Biashara ya kunenepesha ng'ombe kuuza

Hii biashara ni nzuri ila ningependa kujua gharama za kumnenepesha huyo ng'ombe kwa miezi hiyo ni kiasi gani?
 
Hii ni story ndefu na ya kitaalamu. Ila, kwa kifupi, na ili kukusaidia nijibie maswali haya,kabla sijaendelea na story
1. Hapo ulipo, kuna mazao gani yanalimwa kwa wingi?
2. Kuna viwanda vinavyosindika mazao hayo? Na ni mazao yapi husindikwa
3. Kama hakuna viwanda, kuna maduka ya vyakula na dawa za mifugo karibu na unakofanyia ufugaji?
1.Alizeti na mtama (Dodoma)
2.Vipo vya kukamua alizeti tuu
3.Lipo duka moja tuu
Karibu mkuu....
 
Kwa kifupi,Maeneo kama Dodoma inawezekana kufanyika unenepeshaji kwa kutumia vyakula ulivyovitaja. Aidha kiwango cha faida kitatokana zaidi na bei ya vyakula. Asilimia 60 hadi 70 ya gharama za unenepeshaji hutokana na vyakula vya ziada,nje ya malisho kwa kuchunga au kuwaletea walipo.
Utakavyovipata kwa urahisi na bei nafuu,utarajie faida kuongezeka.
Maji ya kutosha kwa ajili ya kunywa mifugoni muhimu pia.
Dodoma ni sehemu kame hivyo malisho,maji,mazao na mabaki yake nafikiri yatakuwa kidogo.
Aina ya mazao uliyotaja yanapatikana huko yanaweza kutumika endapo kutaongezewa vitu vichache kuchanganyia. Kabla ya kushauri zaidi mchanganyiko, nipe bei kwa kilo ya mtama, na mashudu ya alizeti.
Mtama mara nyingi yanakuwa makubaliano na muuzaji,wanapima kwenye kopo(chibuku) hasa kwenye minada na bei ni kati ya sh. 200-1000 inategemeana na msimu wenyewe. kwa mfano sasa hivi tunaingia kwenye bei rahisi.
Mashudu hayana bei kamili kutokana na huku wanunuzi ni wachache,hivyo ni makubaliano kati ya mnunuzi na muuzaji na hata saa zingine hayapomwi. naweza kusema ni bei rahisi
 
Bandugu fursa nyingine hiyo mtaji mdogo tu kama m2 ivi, especially kwa wale wa mikoani, tafuta sehemu yako yenye marisho mazuri, nunua ng'ombe hata watano kwa lak 2 au 3 , walishe vizuri uza baada ya miezi 2 ivi wakinenepa vizuri hapo unaweza uza kwa lak 5 au 6 kwa kila ng'ombe.
kwa anaetaka kujikomboa na magu fursa hiyo hapo
Nawasilisha
Mkuu nilijua kuna namna ya kuwanenepesha kumbe ni majani tu, kama ni majani hapo ni bahati nasibu either anenepe au akonde.
Kama kuna njia artificial or natural za kunenepesha share nasi.
 
Nielewe. Nataka kufanya kitu kinaitwa uchanganyaji vyakula"feed formulation" kwa kutumia vitu vinavyopatikana kwa wingi. Chakula kitakachochanganywa lazima nijue gharama yake kwa kilo. Kujua gharama ya chakula hicho,lazima nijue vilivyomo vina bei gani? Mwisho nifanye financial analysis -mchanganuo wa gharama kifedha na vigezo vingine vya kitaalamu. Lengo ni kuona kama italipa au hailipi,ndipo nitoe ushauri ufanye au usifanye au iweje!
Ukisema ni rahisi tu, hiyo haitoshi.
Me nadhani ni vyema mkuu ukaleta hivyo vipimo na namna ya uchanganyaji wa hivyo vyakula kwa sababu Tanzania yetu kwa kawaida haina bei sahihi haswa katika mazao so tukisema tuanze mahesabu nitakuwa najidanganya kwa maana kijiji hiki naweza pata kwa bei fulani na kile bei ikawa tofauti.
Pia tukitoa gharama za hivyo vyakula kuna mambo ya usafiri na mengine mengi yatahusika hapo.
Mwisho wa siku kulingana na mazingira nilipo nitaweza kufanya upembuzi ili kujua kama itanilipa ama la. Lete mchanganuo mkuu.
 
Bandugu fursa nyingine hiyo mtaji mdogo tu kama m2 ivi, especially kwa wale wa mikoani, tafuta sehemu yako yenye marisho mazuri, nunua ng'ombe hata watano kwa lak 2 au 3 , walishe vizuri uza baada ya miezi 2 ivi wakinenepa vizuri hapo unaweza uza kwa lak 5 au 6 kwa kila ng'ombe.
kwa anaetaka kujikomboa na magu fursa hiyo hapo
Nawasilisha

= malisho
 
Mimi nimeanza msimu huu tayari nimenunua kama 50 hivi mwaka huu bei zilikua chini sana,bei ya juu kabisa nimenunua 130,000,kwangu ni biashara mpya ila nipo kwenye kuitafiti kuona changamoto na faida zake,kwa sasa naendelea kunenepesha kwani mvua zimeshaanza na malisho sasa yapo yakutosha
Unafanyia wapi
 
Very Good. Tunatakiwa kuchangamka namna hiyo,na usishangae ukaja uza 500,000/= kila mmoja. Kitakachokukwamisha ni kama utauza soko la ndani. Jitahidi uuze nje ya nchi watakapokuwa tayari. Takwimu za karibuni,zinaonyesha nyama inadoda kutokana na ukwasi. Mfano Dar,kuna maeneo kilo moja ya nyama ni Tsh 5500/= ambayo huko nyuma ilikuwa 8000/= hadi 9000/=. Ukipiga hesabu,ngombe wa kilo 250 (kwa ambao unao hawatafika hivyo),akichinjwa 48% ndio nyama sawa na kg 120*5500/= sawa na 66000. Ina maana atanunuliwa kama 400,000/ hivi mnadani Pugu. Ila huyohuyo ukimpeleka mf. Kenya,waweza kupata 600,000/= au zaidi.
Sijakupata naomba ufafanuzi
 
Mimi nimeanza msimu huu tayari nimenunua kama 50 hivi mwaka huu bei zilikua chini sana,bei ya juu kabisa nimenunua 130,000,kwangu ni biashara mpya ila nipo kwenye kuitafiti kuona changamoto na faida zake,kwa sasa naendelea kunenepesha kwani mvua zimeshaanza na malisho sasa yapo yakutosha
 
vp mkuu project yaendeleaje ikiwa mafanikio na changamoo ya hii project nahitaji jifunza
 
Back
Top Bottom