Msaada: Nifanyeje ili usajili wa jina la biashara ziendane na huduma nitakazozitoa ikiwa ni pamoja na microfinance?

Shozylin

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
297
607
Wakuu nimekwama hapa ki mawazo nilikua naomba ufafanuzi.

Nilikuwa nasoma uzi mmoja humu unaoelezea mtu anaetaka kufungua microfinance wakati wa usajili sharti jina la biashara liwe na neno microfinance, microcredit, financial service, credit

Sasa mfano Mimi Nina Ninafanya huduma za kifedha za uwakala na nikawa nimeshasajili jina langu mfano shomile investment na Nina taka kusajili kampuni ambalo litazijumuisha huduma za kifedha ndani pamoja na microfinance ziende kwa jina moja

Utata unakuja kwamba nitatakiwa kusajili jina la biashara lingine ambalo litakua shomile company limited.? Ambalo litajumuisha huduma za kifedha

Au

Kampuni la microfinance litajitegemea na huduma za kifedha.?

Nifanyeje ili huduma hizi zikiwa zimezajiliwa ki sheria ziwe chini ya kampuni moja.?

Jina la biashara linaweza kubadilika.?

Nitumie jina gani ambalo likisimama litatambulisha huduma zote.?

Asanteni
 
Jumatatu asubuhi wapigie simu BRELA watakupa majibu ya maswali yako haya mepesi.
 
- Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), kuna mwongozo mpya wa maombi ya leseni ya biashara kwa watoa huduma ndogo za fedha bila kupokea amana (makampuni ya kukopesha) uliotolewa Juni 2020.

- Mwongozo huo unataka kuwa jina la kibiashara la mwombaji liwe na maneno yafuatayo:“Microfinance”, “Finance” “Financial Services” “Credit” au “Microcredit.

- Hivyo, kama unataka kufungua kampuni ya microfinance, unatakiwa kusajili jina la biashara linaloendana na shughuli hiyo. Kwa mfano,

Shomile Microfinance Company Limited au
Shomile Financial Services Limited.

- Kama tayari una jina la biashara lililosajiliwa, unaweza kulibadilisha kwa kufuata taratibu za BRELA. Unatakiwa kuomba mabadiliko ya jina la biashara na kulipa ada husika.

- Kama unataka kujumuisha huduma za kifedha ndani ya kampuni yako, unatakiwa kuainisha shughuli hizo katika MEMARTS au Katiba yako. Unaweza pia kuomba mabadiliko ya MEMARTS au Katiba yako kwa BRELA.

- Kwa kuongezea, unatakiwa kutimiza vigezo vingine vya mwongozo wa BOT, kama vile mtaji usiopungua shilingi milioni 20, elimu na utaalamu wa wajumbe wa bodi na mtendaji mkuu, sera ya mikopo, taarifa za fedha zilizokaguliwa, cheti cha TIN, nk.
 
Mkuu Asante Sana
 
Kwani ukitaka kufungua kampuni ya kutoa mikopo ni vigezo vp unatakiwa kufuata au kuwa navyo?
 
Habari, usajili wa majina ya biashara BRELA unafanyika moja kwa moja kupitia mtandao wetu wa ors.brela.go.tz, unaweza kufanya mabadiliko kwa jina la biashara ambalo tayari limekamilisha usajili moja kwa moja kupitia mtandao wetu wa BRELA ORS. Kutokana na shughuli ambayo unahitaji kufanya unatakiwa pia kuwasiliana na ofisi za Benki kuu ya Tanzania (BOT) kwaajili ya kupatiwa utaratibu na vigezo
Kwani ukitaka kufungua kampuni ya kutoa mikopo ni vigezo vp unatakiwa kufuata au kuwa navyo?
Habari, ilikuweza kusajili kampuni yako kwa biashara ya kukopesha fedha unatakiwa kuanzia BRELA kwa kusajili kampuni husika kupitia mtandao wetu wa ors.brela.go.tz kisha utatakiwa kufuatilia kibali kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT), baada ya kupata kibali kutoka BOT utatakiwa kufuatilia namba ya utambulisho wa mlipa kodi kutoka TRA na baada ya hapo utatakiwa kufanya maombi ya leseni ya biashara kutoka BRELA kupitia mtandao wetu wa business.go.tz
 
Back
Top Bottom