Bernard Membe kutoka CCM kunanikumbusha siku Prof. Malima alipotoka CCM 1995

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
BENARD MEMBE KUTOKA CCM KUNANIKUMBUSHA SIKU PROF. MALIMA ALIPOTOKA CCM 1995

Ilikuwa siku ya Ijumaa tarehe 15 Julai 1995, magazeti ya siku hiyo ‘’Majira,’’ ‘’Nipashe,’’ pamoja na gazeti la CCM ‘’Uhuru,’’ na Shirika la Habari la Tanzania (SHIHATA) walikuja na habari kubwa katika wino mweusi uliokoza kwenye kurasa za mbele kuwa Prof. Malima atajitoa CCM akiwa kasimama kwenye membari ya msikiti wa Gongoni Tabora baada ya sala ya Ijumaa.

Mji Dar es Salaam ulikuwa umeamka au umeamshwa na habari kubwa, nzito na ya kutisha kuhusu Prof. Malima.

Magazeti yote yalimchukia Prof. Malima na wakimzulia kila aina ya uongo.

Wahariri wa magazti haya kama vile wanamtumikia bwana mmoja walikuwa wamefanana katika stori zao.

Walikuwa kama vile wanauliza na kutoka ujumbe wa fitna.

Prof. Malima alikuwa anaipeleka Tanzania katika siasa ambazo hazikupata kutokea baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.

Prof. Malima alikuwa anachanganya Uislam na siasa kitu ambacho ni mwiko mkubwa kufanyika baada ya kuwa Tanganyika ishajikomboa.

Mambo kama hayo Waislam waliyafanya sana wakati wa kupambana na ukoloni wa Waingereza.

Wakati ule ule misikiti yote ilikuwa ngome za TANU na uwanja wa mapambano Mufti Sheikh Hassan bin Ameir akiuza kadi za TANU misikitini kuwahamasisha Waislam wamuunge mkono Nyerere na TANU kumwondoa Mwingereza katika ardhi ya Tanganyika.

Kanisa ndilo lilikuwa mbali na harakati hizi.

Lakini hili la Prof. Malima kutoka CCM ndani ya msikiti liliwashangaza wengi na wakajiuliza kwa nini iwe hivyo?

Wakajiuliza ni ujumbe gani Prof. Malima alikuwa anaufikisha kwanza kwa taifa zima, kwa Waislam na kwa wasiokuwa Waislam?

Wengi wakasema Prof. Malima sasa anataka kuchafua amani ya nchi kwa matamanio yake binafsi ya kutaka ukubwa na madaraka.

Rangi aliyopakwa Prof. Malima ilikuwa ya mtu hatari sana.

Prof. Malima hakutangaza kujitoa CCM msikitini Ijumaa ile.

Hapa kuna kisa kizuri cha kusisimua jinsi Waislam kwa kuamini propaganda za magazeti na SHIHATA walivyojaza msikitini kuja kumsikiliza Prof. Malima akijitoa CCM kwenye membari ya msikiti wao.

Waislam walijazana hadi nje ya msikiti hali ambayo haikupata kutokea.

Makachero na walijazana wengi ndani na nje ya msikiti siku ile na wengine wakirandaranda katika mitaa ya karibu na msikiti.

Yaliyotokea msikitini pale siku ile yanahitaji makala maalum kuhadithiwa.

Prof. Malima wala hakuwepo Tabora siku ile achilia mbali kuwepo pale msikitini.

Prof. Malima alijitoa CCM siku ya Jumapili tarehe 17 Julai, katika mkutano wa hadhara mkubwa haujapatapo kuonekana mjini pale.

Mpashaji wangu wa habari Mzee Bilal Rehani Waikela anasema mkutano ule uliofanyika Viwanja vya Uyui ulijaza watu kufru kushinda mkutano wa Kura Tatu sokoni Tabora mwaka wa 1958.

Katika hotuba yake Prof. Malima 1994 Prof. Malima alisema CCM imeacha maadili ya usawa na haki kwa raia wake wote na badala yake imejenga matabaka baina ya Watanzania.

Prof. Malima akasema anajitoa CCM na kujiunga na upinzani ili kuondoa matabaka na kuleta usawa na haki kwa raia wote kitu ambacho hakijafanyika toka uhuru upatikane mwaka wa 1961.

Alipofariki Prof. Malima hotuba hii ilipewa jina, ‘’Usia wa Prof. Malima.’’

Hotoba hii ilipendwa sana na Waislam na ndiyo wao waliita, "Usia wa Prof. Malima."

Nasubiri kumsikiliza Benard Membe kwani keshajitoa CCM na kaazimia kugombea urais wa Tanzania.

Membe atakuja na agenda gani?
 
Attachments

  • PROF. KIGHOMA MALIMA.jpg
    PROF. KIGHOMA MALIMA.jpg
    17 KB · Views: 2

Mimi ningali memba wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Malima alikuja kutoa Professorial Inaugral Lecture ikiiwa "The Political Economy of Devaluation" ikiwa ni baada ya Tanzania ku-devalue shilling. Kama kuna mtu ana mawasiliano na Prof Issa Shivji awasiliane naye kuhusu quality ya ile lecture.

Nadhani kipindi hicho ni Mwandosya tu ndiye aliyeitendea haki lecture yake ya "Mutuality of Science and Technology".
 
Nadhani ninayo nakala ya mhadhara huo kwenye makavazi yangu, ngoja niyafukunyue.
 
Back
Top Bottom