Biashara bwana!

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
4,124
11,901
Mara nyingi huwa napita pale Feri , ni saa moja asubuhi lakini kuna jamaa wanauza juisi baridi ya miwa.

Watu wamejazana sana mara zote utadhani ni mchana wa saa saba! Nilidhani ile biashara inauzika mchana, ila pale kuanzia saa moja kasoro asubuhi jamaa wameshajaza watu.
 
Watu wamelewa jana yake usiku
Wameamka na pombe
Ni lazima apate kinywaji baridi asubuhi.

Kwanza huko Dar si nasikia uwa hamlali?
Huku kwetu mkoa ikifika tu saa 2 uck hiace zinaanza kupotea.
Dar pesa inatafitwa haswa magari yanapungua saa 7 hadi 9 tu baada hapo yanaanza tena jamaa yangu ana Eicher anaamka saa 9....mbagala kkoo ....kkoo gmboto ikifika saa 3 analaza gari amepata hesabu na posho....saa 4 anafungua duka lake hardware ......imetoka hiyo .....mwaka 4 sasa naona anaenda vzr sana anaongeza chumba sebule kupangisha tuuuuu
 
Mara nyingi huwa napita pale Feri , ni saa moja asubuhi lakini kuna jamaa wanauza juisi baridi ya miwa.

Watu wamejazana sana mara zote utadhani ni mchana wa saa saba! Nilidhani ile biashara inauzika mchana, ila pale kuanzia saa moja kasoro asubuhi jamaa wameshajaza watu.

biashara ni code ukizipatia umepatia.
kuna dogo alikuja mkoani hapa kujaribu maisha mpaka kukata tamaa.
ila alipokwenda Dar aliona kitu kimoja swala la jinsi ya kupika chips kama za dar tena zile za kkoo na kinondoni basi kaja kuleta ilo jambo.
unaambiwa anamaliza guni 9 kwa siku treyi za mayai 120 ndani ya siku tatu.
mji mzima kakamata yeye sasa anajenga na kausafiri IST new model.

Biashara zipo nyingi ila ndio una akili ya kuchambua biashara.
baishara sio kujaribu ni kujitosa
 
Ukikosea tobo lako la kutokea utapata tabu sana,hapo hao jamaa wa juice ukienda wewe kuuza juice Yako inaweza ikadoda,
 
Mara nyingi huwa napita pale Feri , ni saa moja asubuhi lakini kuna jamaa wanauza juisi baridi ya miwa.

Watu wamejazana sana mara zote utadhani ni mchana wa saa saba! Nilidhani ile biashara inauzika mchana, ila pale kuanzia saa moja kasoro asubuhi jamaa wameshajaza watu.
Ni dawa nzuri ya hangover.Pia ni nzuri kwa afya.Darisalama joootooo...!
 
Ni kweli mkuu lakini siyo kawaida Juisi ya miwa kuuzwa asubuhi ya saa moja kasoro na bado ukute watu wamejaa.
Ni kawaida tena ni sahihi.Tunatofautiana muda wa kuingia na kutoka mihangaikoni.Ukiwaambia waanze kuuza juisi yao saa tatu asubuhi watatukosa sisi walinzi wa SHING LONG SECURITY CO.LTD.Waacheni nasi tupate huduma ya kutoa hangovers za mnazi.
 
Dar pesa inatafitwa haswa magari yanapungua saa 7 hadi 9 tu baada hapo yanaanza tena jamaa yangu ana Eicher anaamka saa 9....mbagala kkoo ....kkoo gmboto ikifika saa 3 analaza gari amepata hesabu na posho....saa 4 anafungua duka lake hardware ......imetoka hiyo .....mwaka 4 sasa naona anaenda vzr sana anaongeza chumba sebule kupangisha tuuuuu
Mkuu umesema anaamka saa 9 usiku Hadi saa 3 asubuhi ashapata hesabu na posho? Au sijaelewa naomba ufafanuzi hapo.
 
Dar biashara ipo masaa 24, niliona fursa ya kuuza bites usiku. Napika kuanzia saa 11 jioni bites zote, hapo maziwa ya kutosha, chai ya rangi na juice ya matunda.

Nakesha nauza mpaka asubuhi saa 4 nafunga hesabu naenda kulala mpaka jioni tena.
Jamani Dar watu wanakula hata saa 8, 9 au 10. Hapo usiku utawapata bodaboda wakeshaji.

Ikifika saa 12 asubuhi wameshaanza kupata kifungua kinywa, wengine wanabeba za kwenda nazo maofisini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu nilikaa stendi wakati wa usiku watu hawaishi kabisa aise, yaani wanapungua kidogo tu ile mida ya saa nane, saa tisa pale wanaanza kujaa tena.
 
Back
Top Bottom