DOKEZO BIASHARA HARAMU YA BINADAMU: Umeshawahi kujiuliza wauza karanga na kahawa za kutembeza wanatokea wapi hapa Dar?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Imezoeleka watu kufahamu biashara haramu ya binadamu kama biashara inayofanyika kwa kuvuka mipaka, yaani kati ya nchi moja kwenda nchi nyingine, lakini ukweli ni kwamba biashara haramu ya binadamu imeshamiri sana hata ndani ya mipaka ya nchi.

Vijana hawa wengi unaowaona wanatembea barabarani wakiuza karanga na kahawa barabarani ni michongo ya watu hapa mjini kwenye biashara hii haramu ya binadamu. Vijana hawa mara nyingi wanakuwa wanatolewa mikoani hasa mikoa ya mbali kama Kigoma kwa ahadi kuwa akifika Dar atapatiwa kazi. Kwakuwa mtu maisha yakuwa yamemchapa anaona bora akajaribu bahati yake, kumbe ndiyo 'ameshanunuliwa' hivyo!

Akifika Dar anatafutiwa sehemu ya kulala, mara nyingi ni sehemu chafuchafu kama kwenye nyumba zilizotelekezwa, ama kinapangishwa chumba kimoja na wote wanarundikwa humo (maeneo ya Magomeni yanasemekana kutumika sana kwa mambo haya).

Kwahivyo unakuwa umepewa sehemu ya kulala na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na mtaji wa kuanzia, kwa ahadi ya kuwa ukishalipa deni utaweza kuondoka na kuendelea kujisimamia mwenyewe, hapo ndiyo mwisho wako, huchomoki tena.

Kila jioni wanapeleka hesabu kwa bosi wao ambaye atachukua kiasi chote na kumpa hela ndogo tu ya kumfanya kesho yake aweze tena kuzunguka vizuri na mnyororo huo unaendelea hivyo hivyo. Ukisema kwamba unataka kujitoa ama unataka kurudi kwenu, utaambiwa hujamaliza deni lako kwahiyo unatakiwa kuendelea kufanya kazi, na ukisema ujiondoe kilazima basi hupewi hata senti moja. Kwakuwa umetoka mkoani na huna pakufikia unamua kubaki kuendelea kuwa mtumwa.

Jambo hili pia linafanyika hata kwa mabinti, lakini kwa mabinti inakuwa ni kwenye biashara ya ukahaba au wadada wa kazi za majumbani. Binti anatolewa mkoani kwa ahadi ya kupatiwa kazi, wengine kwakuwa wanafahamika na wazazi wa binti inakuwa rahisi kuaminiwa na wazazi wa binti, wakifika Dar kibao kinageuka (maeneo ya Kinondoni yasemekana kuwa maarufu kwa magenge haya).

Mabinti hawa huingizwa kwenye mitandao ya kuuzwa, ambapo wao wanauzwa kama nyanya, ukitaka 'bidhaa' unatumiwa picha, unachagua picha ya binti unayetaka na binti anatumwa, chochote utakachomfanya ni juu yako.

Mabinti wengine hupelekwa kufanya kazi za ndani ambapo baadhi hupewa na mbinu kabisa za kufanya wasikae muda mrefu kwa waajiri wao. Kabla ya kwenda sehemu ya kazi anaambiwa utakaa kwa mfano miezi mitatu au mitano na baada ya hapo aanze kufanya vitimbi hadi bosi wake amtimue.

Akishatimuliwa anapelekwa kwa mtu mwingine ambaye anahitaji dada wa kazi na mnyororo unaendelea. Magenge haya yapo sana maeneo ya Kinondoni, na kibaya zaidi ni kwamba hata mabinti chini ya miaka 18 ni waathirika kwenye janga hili.

Binti akitaka kurudishwa kwao mwendo huwa ni ule ule, unaambiwa umetolewa mkoani na unatuzwa kwa gharama kubwa (matunzo ambayo ukiyaona utasema bora hata kuwa mnyama kuliko kuishi hivyo), hivyo ni lazima ulipe deni ili uweze kurudishwa kwenu, deni ambalo halitakaa liishe milele na wewe kuendelea kuwa mtumwa, labda mpaka muujiza utokee ukapata msamaria mwema wa kukukomboa.

Kinachosikitisha zaidi na kutia hasira pia ni kwamba, kwa baadhi ya maeneo ma 'Madam' na 'Mabosi' wanaomiliki biashara hizi wanajulikana kabisa kuwa wao wanahusika na biashara hizi haramu, swali ni kwamba kwanini hawachukuliwi hatua? Ama kuna watu wachache wanafaidika na uwepo wa magenge haya?

