Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika 1961: Yaliyomfika Prof. Kighoma Ali Malima hayajamkuta kiongozi yeyote katika historia ya Tanzania

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: YALIYOMFIKA PROF. KIGHOMA ALI MALIMA HAYAJAMKUTA KIONGOZI YEYOTE KATIKA HISTORIA YA TANZANIA

Ally Sykes alikuwa na kawaida kuwa akiwa na mgeni yeyote ndani ya ofisi yake ataagiza niingizwe.

Hivi ndivyo nilivyokuja kuwajua kwa karibu watu wengi maarufu.

Iko siku alikuwa na mazugumzo na Kanyama Chiume ndani ofisini kwake basi akaagiza niingie.

Hii ndiyo siku nilipomjua Kanyama Chiume.

Kanyama Chiume alikuwa amekwenda kwa Ally Sykes kumuonyesha ‘’poposal,’’ ya kuandika historia ya wapigania uhuru wa Afrika Chini ya Ikweta.

Baada ya utambulisho Ally Sykes akaagiza ile ‘’proposal,’’ ifanywe foto kopi nipewe nakala moja.

Kama kawaida yake Bwana Ally akanipamba mwisho wa kunipamba.

Mimi nimejikunyata kimya nimejiinamia angalau nionekana mdogo si lolote si chochote mbele ya Mzee Kanyama Chiume ambae mimi najua sifa zake kubwa katika siasa za ukumbozi wa Nyasaland sasa Malawi.

Katika miaka yangu mingi ya kuishi na Ally Sykes kuna mambo nilikuwa nimejifunza mojawapo ni kukataa sifa alizokuwa ananivika.

Haukupita muda mrefu nikakutana na Mzee Kanyama Chiume nyumbani kwa Hamza Aziz.

Kanyama Chiume alikuwa kasoma kitabu cha Abdul Sykes na naamini alipewa nakala na Ally Sykes kwani hiyo ilikuwa kawaida yake anapotembelewa na watu ambao yeye alikuwanao katika siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Siku ile nilizungumza mengi na Mzee Kanyama Chiume akanieleza kuwa yeye kasoma Kitchwele Boys Government School.

Kanyama Chiume akaniuliza, ‘’Kwa nini kitabu chako tabaruku ni Prof. Kighoma Malima?’’

Jibu nilikuwanalo lakini singeweza kumpa jibu hilo Mzee Chiume nilihisi halitompendeza kama vile alivyochukia kwa mimi kumtanguliza Prof. Malima katika kitabu changu.

Hiyo mosi na pili Hamza Aziz alikuwapo pale ikiwa nitasema jambo likawa si la adabu nitakuwa nimefedhehesha yeye.

Nilishangaa kwa nini Kanyama Chiume hakushughulishwa na maneno ndani ya ile tabaruku kwanì maneno yale yalikuwa ya kutikisa nyoyo.

Kuna watu maalum kutoka jamii maalum walikuwa hawampendi Prof. Malima.

Lakini kulikuwa na umma mkubwa sana tena sana ukimpenda Prof. Malima.

Hili lilidhihirika katika maziko yake pale ilipooneka kuwa umati ule uliojumuika katika mazishi yake usingeenea katika msitiki wowote Afrika ya Mashariki.

Nilikuwako katika maziko ya Prof. Malima na niliuangalia ule umma uliokusanyika Uwanja wa Mnazi Mmoja jeneza lake lilipoletwa ili kusaliwa sala ya jeneza.

Nikaiuliza nafsi yangu, ‘’Hawa ndiyo watu ambao wangempigia kura Prof. Malima katika Uchaguzi Mkuu?’’

Mwalimu Nyerere alipata kumnasihi Prof. Malima aliposikia kuwa Prof. anataka kujitoa CCM na kuingia kwenye chama cha upinzani akamwambia, ‘’Prof. usitoke CCM utaigawa nchi.’’

Niliamini maneno ya Mwalimu kama alivyonieleza Prof. Malima.

Mwalimu alikuwa kaliona hili mapema sana na naamini aliingiwa na hofu na hali ya baadae ya CCM na Tanzania nchi ikiwa katika mpasuko.

Katika kitabu chake, ‘Mzee Rukhsa Safari ya Maisha Yangu,’’ Rais Mwinyi kamtaja Prof. Malima.

Nafsi yangu imeumia sana na hicho nilichosoma.

Hata miaka mingi baada ya umauti wake limekosekana jema la kumzungumza.

Nafarajika kwa kukumbuka yale maziko yake tulipokosa mahali pa kumsalia ikabidi twende kumsalia viwanja vya wazi kama vile tunasali Sala ya Eid.

