Barrick Gold Tanzania, na Geita (migodini). kule ukienda, Human recource anaweza kuwa analipwa hata milioni tatu hadi tano kwa mwezi. mlinzi wa mgodini wanalipwa laki tisa hadi milioni moja na nusu. mwanasheria wa kampuni analipwa kuanzia milioni tano kwenda juu kwa mwezi. mfano Tulawaka, hiyo ni net, halafu chakula bure mnapikiwa cha first class (western) unakula tani yako, hivyo huo mshahara hautanunua chakula etc. ndio maana wanamalizia kwenye uzinzi tu wakienda likizo. unafanya kazi wiki tatu, wiki mbili likizo. hao ndo wazungu bwana. pamoja na kwamba wanatuibia sana, lakini watz wenzetu wanaofanya kazi huko ndo wanalipwa hivyo.