Biashara ya kuuza na kununua unga majani ya Mlonge

Biashara ya kuuza na kununua unga majani ya Mlonge

Gamariel

Member
Joined
Sep 8, 2009
Posts
82
Reaction score
6
Ndugu wana JF mwaka 2014 ndio umeshaanza hivyo na Kama vijana tunaanza kusaka fursa.

Nataka kujua kama kuna mtu anaifahamu biashara ya mlonge mti unaosifika kwa mengi.

Je unapatikana wapi Kwa wingi?
Je process ya kukausha majani yake ipoje?

Vipi kuhusu masoko yake ndani na nje ya nchi?

Je taratibu za kusafirisha mbegu au majani yaliyokaushwa ya mlonge nje ya nchi ni ipi?

Kama kuna anaejua faida na hasara ya kufanya biashara hii tujuzane.

Information is power lets share.
 
Ndg, hapa kwetu ichwankima chato kagera, wataalamu waliishia kutuuzia mbegu tu lakini hawakurudi kununua. Kuwa makini
 
Ndg, hapa kwetu ichwankima chato kagera, wataalamu waliishia kutuuzia mbegu tu lakini hawakurudi kununua. Kuwa makini

Najua kulikuwa na hilo sakata, nataka kujua kama kuna watu wanalima na kama kuna faida wanaipata
 
Wakuu, wana jf.
Mimi niko mkoani Dodoma lakini pia wakati mwingine huwa ninakuwa Dar.
Huku nilipo nina stock ya kutosha ya mbegu za mlonge.
Nilishakamua mafuta na kuwauzia mafuta watu kadhaa wa dar na morogoro lakini biashara haikuwa endelevu kwa sababu za hapa na pale.
Sasa nimeamua kuileta kwenu biashara hii ili niweze kupata mbinu, mikakati na soko la mafuta hayo. Tafadhali naomba maoni na ushauri toka kwenu.
Karibuni.
 
tujuze kwanza mafuta ya mlonge ya nini cha ziada zaidi ya mafuta mengine; binafsi najua ila sina uhakika kama wenzangu wanajua matumizi ya hayo mafuta;
Nambie unauza bei gani kwa lita .... plz tuma PM tuwasiliane privately - niko mwanza.
 
Tutaendelea kuwasiliana kwa PM ila kifupi tu ni kwamba mafuta ya mlonge yanatumika katika cosmetics industries kwa ajili ya nywele na ngozi.
Pia yanaweza kutumika kama tiba kwa mba, kuungua au kujikata.
Last but not least, mafuta haya yanaweza kutumika kwa kupikia.
N.B ningependa kufanya biashara na mtu anayejua matumizi ya mafuta haya.
 
Na biodiesel, lubricants. Tangazo lako lilipaswa kutaja ili uwapate walengwa mfano nauza mafuta.....yanatibu......chupa ukubwa.....kwa shilingi...... Namna hii utapata watu.

Kwanza samahani wote kwa kupotea kwa muda. Majukumu yalinibana kidogo ila nashukuru kwa michango yenu.
 
Na biodiesel, lubricants. Tangazo lako lilipaswa kutaja ili uwapate walengwa mfano nauza mafuta.....yanatibu......chupa ukubwa.....kwa shilingi...... Namna hii utapata watu.

Mama Joe nashukuru kwa mchango wako kwangu na kwa wana jf wengine ile unapohitajika mchango wa kijasiriamali.
Heshima kwako.
 
Niko Entebbe Uganda nigependa kupata mbegu, waweza nitumia???

Ndiyo mkuu, ninaweza kufanya hivyo. Niambie unahitaji kilo ngapi, unataka kuzipata kwa njia gani iliyo rahisi kwako kisha tufanye biashara.
Bei nitakupa kulingana na kiasi utakachohitaji.
 
Kuna kitu mtakuwa mme-note hapa.
Kuna KTN na Tiger, msishituke. Tuko pamoja na wote ni member, Malila ananifahamu physically. Mwenzangu yuko field huko hivyo ameniomba niingie kumsaidia. Hata namba ya simu ni yakwake. Yeye yuko Dodoma na mimi niko Dar, kote tunaweza kufanyia biashara.
 
mkuu kwanza ningekushauri kama unaweza cheki na TFDA ili kuweka mambo sawa then piga hela
 
Mimi ni agent wa mlonge kaskazini mwa Tanzania, nahitaji mbegu za mlonge (moringa oleiferfa) kwa kiasi kikubwa sana. Kwa kila kilo moja ninanunua kwa shilingi za kitanzania 1000/= na nitazifuata sehemu yeyote ile Tanzania na tuna mikataba kabisa ya kisheria tunayoingia na wakulima, ili tuje kuchukua mbegu zako ni lazima ziwe zimefika kilo 200, ila kama tumeshaingia mkataba tunaanza kulipa hata ukifikisha kilo hamsini.

Hii ni fursa ambayo mtanzania hatakiwi kuipoteza ili kukabiliana na maisha magumu kwani ndio zao pekee ambalo unaweza kupata faida kubwa ukilinganisha na mazao mengine ya biashara na chakula kwani kwa mfano huwezi uza mahindi kilo moja kwa shilingi 1000, pia ni zao linaloota kwa haraka na haliihitaji matunzo makubwa na linakomaa kwa mwaka mmoja tu. Pia tunaingia mkataba na wakulima ambao wana maeneo na wangepenga kuingia katika kilimo hiki, eneo liwe zaidi ya heka kumi, faida ya kuwa na shamba ni kwamba tunanunua kuanzia mizizi hadi maua kwa hiyo mkulima anapata faida kubwa sana. Nipigie chap chap tuanze kazi, 0759517174
 
Attachments

  • seeed.jpg
    seeed.jpg
    7.3 KB · Views: 385
Back
Top Bottom