Nafarajika kuwa kila atakae soma kitabu cha Abdul akikifungua tu atakutana na ukurasa mzima wa tabaruku yangu kwa Prof. Kighoma Ali Malima.

Kupitia ukurasa huu atamjua Prof. Malima na kile alichokuwa anakipigania.

Usawa na haki kwa wote bila ya ubaguzi wa aina yeyote.

Hakika yaliyomfika Prof. Kighoma Ali Malima hayajamkuta kiongozi yeyote katika historia ya Tanzania.

Wasomaji wangu mnayajua yaliyomfika Prof. Malima akiwa waziri ndani ya serikali ya Ali Hassan Mwinyi?

Screenshot_20211204-075501_Facebook.jpg
 
Mzee,(Leo sikuiti Babu kwa kiwa hutaki)
ungemalizia kabisa tujue mini kilimpata Mzaramo huyu genius!
 
Nimepata kufanya kazi na kijana wake mmoja aliekuwa Mganga mkuu pale Amana Hosp, ni mtu safi anaonekana na mwenye msimamo.
 
Mzee,(Leo sikuiti Babu kwa kiwa hutaki)
ungemalizia kabisa tujue mini kilimpata Mzaramo huyu genius!
Lombo,
Si kama sitaki kuitwa babu.

Umri wangu ni miaka 69 na nina wajukuu wananiita babu kwa nasaba na wengine kwa makamo yangu ya uzee.

Nilichokueleza wewe ni kuwa mimi siwezi kuwa babu yako ila baba yako kwani wewe si umri wa mimi kuwa babu yako.

Nimekueleza hivyo kwa kutaka kuweka kila kitu pale panapostahili.

Kwani wewe baba yako ana umri gani?

In Shaa Allah nitakuwekea hapa yaliyomfika Prof. Malima.
 
Lete Historia Kiongozi,wewe amini Mimi ni mjukuu wako!😄
 
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA 1961: YALIYOMFIKA PROF. KIGHOMA ALI MALIMA HAYAJAMKUTA KIONGOZI YEYOTE KATIKA HISTORIA YA TANZANIA

Ally Sykes alikuwa na kawaida kuwa akiwa na mgeni yeyote ndani ya ofisi yake ataagiza niingizwe.

Hivi ndivyo nilivyokuja kuwajua kwa karibu watu wengi maarufu.

Iko siku alikuwa na mazugumzo na Kanyama Chiume ndani ofisini kwake basi akaagiza niingie.

Hii ndiyo siku nilipomjua Kanyama Chiume.

Kanyama Chiume alikuwa amekwenda kwa Ally Sykes kumuonyesha ‘’poposal,’’ ya kuandika historia ya wapigania uhuru wa Afrika Chini ya Ikweta.

Baada ya utambulisho Ally Sykes akaagiza ile ‘’proposal,’’ ifanywe foto kopi nipewe nakala moja.

Kama kawaida yake Bwana Ally akanipamba mwisho wa kunipamba.

Mimi nimejikunyata kimya nimejiinamia angalau nionekana mdogo si lolote si chochote mbele ya Mzee Kanyama Chiume ambae mimi najua sifa zake kubwa katika siasa za ukumbozi wa Nyasaland sasa Malawi.

Katika miaka yangu mingi ya kuishi na Ally Sykes kuna mambo nilikuwa nimejifunza mojawapo ni kukataa sifa alizokuwa ananivika.

Haukupita muda mrefu nikakutana na Mzee Kanyama Chiume nyumbani kwa Hamza Aziz.

Kanyama Chiume alikuwa kasoma kitabu cha Abdul Sykes na naamini alipewa nakala na Ally Sykes kwani hiyo ilikuwa kawaida yake anapotembelewa na watu ambao yeye alikuwanao katika siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Siku ile nilizungumza mengi na Mzee Kanyama Chiume akanieleza kuwa yeye kasoma Kitchwele Boys Government School.

Kanyama Chiume akaniuliza, ‘’Kwa nini kitabu chako tabaruku ni Prof. Kighoma Malima?’’

Jibu nilikuwanalo lakini singeweza kumpa jibu hilo Mzee Chiume nilihisi halitompendeza kama vile alivyochukia kwa mimi kumtanguliza Prof. Malima katika kitabu changu.

Hiyo mosi na pili Hamza Aziz alikuwapo pale ikiwa nitasema jambo likawa si la adabu nitakuwa nimefedhehesha yeye.

Nilishangaa kwa nini Kanyama Chiume hakushughulishwa na maneno ndani ya ile tabaruku kwanì maneno yale yalikuwa ya kutikisa nyoyo.

Kuna watu maalum kutoka jamii maalum walikuwa hawampendi Prof. Malima.

Lakini kulikuwa na umma mkubwa sana tena sana ukimpenda Prof. Malima.

