Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 38,026
Hapo kwenye red nakubaliana na wewe ni kweli kuwa mfanyakazi ofisini lets say PPF tower ndo ofisi yake AKANUNUE GUTA, HATAKUBALI SIMPLY BECAUSE GUTA NA PPF TOWER ''WHERE AND WHERE'' I mean wapi na wapi?Aisee ukimwambia mtu yeyote anayefanya kazi maofisini akanunue guta atakushangaa sana! Lakini ukiangalia it really make sense.
Hizi biashara za magari ni nuksi sana aisee. hasa kama na wewe tajiri hujui spea za magari. yaani utafilisika.
nakumbuka yalinikumba haya haya ya mkuu hapo juu. nilinunua Hiace 14m baada ya miezi miwili niliuza 8m huku nikiwa nimeshaingia gharama zaidi ya 1.5m. its better ukajenga nyumba kama una mtaji
kaka pole, mimi miaka 3 iliyopita nilinunua saloon car 2 - ili nifanye taxi - kaka yalinikuta ya musa- hakuna hesabu yoyote gari zote zina matatizo kila baada ya siku mbili - matokeo yake mshahara wangu ukawa unaishia kutengeneza hivyo vimeo viwili. kwa hasira kimoja nikampa fundi wangu kwa hasira - kingine nikauza laki 7 pesa zote nikampelea mzee wangu. toka hapo sitaki kusikia taxi - bajaji au hiace. unaweza kufa siku si zako
Kila biashara/shughuri yoyote ina ugumu na karaha zake.
Biashara ya daladala inalipa na ni nzuri kwa wale wasio na muda mchana .As rule of thumb. HIACE (Tajiri=24days x 45,000/=, Service= 2days x 45,000/=, trafic&sumatra&majembe=2days x 45,000/=, Dereva= 2days x 45,000/=).Break even ni 22months.
Hayo ndiyo mahesabu ya makadirio kwa uzoefu.
Katika utafiti nilioufanya wamiliki wa daladala wanaoendelea vizuri wanafanya yafuatayo bila kukosa.
1.Hakikisha siku ya service gari inatengenezwa vizuri na unasimamia.Gari yako
iwe nzima sana.(pesa ya gari si yako hadi utakaporudisha mtaji).
1.Mafuta full tank ni ya tajiri, yanakaguriwa kituo cha mafuta au anapopaki
daily.
2.Leseni na certificate vyote original anashika tajiri
3.Mshahara kwa mwezi kwa hiace ni 50,000/= coaster ni 90,000/= kwa mwezi.
4.Akilete hesabu pungufu, akipoteza suti, jeki, spanner au uzembe wowote
unaandika deni anakatwa mwisho wa mwezi.
5.Ajira yake iwe na referee,barua ya mjumbe , na ujue kwake na awe ameoa.
6.Ukiendesha gari kwa miezi 30 fikiria kuuza , kwa kuwa hiyo ndo faida safi.
7.Chagua garage 2 zenye mafundi unaowaamini ili ukipigiwa simu, nawe unawaelekeza dereve apeleke garage unatakayo mwambia, DEREVA ASIPEWE MADARAKA YA KUTENGENEZA GARI YAKO
Hayo machache, pia maguta yana karaha/kero sana , ila ukifanya kama ndo maisha yako inakutoa kama vile daladala.
Mkuu pole sana
Tafuta vijana uwatrain halafu uwape magari hayo, hao walioacha au kuacchika sehemu zingine watakupasua kichwa kama unavyosema.
Mimi pia nafikiria kuingia kwenye hiyo Industry, nini ushauri wako? Nina jamaa yangu anazo daladala tatu yeye anawachukua watu anawapeleka driving halafu anawapa magari yake
Vijana anawachukua bush sehemu aliyotokea yeye (Njombe), the way alivyowajenga wanaona wao ni sehemu ya biashara hiyo hata kama gari linashida wanatoa taarifa mapema sana na wakifikia target/month anawareward kidogo. Kabla ya hapo alichukua wahuni wa hapa mjini ilikuwa wakishapata pesa yao tu wanaanza kupiga simu gari limekufa mara wamekamatwa ilikuwa balaa.kama hautosimamia mwenyewe,i.e fulltime management nakushauri ufanya investment ktk secta nyingine. huyo jamaa anayewapa trainning anawatoa bush au anawachukua vijana hapa town?
Vijana anawachukua bush sehemu aliyotokea yeye (Njombe), the way alivyowajenga wanaona wao ni sehemu ya biashara hiyo hata kama gari linashida wanatoa taarifa mapema sana na wakifikia target/month anawareward kidogo. Kabla ya hapo alichukua wahuni wa hapa mjini ilikuwa wakishapata pesa yao tu wanaanza kupiga simu gari limekufa mara wamekamatwa ilikuwa balaa.
JF MEMBERS,
biashara ya dala dala inanipasua kichwa,gari ziko mbili.(24 seats)
tatizo :madereva kila siku story,mafuta hawaweki.(utaskia Boss msingi wa mafuta umekata)wakiweka mafuta quality ya mafuta mbovu nahisi ni mafuta ya videbe.
Ma-Traffic ndo usiseme pasua kichwa.
Nimegundua kuwa hata nami naanza kubadilika tabia nakuwa kama machizi wa hii Dala-Dala industry.
Kama kuna mtu ameweza kuifanya hii biashara successfully anisaidie kumanage hii biashara kwa makato ya management fees.
JF MEMBERS,
biashara ya dala dala inanipasua kichwa,gari ziko mbili.(24 seats)
tatizo :madereva kila siku story,mafuta hawaweki.(utaskia Boss msingi wa mafuta umekata)wakiweka mafuta quality ya mafuta mbovu nahisi ni mafuta ya videbe.
Ma-Traffic ndo usiseme pasua kichwa.
Nimegundua kuwa hata nami naanza kubadilika tabia nakuwa kama machizi wa hii Dala-Dala industry.
Kama kuna mtu ameweza kuifanya hii biashara successfully anisaidie kumanage hii biashara kwa makato ya management fees.