Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Lesseni Tsh. 48000/= na Ushuru Lazima ulipie Kila Gunia lililo teari kusafirishwa kabla ya kulitioa sehemu husika.
Kiongozi Asante kwa maelezo yaliyonyooka....Nataka kujua kuhusu Leseni natakiwa kukata nikiwa huko au nakuja nayo ninakofanyia Bishara
 
Huko Huko
Asante kaka....Nina mawasiliano yako.....kuna dogo 1 amemaliza chuo ana kamtaji kake anasaka Fursa nitamshirikisha...ila hebu niambie kwakuwa ww uko pale siku nyingi unajuana mengi kwa MTU mwenye mtaji mdogo anaweza kupata usafiri wa kuchanga na watu wengine?.....
 
Asante kaka....Nina mawasiliano yako.....kuna dogo 1 amemaliza chuo ana kamtaji kake anasaka Fursa nitamshirikisha...ila hebu niambie kwakuwa ww uko pale siku nyingi unajuana mengi kwa MTU mwenye mtaji mdogo anaweza kupata usafiri wa kuchanga na watu wengine?.....
Yeah Mtachangia Gari ili kujaza Gari Zima kama vile Fuso ,Tundum n.k Itategemea Gari inahitaji Jumla gunia ngapi ili kujaa . Ondoa shaka kuhusu Transport shida Ni soko Weka mazingira mazuri ya soko kwanza, Kwan suala la mzigo halina Tabu.
 
Yeah Mtachangia Gari ili kujaza Gari Zima kama vile Fuso ,Tundum n.k Itategemea Gari inahitaji Jumla gunia ngapi ili kujaa . Ondoa shaka kuhusu Transport shida Ni soko Weka mazingira mazuri ya soko kwanza, Kwan suala la mzigo halina Tabu.
Asante sana Kiongozi umeeleweka!!
 
HABARI ZENU WAKUU
Ni Muda WA Miezi Mitano sasa Toka nihitimu Chuo pale Chuo kikuu cha Mtakatifu Agostino (Mwanza) Tawi kuu. Namshukru Mungu nkapata Degree yangu ya Kwanza ya Falsafa na Elimu, lakini kwa kipindi chote hicho mpaka Sasa hivi nafanya Temporary work kwa Rafiki yang kipenzi (Boss Fulani) mmiliki WA Magari kadhaa ya mizigo na Mnunuzi WA Tani za Dagaa kutoka mikoa ya Mara na Mwanza.

Kiukweli Nje ya Business ya Magari ya Mizigo ( Semi - Trailers) especially Scania R 420 , 114 n.k Jamaa hyu Business ya Dagaa inamlipa Sana kuliko Magari na PIA sisi kama wasimamizi wake Maisha yanaenda japo kazi Ni Ngumu ILA masilahi yapo .
Biashara hii Dagaa hufanywa kwa kuchukua Dagaa kutoka huku na kupelekwa Dar, Congo, Tunduma, Arusha na kwingineko Na inalipa Sana ukizingatia yafuatayo, Mtaji, Soko, Muda WA kusimamia na juhudi na watu (Social capital), n.k

Mimi kesho na kesho na kesho ntaka Nijipange na nianze Mdogo mdogo
Karibuni Musoma karibuni Kwenye Dagaa. Tafadhali Mchanganuo kama ifuatavo; Dagaa inayonunulia Ni Dagaa chafu (Chakula ya kuku) na Dagaa safi Chakula ya Binadam
1. Chakula ya kuku Inauzwa kwa Dumu Yan ndoo ya Litre 20 , Mara nyingi dagaa hii ya Chakula ya kuku huuzwa kwa Tsh. Elfu 10,000/= mpaka Elfu sita na Mia Tano kwa Kama Dagaa imepatikana nyingi Sana bei yake hususha Automatically Kwan kwenye Masoko Hufurika Sana.


UANDAAJI Chakula ya kuku huandaliwa kwa kuwekwa kwenye Gunia kubwa ambapo Kila gunia hubeba Dumu 21 na @ Gunia likipimwa hutoa kilo kuanzia 120- 95.

