mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 9,909
- 13,288
Sasa hiyo kuyapatia maisha si ndio hadi uwe na akili za biashara,vinginevyo mkataba ukiisha utarudi kuwa maskini tena.Ata hapa bongo mbona watu wanalipwa millio 15 take home nyumba gari juu ya kampuni. Ni kwambu huku napo inabidi upambane na vitabu sana tuu ili upate hizo kazi.
Sasa take home ya mil 15 kwa bongo hii mkataba say wa miaka 3 sii ulishayapatia maisha
Kuna watu wengi tu nawafahamu wanalipwa mishahara ya milioni 6 hadi 15 kwa miaka zaidi ya 10 na bado mtu hajajipata,wengine hata nyumba ya kulala hawana,wengine kila mwezi wana madeni mtu akipokea mshahara hauvuki wiki 2 kashamaliza kisha anatafuta sehemu ya kukopa hela asogeze siku.
Ishu ya msingi hapa sio ukubwa wa mshahara ila ishu ya msingi ni Financial freedom.
Tajiri hata awe anakulipa milioni 50 usijiamini muda wowote anakugeukia na kingine tena ukishakuwa muajiriwa hajalishi ni wa level gani lazima upelekeshwe huwezi kulala na kuamka muda unaotaka wewe,huwezi kukaa nyumbani na familia yako vile upendavyo wewe kwa kifupi lazima uwe mtumwa