Biashara ya mahindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya mahindi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by DATOGA, Nov 18, 2011.

 1. D

  DATOGA Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wana JF kwanza nawasalimuni kwa heshima kubwa sana. Nimekuwa nikisoma maoni ya wachangiaji tofauti na nimegundua JF ni Online University there are real great thinkers (i admit that). Anyway......
  Naomba wanajamii mnishauri kama Biashara ya kutoa nafaka hasa MAHINDI toka mikoani kuleta Dar kama inalipa.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Duh....dar kila biashara inalipa, bt ukiwa na mashiine yako ya kusaga ni bora zaidi, faida twice!! Mapumba na kila kitu utauza!
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Nov 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  mkuu hii biashara haiwezi lipa kwa sababu zifuatazo,1. Hakuna unacho ongeza hapo mean thamani2. Waga ni ujanja ujanja utakufanya ufanikiwe- unachukua gunia la mahindi unachanganya na mahindi mabovu na kazalikamkuu imefika wakati watu wafanye biashara kitalaamu, namaanisha kuongeza thamani katika hiyo baishara yako.1. Nunua mashine ya kukoboa na kusaga2. Tafuta vifungashio vyako mwenyewe3. Anza kupaki kwenye mifuko ya kilo 2, kilo 5 na kilo 104. Anza na wateja wa mitaa unayo ishi ukisha fanikiwa kuwateka ndo uangalie kusambaza na kwenye mitaa mingine.5. Kwenye ishu ya ushindani jalibu kutafuta vitu ambavyo vitawafanya wateja wanunue unga wako na si unga wa baharesa, mohamed entreprises na azania na wengineo- hii biashara ina compettion kubwa sana but lazima na wewe upambane vilivyo na si kuanza kushindwa hata kabla ya kuanza kuzalisha,au kama uko mikoani anzia kupaki huko huko mkoa ulipo make parking nyingi sana zinafanyika dar mwisho
   
 4. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu ur rty kwa dar ukiwa na store + masine yako au kama uwezo mdogo unaingia mkataba venture na mwenye mashine mnaganya biashara.
   
 5. D

  DATOGA Member

  #5
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nashukuru sana ndg zangu, vipi hiyo mashine ya kusaga ina cost bei gani , ishu kama store haitanisumbua sana, ila hilo wazo la mashine pia poa ila naomba kujua bei yake kama kuna anaejua.
   
 6. N

  NIPENDEMIMI Member

  #6
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  bila kufanya processing ya hizo nafaka unazonunua mikoani hutafanikiwa -- ukizingatia gharama zifuatazo:
  a) Ukusanyaji -- gharama za ukusanyaji, accomodations, man power for at least 10 days kwa Tani kumi. Huko mikoani utanunua kwa debe Tshs 5000 ambalo ni kilo 18. Kujaza mzigo Tani Kumi utahitaji 2,780,000/= million.
  b) Usafiri -- Lazima utakodi fuso -- lets say unachukulia mzigo Tanga or Moro approx 800,000/- mpaka manzese sokoni.

  Add: 2,780,000+800,000 = 3,580,000= Million. Gharama ya kuleta Tani 10 toka mikoani.

  Kuuza:
  Bei ya sasa ni Tshs. 380 mpaka 390 whole sale kwa sasa = kwa hiyo Tani 10 inakuwa 10,000 x 390 = 3.9m.

  Faida yako:

  3,900,000 -3,585,000 = 315,000 ( FAIDA YAKO KULETA MZIGO WA TANI 10 TOKA TANGA & MORO & DODOMA)

  Hapo hujaweka gharama zingine zingine - maji ya kunywa, nk nk . ---- ndiyo maana jamaa kakwambia lazima ufanye processing, otherwise mzee unapoteza muda.
   
 8. I

  IGO Member

  #8
  Nov 18, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu uko sahihi kabisa mimi nilianza kwa kuleta mahindi dar kutoka dodoma nilipata faida maramoja tu na hasara mara tatu,kwasababu ya price flactuation,unanunua kwa bei kubwa unakuta bei ya soko imeshuka, na wateja maranyingi wanachukua kwa mkopo kwa hiyo unalazimika kukaa kama wiki moja au mbili kusubiri ela kwa hiyo garama ya chakula na malazi na matumizi mengine inaongezeka.nikaamua kuacha nikanunua mashine nikaanza kusaga kupaki na kusambaya mwenyewe upinzani ni mkubwa unaitaji tu kuwa mbunifu utafanikiwa.
   
 9. D

  DATOGA Member

  #9
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sasa naomba nifahamu hiyo mashine nitanunua kwa bei gani ndg yangu, maana maoni yenu yako strong sana, ahsanteni
   
Loading...