Sitasahau biashara ya uchimbaji ilivyonifilisi

MC44

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
2,170
3,269
Nipo Geita kiutafutaji kwa miaka 6 sasa. Mwaka 2017 kuliibuka machimbo jirani na ninapoishi.

Kama utakuwa una ABCs za uchimbaji mdogo wa dhahabu, kuna mashimo mafupi (sesa) na marefu (Rongo).

Hayo machimbo yalilenga sesa yaanI ni kuchimba ft 15-20 unakuwa ushapata udongo wenye dhahabu.

Nikaona bora nijitose kwenye uchimbaji huu rahisi. Nikasaka mashimo (wenyewe wanaita maduara) ambayo wameshaanza na wanahitaji mfadhili wa chakula.

Nikapata maduara 3 ambayo nilianza siku hiyo hiyo kuhudumia chakula. Nikiwa na matumaini ya kupata mafanikio baada ya siku 3 za kazi.

Duara linatembea mara naambiwa inahitajika kamba. Nikaona sio mbaya nikanunua za kutosha.

Kazi ikapigwa weee, mara duara limekuwa refu sasa wanahitaji rola ya mti ili iwarahisishie kuvuta mchanga chini. Kidume nikaona poa tuu mzigo si unakuja.

Hapo katikati jamaa wakaomba vitu kama tochi, betri, pesa ya kunoa vitendea kazi, nikaona sio mbaya siku zimekaribia.

Kisanga kilipoanza sasa

Lile eneo lina maji mengi sana maji ya pale mzungu aliyapigia saluti lakini tukamuona hana akili.

Tukumbuke nilishika duara 3. Watendakazi wa duara 2 walikuwa wanajua wanachokifanya wakatoka baada ya kuona hawapati mwamba wa karibu. Hivyo nikabaki na duara 1.

Duara inajaa maji nikatafuta pump ndogo ya kukata maji. Hizi ni pump ndogo zina boya dogo kwa juu ni mahususi kwa visima. Lakini tunalazimisha maduarani.
Zinaendeshwa na jenereta.

Jamaa anakata maji unalipa 20,000 halafu anaingia kwenye uanachama. Akishakata vile yale yanayotoka kidogo kidogo mnakuwa mnachota kwa dumu hadi wakipumzika labda usiku hapo ndo anakuja tena.

Ikafika stage maji hayafai kuchota kwa dumu. Nikatafuta pump ya kukodi halikupatikana basi kidume nikamwambia bibiye tutafute hela tununue pump full set.
Na yeye akishasikia pesa nyingi huwa anachanganyikiwa kabisa.

Hapo nishachoma hela sina hata 100 kibanda nilichokuwa nacho nikafilisi, huduma hakuna, pesa haiingii, ujenzi nikasimamisha nyumba ilikuwa kwenye lenta sikufunga na tofali ni za choma fikiria mvua zikinyesha.

Basi turudi kwa bibiye. Akasema tutafute mahali tukope. Tukazunguka mjini kutafuta wale jamaa wa kukopesha kwa riba.

Jamaa yangu, ngoja nikuache kwanza hapa weka kumbukumbu. Huku nyuma pale duarani kuna mzee yeye ni kamati ya ufundi.

Kila siku ni kwenda kwa waganga kupiga Ramli na kumpa dawa. Kila mganga anapoenda anaambiwa mambo safi utajiri upo dhahabu itapimwa kwa kilo sio gm tena, ikianza kutoa mtakodisha polisi maana kuna viongozi wakubwa wataitafuta hiyo duara na makorokoro mengine mengi.

Nikaona ni vyema japo sijaenda kusikiliza mwenyewe. Vijana wanahamu ya kazi balaa walikuwa 6 wanapungua wakabaki 3 ikabidi tutafute mmoja wawe wanne.

Hapo katikati kila mmoja anatafuta mganga wake na anawaambia mtapata kwenye duara hiyo.

Hata tuendelee kule mjini. Tulipata jamaa mmoja ni mwal akatukopesha mil 1 kwa riba ya %15 kwa mwezi ah nikaona ndani ya wiki tuu hela isharudi mke wangu akasaini ile hela akaacha kadi.

Tukaingia dukani nikaongezea kama laki 5, ikawa mil 1.5 nikanunua
- Pump ndogo.
- Generator ya kingmax 8800
- Cable
- Pipe
- Na vitu vidogo vidogo.

Kule kambini nikabadili utaratibu wa kula nikanunua unga, dagaa wajipikie.

Nikafikisha mzigo duarani kila mmoja ni shangwe nikajiona mwamba. Kumbe viazi tu.

Jenereta inakula mafuta balaa lita 1 inasaga kwa dk 30 imekausha na inatakiwa kurun muda wote mtu akiwa chini.

Kwa bahati nzuri nikapata wengi wa kuwakatia maji kwenye duara zao hivyo muda wa kupumzika kwangu napeleka generator kwa wengine nachukua hizo 20 20 zao sio haba nikitoa mafuta kwa siku nalala na 50 -70.

Hii ikawa inaendesha shughuli za duarani kwangu. Gharama zikawa kubwa lakini zinapozwa na kufanya kazi pengine.

Duara likatembea likahitaji kufungwa matimba, hii ni miti inayofungwa pembeni nayo hii ni gharama kubwa.

Itaendelea.

Mwendelezo

Mara nikaanza kutafuta mdhamini wa matimba, huku na huku hola. Ikabidi nikomae wapige kazi kibishi japo ni riski. Hapo pump ikaanza msala, mara kuungua, mara hitilafu ndogo ndogo tuu, mara jenereta izingue maana ngoma ilipiga kazi zaidi ya uwezo wake.

Pump ndogo ikiungua au iki heat unatoa nyaya zote na unasuka upya, kusuka ni 150. Kama ina shida ndogo labda kebo imekatika ndani lazima fundi ale 20-30. Jenereta ndo nafuu kidogo na kipindi kile ilishaungua mara 2.

Nikaona hawa jamaa wanapanda na chabo (sampuli ya mwamba ) inaonekana vumbi ya dhahabu na shaba kwa wingi. Hapa watendakazi wanakuambia yaan nina v8 yangu hapo chini, hii duara sibanduki.

Nikaona niwe nashuka chini, sio siri nilianza kutumia ponch bila kupenda. Aisee kazi ya chini ni balaa, unatoka hoi hoi.

balaa lingine tena linaanza.
Tumekuta mwamba mgumu hatari hakuna ponchi ya kutoboa. Ikabidi tuanze mlipuko. Hapo kidogo akili zikaanza kujikaza sawa. Huyu jamaa wa kamati ya ufundi ni kuomba tuu nauli aende kwa waganga mara akaja na jibu kwamba kuna mtu wa hivi na hivi ana mkosi inatakiwa aje aoshwe maana huyo ndo ameshika utajiri wenu. Yeye ndo atapata mwamba wa mali katika shift yake na blaa blaa nyingi. Kidume nikaona kumbe issue ndogo tuu nikamwambia aende na gharama zote kwangu..

Kumbuka duara inahitaji miti(matimba), nikapeleka kibabe sasa tumekuta jabali gumu (westi) linahitaji mlipuko na haiwezi kurongwa kabla ya kufungwa miti (matimba). Nikaanza gharama za miti na fundi ikala 300's kwa kuibania maana. Nikaleta compressor ikadrill tundu 3 kwa gharama ya 100's. Tukalipua lkn haikuweza kuvunja mwamba sehemu kubwa.

Hapo na mimi nishaanza kuzunguka kwa waganga, wanasema ukitoa hilo jiwe gumu tu,utaaga umasikini. Ilikuwa changamoto sana kwenda kwa waganga ukizingatia jinsi jamii inavyonichukulia huku, mtu wa kanisani, nakumbuka siku niliwahi kubadili njia na kuzuga kutafuta punda nikiwa natafuta mganga nilijicheka sana.

Mlipuko wa kwanza haukauweza kumaliza lile jabali, ikabidi nirudie tena. Hapa nikatumia drilla wa mkono cha ajabu fataki hazikulipuka,akatega tena mambo yakawa yale yale. Nikarudisha compressor, tunapiga tena 3 lkn jabali bado ipo.

