Biashara ya madawa ya kulevya.

Makwarukwaru

Member
Mar 10, 2012
66
25
Kwa mtazamo wa kawaida, madawa ya kulevya ni kitu kinachopigwa vita sana. lakini kiuhalisia haiko hivyo. Kwani watu wanauza madawa haya peupe bila woga wala wasiwasi. Nani yuko nyuma ya biashara hii?ananguvu kiasi gani mpaka imekua halali kiasi hiki?Ukitembelea maeneo ya kawe ukwamani vijana wanatumia madawa 24/7 bila kificho wala wasiwasi,nani yuko nyuma yao anaewapa kichwa kiasi hiki? Sijataka kusema maeneo mengine ila hali ni mbaya,kama serikali kila mara inapiga kelele kuhusu madawa hawa mbona hawakamatwi? Mwisho, bangi ikikamatwa huwa inaharibiwa tunaona, ule unga unaokamatwa huwa unapelekwa wapi au unafanywa nini?
 
dah!!! umenifanya nimkumbuke marehemu Amina Chifupa, alitaka kutujibia haya maswali maana alidai alikuwa tayari anayo majibu yake. kwa bahati mbaya hakujaaliwa kuishi na kutupatia hayo majibu, YASEMEKANA WAHUSIKA WALIM-NYAMAZISHA FASTA. kwa hiyo ndugu yangu, nionavyo mimi, kutaka kuwajua wahusika, ni sawa na ku-beep kifo. lakini siwezi kushangaa kuwa ni watu wenye nafasi zao kwenye hili LI-SERIKALI BOVU KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA SERIKALI HAPA DUNIANI, maana katika hali ya kawaida haiwezekani pamoja na kelele zote hizo halafu eti wahusika hawakamatwi, si ajabu anayepiga kelele ndo mmiliki wa hiyo biashara, ROHONI KWA MTU MBALI.
 
Hili ni janga baya sana sana mie humwambia Mungu wangu kila auzaye basi Mungu amhukumu hapahapa duniani asimkawize. It is so painful jamani kwa watoto wanapoingizwa katika matumizi ya madawa haya. Mungu tunusuru na angamiza biashara hii.
 
utakuta list ni ya wakubwa wa serikali na viongozi wakubwa wa kidini ndio maana wanashindwa kufichuana...MOJA AKIMWAGA MBOGA MWINGINE ANAMWAGA UGALI
 
Tanzania bila madawa inawezekanaa! Tanzania bila madawa inawezekana haijashindikana inawezekana! Hiphop bila madawa inawezekana Hiphop bila madawa inawezekana haijashindikana inawezekana!
 
Wakubwa wa hii nchi wanausika wao na marafiki zao. Sasa nani atamwangusha mwenzie wakati wote wameshika kwenye ncha ya kisu kwamba huyu akifunguka basi na yule nae anafunguka. Hili ni janga la dunia na wala sio la tanzania peke yake so vita yake ni kali sana. Ukiamua kupambana basi ujue siku yoyote unaweza ukatangulia kwa muumba.
 
Mtambo wa madawa kulevya mliukamata , lakini maendeleo ya kesi mbona hatujayapata? - Wimbo wa bongo fleva
 
Ishu iko deep sana..drug dealers wote wanajulikana ni vile serikali haitak kuwatoa tupo nao tunasubir wazulumiane ndio wachomane
 
Wana JF. hii ishu ya Madawa ni janga la Dunia Nzima...
Mfano: nikikwambia Afghanistany ni nchi ambayo ilikuwa inategemea Opium katika uchumi wake na ishu ya ugaidi ni danganya toto yenye kuficha ukweli... vile vita maslahi yalikuwa ni

1. kupunguza uzalishaji wa Opium(ni bei rahisi) Afghanistany kwahiyo bidhaa hiyo ikipungua itaweza kuwapa fursa Wamiliki wa mashamba ya Coka yaliyopo Amerika ya kusini kufanya biashara duniani kote.

2. yale mafuta yaliyopo Iraqy ndio chachu ya kuvamiwa nchi hiyo kwa kigezo cha ugaidi...

Sasa jiulize tofauti na AntDrugs wa Kulasini ni taasisi gani hapa TZ ipo kwa ajiri ya kazi moja tu ya kuzuia hayo madawa... na je ulishawahi kusikia changamoto zao... labda za kukimbizana na Mateja lakini si Vinara wa kuuza hayo Madawa maana jamaa nahisi wana mkono mzuri kwa kutoa rushwa... nahisi hata escort wanaweza kupewa
 
dah!!! umenifanya nimkumbuke marehemu Amina Chifupa, alitaka kutujibia haya maswali maana alidai alikuwa tayari anayo majibu yake. kwa bahati mbaya hakujaaliwa kuishi na kutupatia hayo majibu, YASEMEKANA WAHUSIKA WALIM-NYAMAZISHA FASTA. kwa hiyo ndugu yangu, nionavyo mimi, kutaka kuwajua wahusika, ni sawa na ku-beep kifo. lakini siwezi kushangaa kuwa ni watu wenye nafasi zao kwenye hili LI-SERIKALI BOVU KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA SERIKALI HAPA DUNIANI, maana katika hali ya kawaida haiwezekani pamoja na kelele zote hizo halafu eti wahusika hawakamatwi, si ajabu anayepiga kelele ndo mmiliki wa hiyo biashara, ROHONI KWA MTU MBALI.

kujaribu kuwagusa hao wauza madawa ya kulevya ni kujitoa muhanga
 
Back
Top Bottom