Biashara ni alternative ya wakosa ajira

Biashara ni alternative ya wakosa ajira

Screenshot_20250322-160257_WhatsApp.jpg
 
Kumachawa ww biashara utaifanya bila mtaji unadhan wote wanaolalamika ajira hawana mawazo ya kufanya biashara kama mtu hana hata hela ya vocha jero na anaish kwao hiyo biashara anaifanyaje au ndo utaleta porojo za kuwa winga au siyo.
 
Kijana ukikosa ajira acha kulia lia tafuta biashara uwe unafanya.
Biashara ina hela sana
Kila kitu huwa kina maandalizi yake . Nasema hivi kwa sababu ukiangalia asilimia kubwa ya elimu yetu imejikita kwenye kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri. Lakini pia familia nyingi ni maskini kiasi kwamba wanapambana watoto wao wapate elimu angalau waje waajiriwe ili kujikomboa na kuikomboa familia. Biashara inatakiwa maadalizi pia kuanzia namna ya uendeshaji na changamoto kubwa kwa watanzania ni mtaji. Kama nilivyosema familia nyingi ni maskini hivo hata mtaji ni changamoto. Pili biashara huingii kichwa kichwa ni kitu ambacho lazima uwe umefanya tafiti ya kutosha maana hakuna biashara mpya utakayokuja nayo kwa sasa ukajikuta upo peke yako. Mfano mdogo juice sasa hivi kuna wafanyabiashara wakubwa tu na teknolojia zao wanapambana yupo Azam, Mo, Jambo na wengine. Ukisema maziwa kuna Tanga Fresh, Asas . Ukisema mkate Azam humkosi.Hiyo ni mifano midogo tu ambapo kwa mtu ambaye anataka kweli biashara ni kuwa na mtaji mkubwa na utaalamu wa kutosha. Ukisema labda nguo hapo pia mtaji unahitajika lasivyo utakuwa na fremu zenye nguo chcche na hatimaye tozo zikakushinda lipa.
Nadhani ni vyema ukawepo mkakati wa kitaifa wa kuinua sekta binafsi waweze kuwekeza zaidi itasaidia kupunguza ukosefu wa ajira maana wapo ambao watapata ajira moja kwa moja kwenye viwandakwa ajili ya uzalishaji lakini pia wapo ambao watapata fursa ya kuzalisha malighafi kwa ajili ya viwanda, wapo watakaopata fursa ya kusafirisha na hatimaye wapo ambao sasa wanaweza pata fursa ya kuuza bidhaa hizo.
Kingine ni kuwepo na mkakati wa serikali kuwatafutia fursa wafanyabiashara/vijana wetu masoko nje ya nchi/connection/mikopo na elimu ya namna ya kuendeleza biashara zao.
 
Kumachawa ww biashara utaifanya bila mtaji unadhan wote wanaolalamika ajira hawana mawazo ya kufanya biashara kama mtu hana hata hela ya vocha jero na anaish kwao hiyo biashara anaifanyaje au ndo utaleta porojo za kuwa winga au siyo.
Watanzania wengi tunafeli kwa sababu ya mawazo kama haya.
Unamdharau winga wakati akikusanya hela kwa siku ukazidisha mara mwezi ni zaidi ya mshahara wa muhasibu au daktari wa Hamashauri.
Eti utamkuta mtu kazi yake ni kula,kulala,akiamka anakaa kwenye sofa kashika remote ya Tv kwenye sebule ya shemeji yake ukimuuliza wewe unafanya biashara gani?anakujibu sina mtaji,sasa unataka huo mtaji uanguke kutoka mbinguni?
Kama ni kijana wa kiume nenda kajichanganye kwa wahindi upige vibarua umake pesa kwa miezi kadhaa upate mtaji ufanikishe lengo lako na kama ni kijana wa kike nenda katafute vibarua hata kwenye migahawa au saloon umake pesa upate mtaji utimize lengo lako badala ya kupoteza muda kulalamika kila wakati huku umri unaenda muda haurudi nyuma.
Mimi nimeishi na vijana wa kutoka nchi mbalimbali wa kutoka Kenya,Uganda,Sudan,Ghana,Nigeria,Sierraleone,Gambia sasa kila nikiwacheki hawa vijana ujanja wao wa kujiongeza nikilinganisha na kwetu TZ najiona tuko nyuma mno yaani wametuacha mbali.
Wenyewe unakuta kijana ana miaka 19 tayari ameshajiongeza anachekecha haraka haraka mazingira ya nyumbani anagundua hapaliki anapanda anasafiri kwenda ughaibuni anatua kiwanjani kugombania ajira tena hawa ni form 4 tu ila wana confidence hatari ukiingia kichwakichwa kwenye interview na degree yako wanakuaibisha wanachukua ajira.
 
Back
Top Bottom