Hili lilidhihirika katika maziko yake pale ilipooneka kuwa umati ule uliojumuika katika mazishi yake usingeenea katika msitiki wowote Afrika ya Mashariki.

Nilikuwako katika maziko ya Prof. Malima na niliuangalia ule umma uliokusanyika Uwanja wa Mnazi Mmoja jeneza lake lilipoletwa ili kusaliwa sala ya jeneza.

Nikaiuliza nafsi yangu, ‘’Hawa ndiyo watu ambao wangempigia kura Prof. Malima katika Uchaguzi Mkuu?’’

Mwalimu Nyerere alipata kumnasihi Prof. Malima aliposikia kuwa Prof. anataka kujitoa CCM na kuingia kwenye chama cha upinzani akamwambia, ‘’Prof. usitoke CCM utaigawa nchi.’’

Niliamini maneno ya Mwalimu kama alivyonieleza Prof. Malima.

Mwalimu alikuwa kaliona hili mapema sana na naamini aliingiwa na hofu na hali ya baadae ya CCM na Tanzania nchi ikiwa katika mpasuko.

Katika kitabu chake, ‘Mzee Rukhsa Safari ya Maisha Yangu,’’ Rais Mwinyi kamtaja Prof. Malima.

Nafsi yangu imeumia sana na hicho nilichosoma.

Hata miaka mingi baada ya umauti wake limekosekana jema la kumzungumza.

Nafarajika kwa kukumbuka yale maziko yake tulipokosa mahali pa kumsalia ikabidi twende kumsalia viwanja vya wazi kama vile tunasali Sala ya Eid.

Nafarajika kuwa kila atakae soma kitabu cha Abdul akikifungua tu atakutana na ukurasa mzima wa tabaruku yangu kwa Prof. Kighoma Ali Malima.

Kupitia ukurasa huu atamjua Prof. Malima na kile alichokuwa anakipigania.

Usawa na haki kwa wote bila ya ubaguzi wa aina yeyote.

Hakika yaliyomfika Prof. Kighoma Ali Malima hayajamkuta kiongozi yeyote katika historia ya Tanzania.

Wasomaji wangu mnayajua yaliyomfika Prof. Malima akiwa waziri ndani ya serikali ya Ali Hassan Mwinyi?

View attachment 2032158
Huwa ndg alikuwa mchochezi wa kidini UDSM na hata alipokuwa waziri wa elimj. Alilisha maneno kuwa wakristo wanapendelewa sana. Lakini hakutambua pia ufaulu wa shule za kiisalamu ulikuwa mdogo sana ukingilisha na ukristo. Atakumbukwa kwa hilo
 
Mkuu hapo umechokoza nyoka kwenye shimo....Mleta mmada hili la Waislam kuonewa ni eneo lake la unobezi subiri...uone!
 
Lete Historia Kiongozi,wewe amini Mimi ni mjukuu wako!😄
Lombo,
Mimi si mtu wa maskhara ya kijinga.
Nakusihi usiniingize huko.

Wajukuu zangu hawajavuka miaka 7.

Wewe unataka kunitania na mimi ni mtu mzima ninaechunga staha na heshima yangu.

Siwezi kukuruhusu kuniweka katika nafasi isiyo yangu kwako.

Mimi kwako nabakia baba yako ikiwa unapenda kuniadhimisha kwa umri wangu.

Hupendi hivyo nibakize kama mtu mwingine yeyote.

Kulikuwa na mtu hapa JF akiniita mufti, maalim na mengine mfano wa hayo.

Nikawa namueleza kuwa mimi siko katika fani hizo mimi ni mtu wa kawaida tu.

Nikawa namueleza kuwa siwezi kuitika katika sifa hizo.

Ajabu kama wewe akawa kashikilia kuniita hivyo.
 
Mkuu hapo umechokoza nyoka kwenye shimo....Mleta mmada hili la Waislam kuonewa ni eneo lake la unobezi subiri...uone!
Lombo,
Hakika mimi nimetafiti kwa muda mrefu katika historia ya Waislam wa Tanganyika.

Hadi sasa nimeandika vitabu vinafikia 10.

Nina research papers nilizowasilisha vyuo kadhaa Ulaya, Marekani na hii Afrika yetu.

Nina kitabu kilichopitiwa na magwiji wa African History ndani ya Cambridge Journal of African History.

Yapo mengi.

Utafiti wangu haujajikita kueleza yale ambayo wewe umeita, "kuonewa Waislam. "

Utafiti wangu umepata sifa na ndiyo sababu ya mimi kualikwa kote huko kwa kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini juu ya haya yote hapakuwa na sababu ya kumtisha Abel.

Yeye kaeleza ayajuayo hakuna ubaya wowote.
 
Back
Top Bottom