweza kuanza na hata milioni tatu.
  Mie ni muajiriwa katika kampuni binafsi na huwa naingia kazini kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni na siku pekee ninayo pata muda wa kuwa nyumbani ni Juma Pili pekee. Nimekaa nikawaza biashara ya kufanya maana nimeona si vyema kuishi kwa kutegemea mshahara tu na maisha yanavyozidi kupanda kila kukicha nikaona niwashirikishe wanajanvi wenzangu.
  Biashara ya duka naona ni kama kwangu si rahisi maana hata mtu mwaminifu wa kuacha dukani sina.
  Nikafikiria Salooni za kiume lakini bado haijaniingia akilini maana sina iterest na saloon kabisa.
  Nimefikilia kununua Toyo (Boda boda), pickpick za abiria mbili ila naona kuna jamaa kadhaa wananidiscouragena kwamba kufanya hivyo ni hasara na wengine wana sema marejesho ni kidogo sana maana hivi sasa dreva toyo hurejesha shiling 30,000/= kwa wiki. Kwa upande wangu naona nikiwa na toyo mbili nitaweza kupata 60,000/= kwa wiki ambayo naona si mbaya sana jabo ningependa kupata ushauri wenu.
  Ningeomba tafadhali mwenze kuweza kunishauri biashara nyingine mbali na biashara ya toyo tafadhali nishaurini nisije poteza ela zangu kuingia kwenye biashara nisiyoiweza.
  Biashara nyingine mbadala ningependa kuitafakari tafadhali kwa mwenye mawazo mengine.

  Nitafurahia nikipata michango yenu tafadhali wana janvi.
  Kila wazo litaheshimika liwe hasi au chanya.

  Asanteni sana kwa muda wenu.
   
 2. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Kama kazi unayo basi mie nakushauri uachane na biashara yoyote kwa kuwa itafikia sehemu inakulazimu utoroke kazini uende kukagua biashara yako. Pia inaweza kukusababishia kushindwa kufanya kazi ya bosi wako na kujikuta unaelekeza nguvu kubwa ktk mradi wako,bosi wako akigundua changes zozote inaweza kuhatarisha ajira yako.ushauri wangu kwakuwa unahiyo 3m bora uiwekeze ktk kununua viwanja pembeni ya mji au mashamba,ufanye hivyo kwa kila unapopata mshahara wako mpaka utakapo fikia ukomo wa ajira yako na ikitokea ukadumu kwa mwaka 1 au 2 ninaimani utakuwa unamiliki maeneo mengi zaidi,ubora wa kuwekeza ktk mashamba kwanza yanajichunga menyewe 2 kila siku yanaongezeka thamani 3 ni aseti nzuri na haina risk kubwa.
   
 3. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Asante sana ndugu Slave.
  Ushauri wako mzuri sana na ninauheshimu sana. Ninakaribisha mawazo ya wanajanvi wengine tafadhali, ushauli wa yeyote yule utathaminiwa.

  Asanteni sana.
   
 4. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  MiMI NAOMBA NISEME WEWE UNASEMA UNAHITAJI MAWAZO YA BIASHARA WAKATI HAPO HAPO UNASEMA HUMUAMINI MTU? EBU JIULIZE KAMA BOSS WAKO ASINGEKUAMINI UNGEKUA NA KAZI? NB:WAPENDE KWANZA WANAOKUZUNGUKA NA KUWAONA NI WAAMINIFU NDUGU NAWE UTAPATA AMANI YA KUFANYA BIASHARA. LA SIVYO KILA SIKU UTALALAMIKA UNAIBIWA!
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Ushauri wako siuungi mkono hata Kidogo, Kuanzisha Biashara Ukiwa Kazini Ndo Njiaa rahisi na isiyo kuwa na Risk kubwa na ni Transision kuelekea Kijiajiri Mwenyewe, Kilichopo ni Mwanzisha Biashara Kujipanga na Kuona Ataendesha Vipi Biashara yake huku akiwa anafanya kazi, Ishu ya Kununua Viwanja ni Ok ila sidhani kama Uko Arusha wewe,

  Na nina uhakika wewe ni Mfanya kazi make Mfanya Biashara hawezi kutoa ushauri wa Aina Hii na imefika mahali kwa Mtu anaye penda Kuanzisha Biashara awafuate wafanya Biashara wampe ushauri na si kupewa ushauri wa Mtu ambaye hata Kibanda cha kuchajisha Simu hana, So huwezi pata ushauri wa Maana kutoka kwa Mwajiriwa sanasana utapata ushauri wa kukukatisha tamaa
   
 6. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kwa ufupi tu inabidi mtoa mada aangalie na kuuchambua ushauri wa kila mmoja wetu, tatizo ninalo liona mie ni kwamba hawezi kufanya kazi na biashara kwa wakati mmoja,hapa inaonyesha vyote anavitaka kwa wakati mmoja, naomba ujaribu kupima hapo.kama angesema anataka kuacha kazi ili awd mfanyabiashara hapo ingekuwa sawa kwa kile unachoamini wewe,lakini kama atakuwa na kazi kisha biashara lazima kimoja kitamponyoka wahenga walisema mshika mbili....? Kuhusu mie kumiliki kibanda cha simu,kwa taarifa tu nikwamba hizi biashara pia huwa zina risk yake inapo tokea umefirisika gafla basi aseti hasa ya ardhi inaweza kukurejesha tena barabarani. Mie binafsi najivunia kumiliki ardhi sehemu ambayo niliinunua laki moja miaka miwili iliyopita kwa sasa naweza kuiuza milioni 4 tena kwa kuringa.
   
 7. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  mkuu ... watu wanatoka kazini saa12 jioni na wanaingia kwenye private bizz mpaka hata saa 7 usiku ... usiwe muoga wa fortunes ... unataka asubirie NSSF halafu uanze kumcheka eti it is too late

  go go go
   
 8. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Aksante sana kaka.
   
 9. k

  kamkoda JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 396
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ila hakikisha pikipiki hizo zinajulikana kwa jina la askari mmoja maarufu hapo mjini kukwepa notification, pesa itarudi fasta!
   
 10. GreatMkubwa

  GreatMkubwa Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Wazo zuri kufanya ujasiriamali, binafsi ni mwajiriwa wa serikali, naingia kazini saa mbili natoka saa kumi moja kwamoja naenda kwenye ujasiriamali wangu nakaa huko nikipiga kazi mpk saa nne au hata sita usiku ndo narud geto! Kazini niko fiti kama kawaida na hakuna ulalamishi wa aina yoyote, nakushauri uendelee na wazo lako la kujiajiri mkuu.
  Kuhusu biashara ya kufanya kwa 3Mil, nakumbuka niliwahi kufanya biashara ya bodaboda pale moshi wakati nipo chuo, jamaa alkuwa ananpa 42,000 kwa wiki ila cha moto nilikipata, kwanza hatunzi pikipiki, hafanyi service kama tulivyokubaliana kwa mfano tulkubaliana kw mkataba kabsaa kuwa service isiyozidi Tsh 2000 afanye yy ila siku moja niliona pkpk haina indikator na glass y taa y mbele ilipasuka wala hakurekbisha pamoja na kumwambia afanye hivyo.. ananipa hela mwezi mmoja vizuri ila mwezi unaofata hela karibu yote itaishia kweny service!!! nilifanya utafiti nikagndua wanakusanya mpaka 30,000 per day siku nzuri na 15,000 kwa siku za kawaida!! jiandae kwa changamoto.
   
Loading...