Wakuu usimuamini kumpa mtu kijana/binti wako kuwa nakusaidia kumsomesha au kumpatia kazi sehemu fulani bila kujiridhisha kabisa kwamba mtoto wako anaenda kuwa salama huko aendako. Siyo kwamba kila mtu anyekuja kukupa msaada ana nia ovu lakini ni vizuri kuchukua tahadhari.

Dunia imebadilika sana, na maovu yameongezeka, tujitahidi kuwa walinzi wa kila mmoja wetu, leo unaweza kupuuza kwakuwa siyo mtoto wako au ndugu yako kesho yakakufika wewe ukasaga meno, na mamlaka kwa nafasi yake uchukue hatua na kushughulika na jambo hili, kwasababu hali inatisha.
 
UJUMBE MUHIMU SANA. BAHATI MBAYA JF WATU HAWASOMI VITU KAMA HIVI....
 
Imezoeleka watu kufahamu biashara haramu ya binadamu kama biashara inayofanyika kwa kuvuka mipaka, yaani kati ya nchi moja kwenda nchi nyingine, lakini ukweli ni kwamba biashara haramu ya binadamu imeshamiri sana hata ndani ya mipaka ya nch...
Sawa ndugu tufanyeje sasa ? Je unaweza kusaidia kutoa ushirikiano wa sehemu wanapohifadhiwa hawa vijana? Je, unaweza kutoa ushirikiano tukihitaji hayo majina ya hao vijana?

Tanzanians tujipende na tupambane embu tuamke tuwatetee wenzetu wanahangaika na ujinga wa hivi.
 
Kwa kweli kwa namna ulivyoeleza ninaamini umefanya utafiti hata kama sio utafiti rasmi, hongera kwa kuibua hoja.

Mamlaka zinatakiwa kufanyia kazi kila kitu mpaka tetesi (sio lazima iwe malalamiko rasmi) kama za mambo haya, wasilete zile majibu zao za hatuwezi kufanyia kazi mambo ya mitandaoni, mmepewa taarifa, fanyieni kazi, chunguzeni - hela za kuendesha ofisi ni zetu watanzania, msitoe visingizio kutofanyia kazi maana hata bila ya mambo kama haya huwa mnazimaliza tu hizo fedha. Fanyeni kazi majanga kama haya tuyazuie mapema
 
Hii jamuhuri vihoja na visa haviishi Kila siku, unaweza Kuta mtu akitaka kupambana na huo upumbavu ana zibwa mdomo
 
Sawa ndugu tufanyeje sasa ? Je unaweza kusaidia kutoa ushirikiano wa sehemu wanapohifadhiwa hawa vijana ? Je unaweza kutoa ushirikiano tukihitaji hayo majina ya hao vijana...
Hizi habari zinafahamika na watu wengi,siyo lazima mtoa mada atoe ushahidi kama kweli vyombo vya dola vinataka kuchukua hatua.

Wauza mayai wengi ni kutoka Kigoma, na mtandao wao uko Magomeni na Kariakoo. Wauza karanga wengi ni kutoka Lushoto na mtandao wao uko Tabata. Usipate shida ukikutana nao hata watatu ukiwauliza watakueleza wanatoka wapi.

Sema hawa ma don wa hizibiashara za mayai na karanga wanatumia nguvu za giza ambazo zinawazuia hawa vijana wasikate minyororo
 
Imezoeleka watu kufahamu biashara haramu ya binadamu kama biashara inayofanyika kwa kuvuka mipaka, yaani kati ya nchi moja kwenda nchi nyingine, lakini ukweli ni kwamba biashara haramu ya binadamu imeshamiri sana hata ndani ya mipaka ya nchi.

Vijana hawa wengi unaowaona wanatembea barabarani wakiuza karanga na kahawa barabarani ni michongo ya watu hapa mjini kwenye biashara hii haramu ya binadamu. Vijana hawa mara nyingi wanakuwa wanatolewa mikoani hasa mikoa ya mbali kama Kigoma kwa ahadi kuwa akifika Dar atapatiwa kazi. Kwakuwa mtu maisha yakuwa yamemchapa anaona bora akajaribu bahati yake, kumbe ndiyo 'ameshanunuliwa' hivyo!

Akifika Dar anatafutiwa sehemu ya kulala, mara nyingi ni sehemu chafuchafu kama kwenye nyumba zilizotelekezwa, ama kinapangishwa chumba kimoja na wote wanarundikwa humo (maeneo ya Magomeni yanasemekana kutumika sana kwa mambo haya).

Kwahivyo unakuwa umepewa sehemu ya kulala na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na mtaji wa kuanzia, kwa ahadi ya kuwa ukishalipa deni utaweza kuondoka na kuendelea kujisimamia mwenyewe, hapo ndiyo mwisho wako, huchomoki tena.

Kila jioni wanapeleka hesabu kwa bosi wao ambaye atachukua kiasi chote na kumpa hela ndogo tu ya kumfanya kesho yake aweze tena kuzunguka vizuri na mnyororo huo unaendelea hivyo hivyo. Ukisema kwamba unataka kujitoa ama unataka kurudi kwenu, utaambiwa hujamaliza deni lako kwahiyo unatakiwa kuendelea kufanya kazi, na ukisema ujiondoe kilazima basi hupewi hata senti moja. Kwakuwa umetoka mkoani na huna pakufikia unamua kubaki kuendelea kuwa mtumwa.

Jambo hili pia linafanyika hata kwa mabinti, lakini kwa mabinti inakuwa ni kwenye biashara ya ukahaba au wadada wa kazi za majumbani. Binti anatolewa mkoani kwa ahadi ya kupatiwa kazi, wengine kwakuwa wanafahamika na wazazi wa binti inakuwa rahisi kuaminiwa na wazazi wa binti, wakifika Dar kibao kinageuka (maeneo ya Kinondoni yasemekana kuwa maarufu kwa magenge haya).

Mabinti hawa huingizwa kwenye mitandao ya kuuzwa, ambapo wao wanauzwa kama nyanya, ukitaka 'bidhaa' unatumiwa picha, unachagua picha ya binti unayetaka na binti anatumwa, chochote utakachomfanya ni juu yako.

Mabinti wengine hupelekwa kufanya kazi za ndani ambapo baadhi hupewa na mbinu kabisa za kufanya wasikae muda mrefu kwa waajiri wao. Kabla ya kwenda sehemu ya kazi anaambiwa utakaa kwa mfano miezi mitatu au mitano na baada ya hapo aanze kufanya vitimbi hadi bosi wake amtimue.

Akishatimuliwa anapelekwa kwa mtu mwingine ambaye anahitaji dada wa kazi na mnyororo unaendelea. Magenge haya yapo sana maeneo ya Kinondoni, na kibaya zaidi ni kwamba hata mabinti chini ya miaka 18 ni waathirika kwenye janga hili.

Binti akitaka kurudishwa kwao mwendo huwa ni ule ule, unaambiwa umetolewa mkoani na unatuzwa kwa gharama kubwa (matunzo ambayo ukiyaona utasema bora hata kuwa mnyama kuliko kuishi hivyo), hivyo ni lazima ulipe deni ili uweze kurudishwa kwenu, deni ambalo halitakaa liishe milele na wewe kuendelea kuwa mtumwa, labda mpaka muujiza utokee ukapata msamaria mwema wa kukukomboa.

Kinachosikitisha zaidi na kutia hasira pia ni kwamba, kwa baadhi ya maeneo ma 'Madam' na 'Mabosi' wanaomiliki biashara hizi wanajulikana kabisa kuwa wao wanahusika na biashara hizi haramu, swali ni kwamba kwanini hawachukuliwi hatua? Ama kuna watu wachache wanafaidika na uwepo wa magenge haya?

Wakuu usimuamini kumpa mtu kijana/binti wako kuwa nakusaidia kumsomesha au kumpatia kazi sehemu fulani bila kujiridhisha kabisa kwamba mtoto wako anaenda kuwa salama huko aendako. Siyo kwamba kila mtu anyekuja kukupa msaada ana nia ovu lakini ni vizuri kuchukua tahadhari.

Dunia imebadilika sana, na maovu yameongezeka, tujitahidi kuwa walinzi wa kila mmoja wetu, leo unaweza kupuuza kwakuwa siyo mtoto wako au ndugu yako kesho yakakufika wewe ukasaga meno, na mamlaka kwa nafasi yake uchukue hatua na kushughulika na jambo hili, kwasababu hali inatisha.
Duh..
Utumwa wa kusasa huu
 
Hii ni kweli kabisa.
 
Wauza karanga hao wameshindwa kutoroka? Yani siku azunguke na asirudi?

Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom