Biashara ya kwenda China

Buza

Member
Aug 7, 2011
57
14
Natamani kufanya biashara ya kwenda China na kuleta vifaa vya umeme na kuuza.

Naomba ushauri inahitajika mtaji wa kiasi gani kwa kuanzia.
 
Excluding fixed assets, kwa kuanzia tu hata milioni 10 ya kitanzania inatosha lakini pia inategemea na ukubwa wa biashara unayotaka kuianzisha.
 
Ni ushauri umempa Mdizi, lakini pia mm naona bora ungemshauri afanye nn, faida na hasara ya kufanya biashara anayoifikiria Yese.
 
Natamani kufanya biashara ya kwenda china na kuleta vifaa vya umeme na kuuza. Naomba ushauri inahitajika mtaji wa kiasi gani kwa kuanzia.
Wazo lako sio baya. Ila hii biashara ya vifaa vya umeme imeshikiliwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa hapa nchini kwa mfano Tronic,Tropical na wengineo. Kwa mtu Kama wewe unayetaka kuanza hii biashara,sikushauri uanze moja kwa moja na biashara hii. Kwa sababu hao jamaa wenye hayo makampuni wana watu wao TBS na TRA, mzigo wako unaweza kupigwa zengwe na ukachomwa moto kwa kusingiziwa ni bidhaa feki. Wafanyabiashara wakubwa wanacheza rafu sana.

Kuna wakati niliagiza Steel beams kutoka Kenya nikapigwa ushuru wa ajabu sana. Halafu hao jamaa TRA wakaniambia siku hizi Steel beams haziagizwi kutoka nje, wakanielekeza kwa Huyo Muhindi ana kiwanda hapa Dar..na ndio supplier pekee. Kwa hiyo mambo Kama hayo yatakupa picha halisi ya biashara za kusafiri bila kufanya utafiti wa kina. Unaweza ukawa unaleta mzigo na kuuza kwa faida ndogo sana.
kila la kheri
 
Nashukuru kwa ushauri, wakumwitu amenisaidia kufunguka zaidi. Ila hata ushauri wa mdizi ni mzuri lakini nafikiri nahitaji kuongeza mtaji ili niweze kuingia kwenye biashara ya uzalishaji, maana nafikiri biashara ya uzalishaji inahitajika muda ili utengeneze jina.
 
Duh Borat69 umenipa changamoto.
Tunaelimishana tu mkuu. Nafikiri umeshasikia sana na kuona kwenye luninga TBS wakichoma moto bidhaa feki. Mara nyingi zile bidhaa unakuta ameleta mfanyabiashara mdogo kwa hela ya mkopo au kudunduliza. Kuna rafu mbaya sana katika baadhi ya biashara hapa mjini. Au kwa mfano ukiagiza Kontena la spare parts unafikiri kwa nini huwa Wapemba wanakufuata hata hujatoa mzigo na kutaka kununua Mali yote!?
 
Natamani kufanya biashara ya kwenda china na kuleta vifaa vya umeme na kuuza. Naomba ushauri inahitajika mtaji wa kiasi gani kwa kuanzia.
Tuwasiliane, kuna Supplier wa Kichina anakampuni yake hapa East africa na inafanya hiyo kazi ya vifaa vya umeme, nadhani itakuraishia kabla ya kuanza kwenda Chinaa
 
Changamoto nyingine utakayoipata ni kuwa mentality ya watanzania wengi wanasema kuwa vifaa vya umeme kutoka china ni vibovu wa proove wrong kwa kuwaletea vifaa ambavyo ni durable na kwa umeme wetu huu ..... Sijui... Kila la kheri mkuu
 
Jamani kweli Jamii forums mtandao mzuri sana cha ushauri kwa wanachama kwa wanchama wanasaidiana kupeana ushauri na wengine tunapata faida ya kuelewa

Tatizo hawa jamaa hawafunguki indeep.majibu mkato,mtu ambae hata hajawahi kwenda huko na anataka kujua pa kuanzia atatoka kapa tu hapa.
 
Natamani kufanya biashara ya kwenda china na kuleta vifaa vya umeme na kuuza. Naomba ushauri inahitajika mtaji wa kiasi gani kwa kuanzia.

unahitaji kuwa agent au authorized dealer/distributor wa bidhaa fulani, ili ukamate soko hapa tanzania. na si lazima uende china, unaweza kwenda south korea, india, russia, turkey, brazil. hukokuna bidhaa nyingi tu ambazo hazina ma-agent hapa nchini.
 
Tatizo hawa jamaa hawafunguki indeep.majibu mkato,mtu ambae hata hajawahi kwenda huko na anataka kujua pa kuanzia atatoka kapa tu hapa.
Wewe unataka mtu afunguke kivipi zaidi ya hayo maelezo watu waliochangia humu. Au unataka uelezwe mpaka guest au lodge mtu aliyekuwa jana usiku na jina la mwanamke ndio uridhike!?

Kama una Swali uliza specific na utajibiwa accordingly. Kuna watu wengine hatupendi kujaza nafasi kwa bandiko refuuu Kama magazeti ya shigongo. Wewe uliza unachotaka kujua,nina uhakika utapata jibu sio kuja na milawama tu..wabongo sisi,kazi kweli kweli:frusty:
 
Nimeipenda hii.
 
Tunaelimishana tu mkuu. Nafikiri umeshasikia sana na kuona kwenye luninga TBS wakichoma moto bidhaa feki. Mara nyingi zile bidhaa unakuta ameleta mfanyabiashara mdogo kwa hela ya mkopo au kudunduliza. Kuna rafu mbaya sana katika baadhi ya biashara hapa mjini. Au kwa mfano ukiagiza Kontena la spare parts unafikiri kwa nini huwa Wapemba wanakufuata hata hujatoa mzigo na kutaka kununua Mali yote!?

Mkuu Borat69 hebu nitoe usingizini hapo kidogo hapo kwenye red. Nilikua na mpango wa kufanya hiyo biashara ya kuleta spare parts za magari.
 
Last edited by a moderator:
Changamoto nyingine utakayoipata ni kuwa mentality ya watanzania wengi wanasema kuwa vifaa vya umeme kutoka china ni vibovu wa proove wrong kwa kuwaletea vifaa ambavyo ni durable na kwa umeme wetu huu ..... Sijui... Kila la kheri mkuu
Mimi ningekushauri uende Bangkok vitu vya Thailand vina ubora zaidi ya vya China hasa kwa vitu ambavyo watu wa mtaji mdogo huweza kununua,na hata ukileta hapa kwa mfano nguo za Thailand utauza kuliko yule mwenye nguo za Uchina
 
unahitaji kuwa agent au authorized dealer/distributor wa bidhaa fulani, ili ukamate soko hapa tanzania. na si lazima uende china, unaweza kwenda south korea, india, russia, turkey, brazil. hukokuna bidhaa nyingi tu ambazo hazina ma-agent hapa nchini.
Hii nimeipenda sana mkuu. Hebu iongezee nyama kidogo basi ili twende sawa!
 
Jamani kweli Jamii forums mtandao mzuri sana cha ushauri kwa wanachama kwa wanchama wanasaidiana kupeana ushauri na wengine tunapata faida ya kuelewa
Changia basi japo kidogo!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom