Beware na huyu Jack Shoo wa Facebook na mitandao mingine

mimi katoka kunitumia Ujumbe huu sasa hivi Jack Bana
535852_357666904282819_100001185365487_902206_807384955_n.jpg

duh jf ni noma,never bored,badilisha angalau kava ya hiyo cm ni buku unusu tu mkuu.
 
Du, Interne.... mpaka wabongo waje waijulie itakuwa imewaliza wengi. Wewe utampaje mtu ambaye humjui na umeona picha yake tu kwenye fesibuku namba zako za simu? Kwa taarifa yako kwenye fesibuku kuna midume kibao inayojitambulisha kama midemu na imeweka picha za mademu wakali sana, wakisubiri mazoba wawapige.
 
na huyu Hapa ndio Jack Mwenyewe

521808_107886092677955_100003696946164_41011_1656291822_n.jpg

Nyie vidume legelege,yaani banati mashallahu kama mnaona khiyana kumwachia japo kijimilioni acheze? hebu mwambieni aje pande za zenji nimkabidhi visent vyangu halua ,tende na karafuu.
 
Msimshitue jaman waungwana na mim nikamtengeneze huko huko kwenye facebook nataka nikajirengeshe anipe namba yake ya simu au namba ya akaunt yake akinipa tu ajue kaumie namkombea vijisent vyake vyoote.

Mjini shule.
 
Hao wapo Dar mkuu, nenda mavuno house Posta na Sinza kijiweni,

Ni wapigaji tu,

Wapo wengine wakiume wanatembea kuuza kwenye makampuni TENDA fake, mfano walikuja ofisini kwangu wakasema wanatoka Orthodox Church wanatenda huko mpanda na Mbeya za Kufunga Sola!

Mmoja kajitune kama padre John! Lakini wakanikuta mtoto wa mjini mwenzao nikawaambia tuonane baadae Steers,

Baada ya kufika Steers nikawakopa zile tenda na nikazijaza kisha nikawarudishia, kesho yake wananipigia simu kuwa nimeshinda tenda, nilicheka sana nikawauliza mmefika lini mpanda wakasema tulitumia ndege,

Kwakuwa nayajua maendeo maarufu ya wapigaji nikaenda Mavuno house nikawakuta na nikawapa salamu huku wakiwa wametoa mimacho tu!

Wanaofisi na mitandao ya internet ya kupigia masaa yote na mabinti wapo!

Hiyo ndio bongo pole sana!
 
Wapo wengi hao kaka facebok yupo mwingne naijiita zulekha mohammed huyu ni mzanzibar jina lake harisi dume kabisa jina halisi linaitwa Ally Mohammed Hajji kuweni makini na fwecebook kabisaaa
 
Back
Top Bottom