Biashara ya BOOKSHOP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya BOOKSHOP

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by kanyagio, May 22, 2011.

 1. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  wanajamii, kuna rafiki yangu nilikuwa naongea naye weekend hii, anaishi nje ya nchi ila anataka kurudi Tanzania na kuwekeza. mojawapo ya business idea ni kufungua BOOKSHOP,. sasa wanandugu kwa kuzingatia kuwa watanzania wengi hawana mwamko wa kusoma, Je biashara hii inaweza kulipa? na kama inaweza kulipa je wapi ni location nzuri.. na vitabu vinakuwa sourced wapi.. wenye mawazo ya kujenga naomba ushauri wenu ili nami nimshauri huyu rafiki yangu
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kama umefikia conclusion kuwa Watanzania wengi hawana mwamko wa kusoma, sidhani kama Bookshop inaweza kulipa. Labda upate tenda ya kuuza vitabu na vifaa hewa kwenye halmashauri za wilaya, the cost of which, you will be moving very close to Dr. Edward Hosea.
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ni kweli kabisa. Kuna library za mikoa. Akisema afungue karibu na shule, mashuleni pia wana libraries zao.
  Namshauri afungue laboratory watoto wa shule wakajifunze practicals maana mashule mengi swala la practicals linawasumbua.
   
 4. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Mkuu bora ungefungua gesti tu, wabongo ni ngono tu,baas! habari za kusoma haihuu! vitabu vitaishia kuliwa na panya na mende tu.
   
 5. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Biashara ya BOOKSHOP inalipa asa akiwa anadeal na vitabu vya A level na vya colleges. But to make it profitable lazima a outsorce these books from India.
  Cause they are cheaper,nilipokuwa India Vitabu vya Dola Mia apa Tanzania unaviuza na kupata faida mpaka dola 70.Ni ukweli usiofichika kuwa now we have more than 10 unversities and Many Colleges apa Tanzania and books are needed badly,pia shule za secondary ni nyingi kwa sasa
  BUT NEW BUSINESS TECHNIQUES ARE NEEDED TO MAKE THIS PROJECT TO GENERATE SUPPER PROFIT
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  khaaa!
   
 7. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Hapa tunaongelea serious business nisubiri kule chit chat kwa ajili ya porojo.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kuna majukwaa inabidi upigwe ban aisee maana unachafua hali ya hewa.
   
 9. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Hivi ushawahi kuskia gesti ikafungwa bongo kwa kukosa wateja?, haya jibu kwa hoja. Leo ndio utajua kwamba mimi nina share zangu kwenye kampuni ya microsofti
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  gesti sijui. Niulize hoteli.
   
 11. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwanza mwambie jamaa yako afanye Karesearch kadogo kuhusu hiyo Biashara ya Vitabu, kwani zaidi ya kwamba this is a noble course kwa nchi yetu, lakini pia technology imebadilisha ule mtazamo wa zamani waa library. Asikuongopee mtu ndugu yangu, kwa nchi kama Tanzania, nchi ambayo inapolicy ya kufungua shule za kata tu lakini hawana policy ya kusupply vitabu au lab, hii biashara inaweza ikawa na mafanyikio sana.

  Pia, isiwe vitabu tu peke yake. Mtu anaweza kuanzisha Bookstore yenye access na some Academic Journals au E-books copy (Hello Internet!!!), jambo ambalo linaweza kusaaidia watu wengi ambao labda hawana uwezo wa kununua hard copy books.
  Natumaini kwamba jamaa yako akifanya Business Research ya huu mradi mambo yanaweza kuwa poa. Pale Arusha kuna duka la vitabu la miaka mingi sana, nadhani linaitwa CASE BOOKSTORE. Hawa ndio watu wakuwaona ili kujuwa jinsi walivyoweza kudumu kwa miaka mingi kwenye hiyo biashara.


  NB: Mkuu kumbuka kwamba Kielimu katka nchi 3 za Afrika Mashariki, Tanzania ndio inayotoa wanafunzi wachache kuliko Kenya na Uganda kwenye Higher Lerning Institutions zetu. (probabily less than 6,000).Hivyo basi, hii nji ya wadanganyika inahitaji maduka mengi sana ya VITABU na inaweza kuwa biashara nzuri sana.
   
 12. babalao

  babalao Forum Spammer

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ushauri wangu tafuta mtu anayeendesha bookshop akupe siri za biashara kabla ya kuanza, kama hujampata nitafute nitakuelekeza mahala pa kumpata kwa sababu ninao marafiki/wateja wangu wengi wanaofanya biashara ya vitabu na wanauza vitabu vyangu vya mbinu za biashara.
   
