Biashara ya internet

Habari wanaJF,je ni ISP gani katika mkoa wa arusha anayetoa bandwith nzuri,kwa ajili ya matumizi ya internet café?naomba maoni yenu kwa wale mnaofahamu.ni bandwith kiasi gani itahitajika kwa mwezi?na inalipiwa kiasi gani?natanguliza shukrani.
 
Nataka kufungua kiji-cafe changu,nilienda kwa wazee wazima TTCL wamenizingua sasa naelekea kukata mwezi sijui kinachoendelea,mara waniambie njoo baada ya siku tatu,mara cabinet ya eneo lako mbovu yaani tabu tupu.So naomba mnijuze kama kuna ISP yeyote yuko cheap kama hawa ttcl ili niangalie alternative.Natanguliza shukrani
 
hao hao...komaa nao tu!!! kiubishi ubishi hivyo hivyo.
 
cafe hamna kitu siku hizi watu wanamaliza mambo yao kwa mobile tu.
 
Makre - Wenu,

Kama unataka kupata ISP mzuri , nenda Cats-Net limited, wako Samora Avenue,
Life House, 4th Floor.

4[SUP]th[/SUP] Floor NIC life House
Tel: +255-22-2113033
Sales Email : sales@cats-net.com
Mobile : (+255) 0785-091930
 
ttcl bado wazuri kuliko wote. Komaa nao tu! Hutapata wazuri zaidi ya wao labda kama wataka kufanya maamuzi ya hasira!
 
TTCL wazuri ndugu yangu, upo eneo gani nijaribu jinsi yakukusaidia,pia kuna huduma nzuri nitakupatia ambayo nakuhakikishia kwa siku hutokosa wateja 20 baada yakuzoeleka hasa kama upo maeneo ya town, but hii huduma lazima unipatie percent yangu. NB: sifanyi kazi TTCL 😀
 

hahaha bro mbona unajishitukia
 
cafe hamna kitu siku hizi watu wanamaliza mambo yao kwa mobile tu.
Acha fix weweeee?? Hata New Africa Hotel kuna Cafe, na hapo wanaoingia 99% wanazo izo mobile na bado cafe inajaa??
Zipo files & software hazisapoti kwa aina flani ya cm....na huwezi soma mafile makubwa ya applications zoote kwa kutumia CM.....kwani wewe huwa unaprint docs zako kwenye CM??...vipi kwa wale kwa mfano wanachuo....kuprint copi zaidi ya mia...wewe unatumia cm yako kufanya hayo??
Rekebisha post yako na uombe msamaa
 
Makre - Wenu,

Kama unataka kupata ISP mzuri , nenda Cats-Net limited, wako Samora Avenue,
Life House, 4th Floor.

4[SUP]th[/SUP] Floor NIC life House
Tel: +255-22-2113033
Sales Email : sales@cats-net.com
Mobile : (+255) 0785-091930

TTCL mzee....mpaka 100,000/ ya 1mbps monthly...na unaweza kutumia com zaidi ya 9, na speed iko poa
 
Asanteni sana waungwana kwa michango yenu,kwa mujibu wa maelezo yenu inaashiria ttcl ni MTAKUJA,sina budi kuwavumilia
 

nipo mikochen A karibu maeneo jiran na shoppers plaza.niPM please kama unanamna ya kunisaidia,natanguliza shukran mkuu
 
Ndugu yangu anataka kuanzisha biashara ya Internet cafe pale Morogoro Mjini. Ingawa bado hajapaelewa sana juu ya utumiaji / uhitaji wa huduma hii pale.
Lakini vile vile, anafahamu TTCL ndiye pekee wanaoweza kumsaidia kumuuzia muda wa internet (hasa ile huduma yao ya NDUKI).

Tafadhali, nimeombwa nimshauri, mimi pia sijaipata kazi hii vema, hebu nipeni taarifa juu ya hayo na zaidi mnayofahamu juu ya biashara hii ya Internet cafe.

Thank you.
 
Hii biashara sasa hivi inashuka umaarufu wake kutokana na watu wengi kufanya mawasiliano yao ya internet kupitia simu za mkononi. Huenda baadae ikafa kabisa kama ilivyokufa biashara ya kupigisha simu vibandani baada ya watu wengi kumiliki simu, na ushindani kushusha gharama za upigaji. Ningeshauri aangalie biashara ambayo itaendelea kupata umaarufu hata baada ya miaka kupita.
 
Too late!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…