Hao wapo Dar mkuu, nenda mavuno house Posta na Sinza kijiweni,
Ni wapigaji tu,
Wapo wengine wakiume wanatembea kuuza kwenye makampuni TENDA fake, mfano walikuja ofisini kwangu wakasema wanatoka Orthodox Church wanatenda huko mpanda na Mbeya za Kufunga Sola!
Mmoja kajitune kama padre John! Lakini wakanikuta mtoto wa mjini mwenzao nikawaambia tuonane baadae Steers,
Baada ya kufika Steers nikawakopa zile tenda na nikazijaza kisha nikawarudishia, kesho yake wananipigia simu kuwa nimeshinda tenda, nilicheka sana nikawauliza mmefika lini mpanda wakasema tulitumia ndege,
Kwakuwa nayajua maendeo maarufu ya wapigaji nikaenda Mavuno house nikawakuta na nikawapa salamu huku wakiwa wametoa mimacho tu!
Wanaofisi na mitandao ya internet ya kupigia masaa yote na mabinti wapo!
Hiyo ndio bongo pole sana!