Habari wanaungwana,
Ningependa kujua zaidi kuhusu biashara ya bwawa la samaki. Ningependa kujuzwa kuhusu yafuatayo:
1. Ni samaki gani ni bora kwa biashara hii?
2. Gharama za kuanzisha bwawa ni nini?
3. Ni vifaa gani vinahitajika kwa ajili ya bwawa?
4. Je, biashara hii ina faida gani na changamoto zipi?
5. Soko la samaki linapatikana wapi?
Mimi ni mdau (mtaalamu) wa ufugaji samaki nina uzoefu wa miaka 4, naomba kuchangia kidogo kwenye hii mada
ufugaji samaki unafaida endapo utafanyika kwa usahihi
1. Samaki bora zaidi kwa ufugaji wa kibiashara ni sato kwa sababu ndio samaki wanaopendwa zaidi, bei yake ni kati ya 10,000 hadi 14,000
2. Gharama za bwawa inategemea na size ya bwawa unalotaka kuchimba au kujenga na aina la bwawa unalotaka kutumia kuna mabwawa ya aina tatu:
I. Bwawa la udogo (Earthen Pond) hili ni nafuu zaidi lakini ni muhimu ardhi yako iwe ya mfinyazi isiyoruhusu maji kupotea kwa haraka
II. Bwawa la kuhamishika (Mobile Pond) Hii ni aina ya bwawa linalotengeneza kwa kutumia pond liner (nylon sheets) au plastic
III. Bwawa la kujengea, aina hii ya bwawa ni yale yanayojegwa kwa cements na totally
Aina ya bwawa utakalo tumia ndio litadetemine gharama
4. Changamoto za ufugaji samaki:
I. Gharama kubwa ya chakula, kilo moja ya chakula cha samaki cha kununua dukani ni kati ya Tsh 3,500 hadi 6,000. Gharama hii inapunguza faida hivyo ni vizuri ujifunze kutengeneza chakula chako mwenyewe ili kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi na kujiongezea faida
II. Mbegu, baadha ya wafugaji wanafuga mbegu zisizofaa kufuga na kupelekea samaki kutokua ndani ya muda uliokusudiwa
III. Maji, vyanzo vya maji wakati mwingine sio vya uhakika havimpi mfugaji uhakika wa kupata maji kwa kipindi chote cha uzalishaji (production cycle)
IV. Usimamizi mbovu, baadha ya miradi inaendesha kienyeji bila muda sahihi wa kulisha, muda wa kubadilisha maji n.k
5. Mahitaji ya samaki ni makubwa sana ukilinganisha na mahitaji, unaweza ukauzia samaki wako hapo hapo unapofugia au ukauzia kwenye soko lolote lililojirani na ulipo