Biashara ya kwenda China

Mimi ningekushauri uende Bangkok vitu vya Thailand vina ubora zaidi ya vya China hasa kwa vitu ambavyo watu wa mtaji mdogo huweza kununua,na hata ukileta hapa kwa mfano nguo za Thailand utauza kuliko yule mwenye nguo za Uchina
Pamoja sana kamanda mfianchi ila naomba details za kwenda Thai ukilinganisha na za kwenda hu ho logistically.
 
Wazo lako sio baya. Ila hii biashara ya vifaa vya umeme imeshikiliwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa hapa nchini kwa mfano Tronic,Tropical na wengineo. Kwa mtu Kama wewe unayetaka kuanza hii biashara,sikushauri uanze moja kwa moja na biashara hii. Kwa sababu hao jamaa wenye hayo makampuni wana watu wao TBS na TRA, mzigo wako unaweza kupigwa zengwe na ukachomwa moto kwa kusingiziwa ni bidhaa feki. Wafanyabiashara wakubwa wanacheza rafu sana.

Kuna wakati niliagiza Steel beams kutoka Kenya nikapigwa ushuru wa ajabu sana. Halafu hao jamaa TRA wakaniambia siku hizi Steel beams haziagizwi kutoka nje, wakanielekeza kwa Huyo Muhindi ana kiwanda hapa Dar..na ndio supplier pekee. Kwa hiyo mambo Kama hayo yatakupa picha halisi ya biashara za kusafiri bila kufanya utafiti wa kina. Unaweza ukawa unaleta mzigo na kuuza kwa faida ndogo sana.
kila la kheri
nakubali kwa ushauri wako hata na mimi nimepata kitu kipya maana ninampango hapo baadae ya kufanya biashara huko huko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom