Uchaguzi 2020 Bi Queen Cuthbert Sendiga Mgombea urais wa Tanzania kupitia ADC, azindua Kampeni Zanzibar, Wavuvi na Wakulima wa Karafuu kuneemeka

ADC Party

Member
Sep 14, 2020
28
29
1600341477154.png

Mgombea wa RAIS Jamhuri ya Muungano WA Tanzania Bi Queen Cuthbert Sendiga aliwaambia wananchi wa PEMBA endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atahakikisha wananchi wa PEMBA watanufaika na zao la karafuu kwa kulipandisha thamani ili liweze kuingiza fedha za kigeni na kuwafanya wananchi hao kuwa na maisha bora na kufurahia kuwepo kwa zao hilo

Aidha mgombea huyo amewaahidi wanachi kuwa atahakikisha wanapatiwa Viwanda vya kusindika samaki ili kuweza kupata ajira za kutosha katika visiwa hivyo, na kuwaondoa wananchi wa Pemba katika lindi la umasikini, hasa wananchi wa Micheweni ambao kwa takwimu za kitaifa inaonesha Wilaya hii ni masikini ya kutupwa hivyo ADC itafanya jitihada Za makusudi kuhakikisha wananchi hao wanindokana na umasikini,

Katika kuhakikisha wananchi wanapata Afya ya kutosha hasa kuepusha vifo vya Mama na mtoto ADC itawekeza katika secta ya Afya kwa upande wa Zanzibar ili kuhakikisha wananchi hao wanaondoka na kuzorota kwa afya zao,

Zaidi amewaasa wanamicheweni na watanzania wote kujihadhari na wanasiasa wanaoleta sera za uvunjifu wa amani,Queen amesema wanasiasa hao waogopwe Kama Corona na amesisitiza kulinda amani ni jukumu la kila mtanzania.

Mgombea huyo anaendelea na kampeni zake kesho katika mkoa wa TANGA
Wilaya ya TANGA, Korogwe, Handeni pamoja na Kilindi
Zanzibar 2020 - Alliance for Democratic Change (ADC) kuzindua Kampeni Kisiwani Pemba kesho Septemba 16, 2020

 
Hivi kumbe kuna wagombea zaidi ya wale watatu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo 16 aisee, wakiongozwa na Lissu wanapitapita kujitambulisha.
Halafu takukuru hawajielewi, Sasa kumzuia mzee Rungwe asibebe ma hot pot naona wamempa sababu tuu , wangemkomalia lazima abebe wali kuku kama alivyoahidi angesema analazimishwa kubeba wali na asingeweza. Sasa kapata la kusema.
 
Wapo 16 aisee, wakiongozwa na Lissu wanapitapita kujitambulisha.
Halafu takukuru hawajielewi, Sasa kumzuia mzee Rungwe asibebe ma hot pot naona wamempa sababu tuu , wangemkomalia lazima abebe wali kuku kama alivyoahidi angesema analazimishwa kubeba wali na asingeweza. Sasa kapata la kusema.
Hahahaha yule angeishia njiani tuu,naona kapumua huko aliko.
 
Back
Top Bottom