USAFIRI Baada ya kuandaliwa na kuwa tayari hupakiwa kwenye Magari ya mizigo na kupelekwa Kwenye Masoko kama vile Dar, Congo,Tunduma, Arusha n.k . bei ya Usafiri Inategemea Mzigo Wako na PIA Maelewano na Mwenye Gari lakini kama Semi- Trailer lenye Contena Kama vile Scania R420 Mara nyingi hubeba Gunia 270 na hapo hutegemea upakiaji WA Makuli husika Na bei hapa Kwa Gari huwa Ni one million and point six 1,600,000/=.

BEI kiwandani dagaa hizi huuzwa kwa kilo ambapo Kilo Ni 3500- 2500 Inategemea Upatikanaji WA Bidhaa na Kiwanda husika.
Kwa hyo gunia Lenye Dumu 21, Na lenye Thamani ya Tsh. 210,000= na Gharama ya 25,000 Uaandaji usafiri , ushuru na Mengineyo na lenye kilo 120 Ambapo @ kilo 3500- 2500 .
Hapo ukipiga Hesabu utakuta kwamba Ni
120*3500= 420000
420000- 235000= 185000
Au 95*2500= 237500 Kama Dagaa umeinunua kwa bei nzuri na umebana Mapato saswa Sawa.

MASOKO
kwa Dar ndo habari yake Kwan ndo Viwanda vingi vya Chakula ya kuku hupatikana Hasa kwa Falcon, Kitunda kwa Matinde few to mention just Na hapa kwenye vizuri kufatilia mwenyewe kuepusha madalali na matapeli WA mujini , Nakaribisha Kitu Maswali, Matusi,Kejeli na Mengine

MAWASILIANO

0767258286/0789258286/0673258086

KARIBUNI MUSOMA KWENYE DAGAA WA CHAFU (CHAKULA YA KUKU).
Kuna mahali umesema hii biashara ni ya Mzee na kaka yako sasa lipi ni lipi
 
Kuna mahali umesema hii biashara ni ya Mzee na kaka yako sasa lipi ni lipi
Samahani Mkuu Kwani Shida Yako nini ?
Hapana sio ya Mzee Wangu wala kaka yangu isipokua anaeifanya Ni Rafiki yang kipenzi kwenye Company yake ndiko nilikokua nafanya na kupata Ujuzi wote kuhusu Biashara za Ziwani.
 
Samahani Mkuu Kwani Shida Yako nini ?
Hapana sio ya Mzee Wangu wala kaka yangu isipokua anaeifanya Ni Rafiki yang kipenzi kwenye Company yake ndiko nilikokua nafanya na kupata Ujuzi wote kuhusu Biashara za Ziwani.
Kule ulikuwa unadanganya kwanini?
 
Kule ulikuwa unadanganya kwanini?
Ndugu yangu kata maneno ya hicho kipande Afu kitengenezee Uzi humu humu Jf au kilete hapa Acha utoto basi kama nimedanganya wee kimekuuma nini ?
Kupitia huu mpaka sasa hv Kuna Watu nshawaunganisha wameshaanza Biashara .
 
Rejea kwenye kichwa cha habari hapo juu.
Kwa yeyote anaye hitaji mzigo huo anitaarifu ili aweze kujipatia Dagaa watamu na waliokaangwa , bei ni poa kabisa wote mnakaribishwa
 
Jamani naombeni ushauri wenu. Binafsi napenda sana nianze biashara ya Dagaa wabichi niwakaange na kuwatafutia soko. Ila sijajua faida na hasara yake ipoje. Na ni wapi wanapendwa sana ila pia bei yake sokoni ipoje na kadhalika. Napenda sana nianze hiyo biashara. Naombeni ushauri wenu nianzeje wandugu.
 
Naomba nikuulize hapo ulipo dagaa zipo? if yes, basi nakuhakikishia kuwa hiyo biashara ina lipa sana cha muhimu uwe makini kwenye packing
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom