Betting imeniliza jamanišŸ™Œ

Betting imeniliza jamanišŸ™Œ

Yofav

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
4,309
Reaction score
7,856
Ni kamchezo fulani ambako usipokuwa na displine anguko lako lipo karibu, Sikuelewa wakati nilipomuona mtu anaedai kupoteza kila kitu kwenye kamari, Nilimuona mjinga nikijiuliza "Amepotezaje???"

Kamchezo ambako usipokuwa makini unaweza kujikuta unadundulizia humo kila senti yako unayoona ni ndogo kwa matumaini ya ipo siku utapata nyingi.

Akili inakufanya uhisi kama unachanga fedha kumbe umechanganyikiwa, Na kama huamini pitia bet history ulinganishe hela uliyopoteza na uliyopata ipi nyingi???

Wapo ambao ni njia yao ya kutobolea sikatai ila amini kwamba kama sio njia yako mkuu kuna siku utaongea mwenyewe.

Nilikuwa na utaratibu wa kujifanya na-bet kiasi kidogo ambacho hata nikipoteza siumii, Imeenda kwa zile chache zilizonipa ushindi nilipata relief na kuhisi mimi pia namkanda muhindi, Nikafika muda naweza ku-stake high na bado nikashinda na ikanipa confidance kiasi nikaanza kuwa hata zile high stake siogopi kupoteza.

To be honest zipo nilizoshinda lakini nimepoteza zaidi, Nimekuja kuangukia pua zaidi mwanzoni mwa week iliyoisha, Ghafla bin vuu kila mkeka wangu unachana, Nimechana mfululizo kiasi nikibiga hesabu akili inaniambia nistake high zaidi ili nirudishe hela yangu lakini bado nimepasuka vibaya mno... Katika hali isiyo ya kawaida imenichukua week tu kupuputishwa 3/4 ya akiba yangu.

Kila nikijaribu kurudi duniani ni kama nazidi kuongeza amount of loss... Na hapa naandika nimetoka kulost hela ambayo ilikuwa ya bill ya moja ya service ya nyumbani... What a loss man!!!!? Nimekuwa mjinga sana kuamini kuwa bet inaweza kudouble hela wakati mwanzo nilikuwa nabet nikiweka 90% za kupoteza eti leo naweka 90% za ku-win what a shame!!?

Naacha hii kitu hadi baada ya world cup kuisha nitarudi tena nikiwa na nguvu mpya inshaallah, Muhimu sijapoteza vyote kabisa acha nikubali kwamba kanji kashinda kwa sasa... Me ni muelewa.
 
Naacha hii kitu hadi baada ya world cup kuisha nitarudi tena nikiwa na nguvu mpya inshaallah, Muhimu sijapoteza vyote kabisa acha nikubali kwamba kanji kashinda kwa sasa... Me ni muelewa.
Machale
Unatakiwa uwe na Machale
Unakua unagundua kabla hujala na kabla hujaliwa
Wewe siku hizi huna Machale ndio maana unaanza kuliwa yaan wanakuua kila ukiweka unakufa ukiweka unakufa sababu huna Machale

Sixth Sense
 
Machale
Unatakiwa uwe na Machale
Unakua unagundua kabla hujala na kabla hujaliwa
Wewe siku hizi huna Machale ndio maana unaanza kuliwa yaan wanakuua kila ukiweka unakufa ukiweka unakufa sababu huna Machale

Sixth Sense
Ndo imekaaje hiyo
 
Wazee wa matreni.... Beting sio mbaya ila wewe ndio tatizo
 
Mkuu shukuru Mungu bado Marinda unayo,siku utapofilisikaa vizuri utakuwa tayari kuweka Marinda rehani ili tubupate mtaji wa kueka mkeka..
 
Wazee wa over,under,2up, GG, DC 😁 huu mchezo kwa macho ya nyama ukiuona unaona ni rahisi sana ila Kwa fikra pevu ni mchezo mgumu sana kuliko unavyodhani.KIUFUPI TU HAKUNA BETTING RAHISI,chance ya kupigwa ni kubwa kuliko kula
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom