Biashara ya Kutoa Mikopo (Microfinance): Hatua, Taratibu za Kufuata na Ushauri wa Uendeshaji

Ukirejea ktk sheria inayotoa mwongozo tunaojadili hapa ni wa taasisi ambazo ni *Non-Depositing Taking* sasa utaona ya kwamba
1. Kampuni na watu binafsi hawa wanaotoa mikopo wapo ktk kundi no 2 ie Tier 2
2. Kampuni au watu binafsi hawa wanaotoa mikopo inatambulika ni mikopo ya muda mfupi na pia ni ya dharula
3. Pia ktk kundi hili ie Tier 2 wapo ktk *high risk* ya kupotez pesa/mtaji kwa wateja kutokana na wateja husika hawana dhamana za maana
4. Wamewekwa kama mbadala wa "Tier 1 financial institutions" kusaidia kundi la wasio na sifa za kukopesheka ktk mabenki
5. Hivyo bhasi kwa hivyo vipengele no 1 hadi 4 wanakubalika kutoa mkopo kwa riba zaidi ya hy ya 17% kwani hata mikopo yao wanayotoa ni ya muda mfupi mfupi tofauti na mabenk ambayo mikopo yao ni ya muda mrefu.

(Tier 1 interest is charged annually VS Tier 2 interest is charged monthly)

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani Mkuu Laki Si Pesa

1. Kuna mambo nadhani ktk semina hy huenda hukuyaelewa au uliyaelewa zaidi ya usahihi wake
2. Hapa twajadili sheria inayotumika sasa 2019 na sio ya 1918
3. Mada hii inajadili Tier 2 na sio Tier 1,3 na 4(Hizi nazo tukipata wasaa na uzima tutaleta makala yake) ambako huko tutaangalia hadi uvushwaji wa madaraja au kushushwa kwa madaraja lkn kwa ushahidi wa kisheria na miongozo iliyopo
4. Weka hoja zako zikiwa na sapoti ya vielelezo vya masuala haya yanayojadiliwa hapa

Niwie radhi kama nimekukwaza


Sent using Jamii Forums mobile app

Mgawanyo wa makundi katika biashara ya microfinance (tiers) unazingatia uwezo Yaani mtaji na uendeshwaji wake

Tier 1 hili kundi linajumuisha deposit-taking institutions ambazo ni banks na microfinance banks.

Tier 2, kundi hili wanatoa mikopo tuu, hawaruhusiwi kuhifadhi pesa yoyote ya mteja kwa sababu yoyote (non deposits taking microfinance)

Tier 3, SACCOs

Tier 4, community financial groups

Kwa mtu anayeanza biashara akianzia tier 2 ni nzuri sio sababu ya mtaji mdogo (minimum capital) peke yake yake bali hata zile operational standards zinakua nafuu. Unapoingia moja kwa moja kwenye tier1 ujue organogram na office zako lazima viwe vya standard ya bank kadri ya muongozo wa regulator
 
Ahsante Sana kwa alieomba ushauri napia ahsante Sana kwa wote waliotoa michango yao mizuri. Kupitia muomba ushauri na washauri wenyewe, na Mimi nimepata ufahamu make hili linanihusu. Ahsante sana
 
Jambo kubwa katika biashara hii lipo katika utekelezaji. Ukiangalia msingi mkuu wa biashara hii ni SERA YA MIKOPO. Sera nyingi za mikopo hazikidhi vigezo vya uendeshaji wa hii biashara matokeo yake ndiyo hilo unalosema hapo juu.

Hii ina maana ya kwamba mchakato mzima kuanzia mteja kuomba mkopo, kukagua biashara au kazi anayofanya, vikao vya mkopo, uandikishaji wa dhamana, kiwango cha marejesho na hadi "recovery" iwapo mkopo haulipwi hazifuatwi. Kwa mantiki hy bhasi utaona mchakato mzima toka chini u akuwa umeshakosewa hvy tarajia changamoto kubwa ktk kulipwa laah uwe wasubiri uaminifu na uamuzi tu wa mdai kulipa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi naona hapo unapoamua kufungua ofisi ya mikopo ingekuwa vizuri zaidi ukachagua kundi mfano kina mama, hili kundi kidogo Ni waaminifu lakini kina Baba mbona utalia kilio cha mbwa?😃😃
 
Back
Top Bottom