 13. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Ngoja niamke kwanza.
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tuwe wakweli jamani:

  Fact ni kuwa Watanzania hatusomi, hatusomi kabisa kama mtu anasoma gazeti basi ujue ni gazeti la kufumua skandali za watu, kama yuko kwenye desktop basi ni facebook etc.

  Ukweli huu unadhihirika na yafuatayo Dar Es Salaam mji wenye watu zaidi ya milioni nne na nusu, shule za msingi zaidi ya mia ,shule za sekondari kadhaa , vyuo vikuu saba kuna bookshop za vitabu vya kiada sio zaidi ya tano. Maana yake kuwakwa kila bookshop moja inahudumia watu milioni moja.

  Ndio maana pamoja na Dar es Salaam kupanuka sana ukilinganisha na miaka 20 iliyopita mpaka leo maktaba yetu ya Taifa haijaongezwa both horizontal. vertically au hata kuweka branchs kwenye surbubs za jiji. Hii ni kiashiria tosha kuwa hatusomi.

  Wanunuzi wakubwa wa vitabu ni wanafunzi both A level, O level na vyuo, niambie ni mwanafunzi gani wa chuo kikuu umemuona anaingia bookshop na kununua kitabu kipya? Ni wanavyuo wangapi waliomaliza na kuanza kazi unawakuta wanatumia reference ya vitabu vyao binafsi walivyonunua wakiwa wanafunzi? I swear in every 100 students unaweza kupata watatu.

  Hali hii juu ina apply pia kwa wanafunzi wa sekondari both A and O level. Tell me when did your son, daughter, young brotheror sister buy a textbook from the pocketmoney that you provide?

  When did any of us buy a textbook for reference in the office, we all go for novels and other funny stuff.

  Ningemshauri rafiki yako aanzishe NGO ya kuhamasisha watu kusoma na hii ianzie shule za awali, majumbani, msingi, sekondari, majumbani vyuo na vyuo vya juu, baada ya hapo ndio aanzishe maduka ya vitabu.
   
 15. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mh jamani Watanzania hawasomi km wengine walivyosema. Unamkuta mtu anaishia kusoma vipower point pre (slide) mwanafunzi wa master kisha akajibu mtihani. Hata novel hawasomi. Niliwahi kufika nchi moja huko, kwenye public transport unakuta watu wanasoma vitabu lakini kwetu hakuna kitu km hicho. Wakijitahidi ni magazeti ya udaku. Huenda ndio maana tunadharaulika. Hivi wewe ujiite lawyer au accountant, financial analysts mara ya mwisho kusoma kitabu ni siku ya mtihani. Tuna tatizo kubwa sn na walimu wetu wanachangia kwa kiasi kikubwa. Kwanini hawawaambiwi wanafunzi wasome vitabu hata hivyo vichache vilivyopo?
   
 16. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wafanyabiashara wawili walikutana na kujadiliana juu ya biashara wanazoweza kufanya Afrika, mmoja akamweleza mwezake kwamba anataka kuleta viatu Afrika; mwenzie akamwambia usipeleke viatu Afrika kwasababu hawajui kuvaa viatu (enzi hizo). Huyu jamaa akasema hiyo itakuwa ni fursa nzuri kwani ataleta viatu bure na kuwafundisha jinsi ya kuvaa, baada ya hapo ataleta kuuza.

  Hivyo basi rafiki yako atalazimika kutengeneza mazingira ya kuwafanya watanzania wengi kusoma vitabu halafu anaanza kuuza vitabu.
   
 17. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  mgombezi i like your example.. bravo
   
 18. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza futa wazo kuwa watanzania WENGI hawana mwamko wa kusoma nazani hiyo research analysis ni wrong.Aje Tanzania akifika aende bbokshop yoyote aombe number simu za booksellers association ,akifika hapo atapata kila aina ya msaada anao taka.
   
 19. w

  wanan Senior Member

  #19
  May 25, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  jaman ukweli kwamba biashara ya vitabu tanzania inalipa tatizo la watanzania wanapenda kufahamishwa kitabu kizuri chenye manufa kwake,mfano lecture wakijuwa anatumia kitabu gani wote watanunua hiko kitabu.hawapendi usumbufu sana,vitabu ambayo unaweza kufanya biashara tanzania.
  1.ambayo vipo kwenye mtalaa wa serikali-msingi & SECONDARY
  2.uhasibu books vya acca,cima na cpa
  3.science books vya a.level na chuo
  4.novel za mapenzi.
  5.pia vya watoto
  nakutakia mafanikio mema
   
 20. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  aisee ahsanteni kwa maoni.. mimi naona huyu jamaa anaweza kufanya static and mobile bookshop nikiwa na maana kwamba unakuwa na bookshop somewhere.. then wakati mwingine unaenda kwenye maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi ku-market bookshop na kuuza vitabu!! what do u think guyz!!
   
Loading...