Bi. Titi Awafichua Waalim Wake wa Siasa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
BI. TITI MOHAMED AWAFICHUA WALIOKUWA WAKIMUONGOZA KATIKA HOTUBA ZAKE ZA KUHAMASISHA WANANCHI

Makala hiyo hapo chini nimeandika baada ya kusona video fupi ya mahojiano ya Bi. Titi.

Haya yaliyomo katika mahojiano haya ya Bi. Titi Mohamed kwangu mimi ni mageni mno kwani sikupata kuyasikia popote pale.

Sikupata kuyasikia popote katika utafiti wangu wa muda mrefu wa historia ya TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Bi. Titi Mohamed amemvika taji Clement Mtamila kuwa ndiye aliyekuwa akimuongoza katika kumfunza vitu gani aseme katika hotuba zake anapokuwa jukwaani kuzungumza na wananchi.

Bi. Titi pamoja na Clement Mtamila kamtaja Oscar Kambona, John Rupia, Dossa Aziz na karani wa TANU jina lake John Msumba kuwa hawa ndiyo waliomuongoza katika hotuba zake.

Bi. Titi kasema kuwa Julius Nyerere hakuwa mwalimu wake.

Walimu wake ni hao aliowataja.

Si wengi wanafahamu kuwa Bi. Titi alihutubia mikutano miwili ya TANU Viwanja vya Mnazi Mmoja hajakutana na Julius Nyerere.

Hii ndiyo historia ya TANU ambayo kwa miaka mingi zaidi ya nusu karne toka Tanganyika ijitawale historia hii haikufahamika.

Historia ya TANU ilikuwa siku zote inaanza na Julius Nyerere.

Haitoki nje ya hapo.
Bahati mbaya Nyerere aliridhia na hali hii.

Clement Mtamila alikuwako katika harakati za uhuru kama kiongozi kutoka enzi za TAA kama Secretary na yeye ndiye aliwakabidhi uongozi ingawa kwa mapinduzi kwanza kisha kufanyika uchaguzi Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes kuongoza TAA mwaka wa 1950.

Huu ulitambulika kama uongozi wa vijana wastani wa umri wao haukupindukia zaidi ya miaka 25 katikati hapo.

Ilipoasisiwa TANU mwaka wa 1954 Mzee Mtamila akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TANU kwa kuwa katiba ya TANU ya miaka ile ilikuwa na nafasi hiyo.

Si wengi wanamfahamu kuwa kikao cha kujadili barua ya Mwalimu Nyerere kuacha kazi ya ualimu ilijadiliwa kwenye kikao cha TANU nyumbani kwa Mwenyekiti Mzee Mtamila Mtaa wa Kipata (sasa Kleist Sykes) na Sikukuu.

Hawa ambao Bi. Titi amewataja ndiyo waalimu wake waliomwanzisha alifu kwa kijiti katika siasa na hawa ndiyo walikuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU ukimuongeza na Bi. Tatu bint Mzee.

1677321977186.jpeg

Kulia: Clement Mtamila, Julius Nyerere, Maria Nyerere na Zuberi Mtemvu

246712212_1046270366120341_8080825610121839410_n.jpg

Bi. Titi Mohamed na Julius Nyerere Viwanja vya Jangwani mikutano ya mwanzo ya TANU

1677322547573.png

Bi. Titi Mohamed na Dossa Aziz​
 
Back
Top Bottom