Hapo msosi unatembea kinyama, msosi mkuu ni ugali dagaa. Washenzi wakaota vitambi huku mimi nakonda mbaya sana. Jamaa wa pembeni wananipamba, jamaa komaa hapa umepita mkanda kabisa. Tangu nichukue ile milioni miezi inasonga inalipiwa riba na nikikwama naenda kuongeza, mara 300 mara 200 deni linakuwa tuu.Nakiri wazi hadi mama mkwe nilimkopa.

Enzi hizo nilikuwa na Samsung Galaxy Grand, ikaibwa nimelala juu ya duara. Vita ikaanza home. Nakumbuka siku mama aliniomba ela ya kuvuna kama laki nikamwambia wiki ijayo nitakuwa na ela nyingi we kopa mahali, ikawa kimya. Akanirudia tena naomba 21000 nijaze gesi ndogo nimpikie mzee, nikamzungusha hadi akachukua.

Baba hataki niendelee na uchimbaji. Mke wangu ana mimba miezi 8 na ndani hakuna hela zaidi ya madeni.

Duara zimerefuka hadi ile pump ndogo inashindwa kuvuta maji sawa sawa inahitaji niletee pump nyingine.

Tena ninza kukodi unalipa 600 kwa mwezi....mafuta na ukarabati ni ww

Huku mganga anasema usiache pesa ipo.

Huku wachimbaji wanasema michirizi inaenda kuungana hivyo tuendelee.

Nikampigia mzee m1 ni mganga mzuri ananifahamu vyema ila yupo mbali na anaweza kutabiri kwa simu tuu.

Mzee akasema " duara ina mali nyingi ila sioni zikielekea chini. Inaonekana zipo juu sio kwa urefu huo mliopo.
Ushauri wangu usitumie gharama nyingine ya kuchimba, tafuta mtaalamu wa karibu akusaidie.

Hapo kazi nimeanza mwezi wa nane, hapo ni Disemba mwanzoni mama nawesabia bado wiki 3.

Muda mwingine mke wangu anafanya biashara ndogo ndogo ananipa 20, napeleka duarani.

Muda mwingine nakosa hata nauli ya boda inabidi nitembee kwa saa 1, hatari sana.

Nikarudi nyumbani nikamwambia bibiye tupumzike kwanza hii kazi. Nakumbuka alilia sana.

Maana tegemeo lote ni duara na unavyojua akili za wanawake kwenye pesa nyingi. Nikarudisha vyombo nyumbani kwa roho ngumu nikarudi kijiweni nikajipanga tena

Mtaji mpesa ulikata, hata vocha haikupatikana tena kijiweni nilibaki nachaji tuu simu.

Nikaanza mdogo mdogo tena nikarudisha hadhi ya kijiwe changu.


Naomba niwaambie kitu kimoja
Hii ni biashara yenye pesa nyingi kama utapatia. Kuna jamaa wananunua magari kama ndala, Anajenga kama anajenga banda la mbwa.

Kwa wenye mtaji mdogo ni bora ukaenda kufanya biashara. Peleka chochote utauza kasoro pingu.Chajisha simu ni 500

Tengeneza guest ni 5,000 kwa siku kulingana na wakati. Hizi zinatengenezwa na turubai au mabati au zile nailoni nyeusi. Mwizi akija anakuja na kiwembe anaingia ndani....

Biashara ya baa na malaya inalipa sana pia chakula. Nakiri wazi sijawahi kuchukua malaya wa mgodini maana ni hatari sana. Ukilala gest chumba kimetenganishwa na capet kama kuna malaya humo unasikia kila kitu. Huwezi lala. Ugomvi ndio kwao kule ila wenye roho nzuri ni wengi sana.

Mwanangu alizaliwa salama sasa anatimiza miaka 2. Madeni tulimaliza na ile nyumba ilibidi ninunue tofali 8,000 kama za mwanzo ndo nikaweza kumaliza maana tofali nyingi ziliharibika na sehemu ya ukuta kuanguka. Sasa nimefunika nategemea kufikia June 2020 niwe kwangu.

Naomba niishie hapa kama kuna maswali nitayajibu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom