Biashara sio kwa ajili ya Kila mtu

Biashara sio kwa ajili ya Kila mtu

Jane Msowoya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2017
Posts
4,824
Reaction score
9,017
Biashara Zina mambo mengi sana hasa ukiwa unafanya biashara za ku build legacy,
Kuanzia Team to suppliers to distributors yaani ni kulala macho tu mpaka mambo yaende

Nashauri kama wewe ni wale watu soft skin usiingie kwenye biashara baki huko huko kwenye ajira au fungua zako pub weka pisi za kwenda basi relax

Niwatakie weekend njema

Biashara inabidi uwe mwamba kweli kweli sio sisi ambao unanunua tu powerself unasema hutu tukiisha kwenye kabox nitakuwa na ka laki kangu niongeze mtaji mpaka nifungue kapharmacy ila sasa ukiuza hata moja tayari koo linakuuliza what's up my nigga?

Unajikuta huna jinsi inabidi ukalewe unasema kesho nikivizia tugonjwa hapa ofisini sitainywa mara ukiuza tena unasikia kwa mzee shirima wamechinja nyama imenona unasema walau nitaanza kesho wacha hii elfu tano nikaile nyama maana jana nimelewa sana mwisho na mtaji wenyewe unakuwa umeishia tumboni kwangu .

Biashara ni ya wamba sio sisi wa what is biology ndugu
 
sijawahi kuingia wala kufanya biashara... nataka niingie rasmi, nifungue biashara ya duka la Mangi.
mnafanya nibaki njia panda!
Duka la mangi:

Hakikisha, sukari, unga wa ngano, unga wa sembe, dona, maharagwe na vitu vya kupima pima kwenye mzani havikauki dukani kwako kwa sababu hapa ndipo biashara ilipo

Vitu vya kwenye maboksi ni zuga tu
 
Biashara Zina mambo mengi sana hasa ukiwa unafanya biashara za ku build legacy,
Kuanzia Team to suppliers to distributors yaani ni kulala macho tu mpaka mambo yaende

Nashauri kama wewe ni wale watu soft skin usiingie kwenye biashara baki huko huko kwenye ajira au fungua zako pub weka pisi za kwenda basi relax

Niwatakie weekend njema

View attachment 3533933
Pub zote ninazopitia hizo pisi kali unazosema hazikai miezi miwili.
 
Kwa kwel,biashara hazihitaji lele mama

Kama ulihudumiwa mahitaji yako na wazazi au serikali( mshahara) ukiwa na umri mpaka wa miaka 25+ automatic wew biashara hautaiweza kamwe
Biashara ili nitembeza KUTOKA mlandege Hadi bubuu nakurusi kupitia mtoni mess nachapa Hadi kidatu nasonga Hadi AMANI NARUDI mlandege KWA MIGUU JUA Kali mvua acha tu MKUU, all in all MUNGU amuachi MWENYE bidii na maombi
 
Biashara Zina mambo mengi sana hasa ukiwa unafanya biashara za ku build legacy,
Kuanzia Team to suppliers to distributors yaani ni kulala macho tu mpaka mambo yaende

Nashauri kama wewe ni wale watu soft skin usiingie kwenye biashara baki huko huko kwenye ajira au fungua zako pub weka pisi za kwenda basi relax

Niwatakie weekend njema

View attachment 3533933
Biashara za ku build legacy ndio tamu sasa
Vitu vyangu hivi
 
Sasa hiyo legacy inakusaidia nini?
Satisfaction. Hiyo ni personal sasa.
Ni sawa na ambavyo huwa sioni mpira unaweza nisaidia nini, ila siwezi hoji wanaoshabikia unawasaidia nini.

Mtu kama Sauli aliyekufa hata kaburi halijatitia tiyari mabasi hayapo barabarani tena mara familia ina ugomvi wa mali namchukulia tofauti sana na mtu mwenye shamba lake na hoteli ndogo aliyefariki mwaka 2000 akaacha hizo Mali kwa familia wakazikuza na kutumia kama mtaji wa biashara nyinginezo walizonazo sasa. Old money is always the best, sio kila kizazi kikija kianze upya.
 
Back
Top Bottom