Baada ya Serikali kushindwa kuongeza mishahara kwa mwaka wa nne sasa,ni bora ikafute kabisa sheria ya mtumishi kubaki na moja ya tatu ya mshahara wake

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,028
144,382
Ukweli ni kwamba, sheria/utaratibu unaotaka mtumishi baada ya makato yote abaki na walau moja ya tatu ya mshahara wake(basic salary),sheria au utaratibu huo imebaki kuwa ni nadharia tu kwani watumishi wengi hivi sasa wanalazimika kukopa katika taasisi binafsi za kifedha na katika SACCOS/VICOBA huku take home yao ikiwa teyari hairuhusu makato zaidi kwa mujibu wa hiyo sheria ya serikali.

Hivyo serikali isijidanganye kuwa hiyo sheria inatekelezwa bali wajue tu ipo kinadharia kwani huwezi kumzuia mtu kukopa wakati unachomlipa hakitoshelezi na zaidi hutaki kukiboresha hivyo ni bora tu wakawaacha watumishi waamue wenyewe ni namna gani watatumia mishahara yao hiyo kiduchu ku-survive.

Kutoongeza mishahara ya watumishi wa umma tangu 2015 na hata kutowapa nyongeza ya kisheria ya kila mwaka,kumefanya watumishi wengi kutokopesheka katika mabenki na hali hii huenda pia inaathiri mabenki na taasisi nyingine zinazofanya biashara ya kukopesha watumishi.

Kwakuwa serikali imeshindwa kuongeza mishahara ya watumishi na ili kumsaidi mtumishi huyu,ni bora ikafutilia mbali hii sheria na pia waje na utaratibu wa makusudi wa kisheria wa kuzipunguzia kodi taasisi za kifedha zitakazoa toa mikopo ya riba nafuu kwa watumishi hasa zile taasisi zitakazoweza kutoza riba ya chini ya asilimi 10(single digit).

Ukiacha mabenki ambayo sijui hukopa kutoka Benki Kuu,siku hizi kuna taasisi nyingi za kifedha(financila institutions) ambazo nazo zinatoa mikopo kwa watumishi ila zinakuwa na riba kubwa hivyo ili kuzishawishi zipunguze riba,ni kuzipa taasisi hizi unafuu wa kodi kwa mashariti ya kuzitaka zipunguze riba katika mikopo wanayotoa kwa wafanyakazi wawe wa serikali hata wale wa sekta binafsi maana katika hizi taasisi watu hukopeshwa bila kuzingatia hiyo sheria ya moja ya tatu na kuna mikopo ya kuanzia mwezi mmoja mpaka miezi 6 na ndio maana nasema hii sheria ya moja ya tatu kiuhalisia ni kama ipo kinadharia tu kwani inadhibiti zaidi ukopeshaji kupitia mabenki na si katika baadhi ya hizi taasisi nyingine.

Au kama kuna hofu kuwa hiyo sheria ya moja ya tatu ikifutwa baadhi ya watumishi watakuwa na mishahara zero mwisho wa mwezi,basi serikali inaweza kuja na utartibu wa kutenga fedha na kutoa mikopo isiyo na riba kwa watumishi wake au yenye riba ndogo ingawa uamuzi huu unaweza kuathiri sekta binafsi lakini ninahakika utaleta ushindani na hata kupelekea taasisi binafsi nazo kushusha riba na kupunguza mashariti ya utoaji wa mikopo ambayo nayo ni changamoto kwa watumishi.

Alafu jambo lingine linalonifanya nisione tena umuhimu wa hii sheria ni uamuzi wa serikali inayojidai kulinda mshahara wa mtumishi kuongeza makato kwa ajili ya Bodi ya Mikopo kutoa asilimia nane mpaka asilimia 15 huku kukiwa na madai(sijui ukweli wake) kuwa makato haya ya Bodi ya Mikopo hayazingatii sheria ya moja ya tatu bali wanakata tu mradi wachukue chao.

I wish I could be Raisi wa TUCTA!!
 
Mkopo wa mtumishi wa umma una risk ndogo lakini bado unakuwa treated sawa na wakopaji wengine. Kwanza hauna gharama za ufuatiliaji kubwa sana nadhani wangepewa kwa riba ndogo pia. Au badala yake serikali itenge kila wilaya hela ya kukopesha watumishi wake na wanawakata direct kwenye salary zao. Hii ingepunguza watumishi kuhangaika na maisha na kukosa furaha ya kuwa na kazi.
 
Tatzo la ngozi nyeusi mtu akishashiba hamkumbuki mwenye njaa
 
Nyie watumishi vipi? Kwano mlilazimishwa kuajiliwa? Kama mshahara autoshi acha kazi vinginevyo funga madomo yengu kapambane na hali zenu
 
kuna wengine ni waajabu kweli, eti anauliza watumishi kwanini mliajiriwa, haki ni haki tu, yamkini hata wewe unaeuliza ni zao la hao watumishi unao wadharau
 
Mkopo wa mtumishi wa umma una risk ndogo lakini bado unakuwa treated sawa na wakopaji wengine. Kwanza hauna gharama za ufuatiliaji kubwa sana nadhani wangepewa kwa riba ndogo pia. Au badala yake serikali itenge kila wilaya hela ya kukopesha watumishi wake na wanawakata direct kwenye salary zao. Hii ingepunguza watumishi kuhangaika na maisha na kukosa furaha ya kuwa na kazi.
Lengo ni mikopo kuelezwa maeneo ya uzalishaji sio maprado yasiyozalisha au nyumba ya million 200 wakati mtu ana mtoto mmoja tu na alternatively ingeweza kuleta nyumba ya 50 millions na 150 millions kiwanda cha kati
 
Back
Top Bottom