Biashara hii ni kinyume cha sheria?

samito

JF-Expert Member
May 16, 2011
631
176
habari za leo ndugu wana JF.

Mwenzenu nimeanzisha biashara ya kukopesha wafanyakazi mkopo wa chap! chap! yaani kuanzia 100,000 mpaka 500,000 na mdeni ni lazima anilipe ndani ya mwezi mmoja na riba ya 20,000 kwa kila laki moja na akishindwa kulipa basi analeta riba alafu deni linakuwa carried forward pamoja na riba yake.

Kwa kifupi wateja wangu wengi ni walimu na wafanyakazi wa serikali na mashirika mbali mbali wenye kipato cha chini.

sasa sijaisajili hii biashara na sijui kama ni halali kisheria, na je ikitokea siku mtu kanirusha afu nikaenda kumshtaki kwa kutumia hivi vikaratasi tunavyoandikishiana haita nitokea puani??

msaada plzzzzzzzzz.... natanguliza shukran
 
Mkuu irasimishe biashara yako. Vinginevyo utajikuta unapanga foleni mahakamani baada ya kesi ya DECI kwisha!
 
Mkuu irasimishe biashara yako. Vinginevyo utajikuta unapanga foleni mahakamani baada ya kesi ya DECI kwisha!

nashindwa kuirasimisha mkuu coz sijui grounds za kisheria na nahisi faida nayopata ni ndogo sana so hofu yangu ni registration complications kama unafaham njia rahisi ya kurasimisha nitafurah zaid mkuu
 
Biashara kama hizo zipo,ila nivyema zaidi ukairasimisha biashara yako,au kwa muda huu kwa kuwa hazitambuliki kisheria ukawa unawatumia advocates kwenye kuandikisha,ila usikate tamaa coz,kampuni zinazotoa mikopo kwa style km hiyo zilianza kama wewe mf,Mwananchi freedom,Opportunity nk...
 
Wewe kwa lugha ya kifinance unaitwa "Loan Shark" .

Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, tumia mwanasheria katika hiyo biashara yako. Mfano unaweza ukawa na mwanasheria mmoja ambaye mnakubaliana kuwa utamlipa amount flan for initial draft ya mkataba halafu katika kila mkopo unamlipa mfano 5% kwa certification. Hiyo 5% utakuwa unamkata mteja husika. So mtu anayekopa 100,000 ajue atalipia pesa ya mwanasheria 5,000 au kwa maana nyingine atapokea 95,000.

Mwanasheria atakusaidia kudesign mkataba uwe within the limits of the law ili uweze kuwa enforciable kwenye mahakama in case of default. Hiyo biashara kuna mahali ikifika lazima utatakiwa kuiweka rasmi. Watu wengi tunaowaona wameendelea kibiashara walianzia biashara ambazo siyo rasmi.
 
1.wanaotoa vibali vya biashara za pesa ni benki kuu.
2.inategemea unaiandikaje mikataba yako
 
Wewe kwa lugha ya kifinance unaitwa "Loan Shark" .

Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, tumia mwanasheria katika hiyo biashara yako. Mfano unaweza ukawa na mwanasheria mmoja ambaye mnakubaliana kuwa utamlipa amount flan for initial draft ya mkataba halafu katika kila mkopo unamlipa mfano 5% kwa certification. Hiyo 5% utakuwa unamkata mteja husika. So mtu anayekopa 100,000 ajue atalipia pesa ya mwanasheria 5,000 au kwa maana nyingine atapokea 95,000.

Mwanasheria atakusaidia kudesign mkataba uwe within the limits of the law ili uweze kuwa enforciable kwenye mahakama in case of default. Hiyo biashara kuna mahali ikifika lazima utatakiwa kuiweka rasmi. Watu wengi tunaowaona wameendelea kibiashara walianzia biashara ambazo siyo rasmi.

Asante mkuu for this useful post nimeanza mchakato wa kutumia mwanasheria
 
Back
Top Bottom