Bernard Membe Kumburuza Kortini Hussein Bashe: AK-47 Vs Mawe!

Bernard Membe Kumburuza Kortini Hussein Bashe: AK-47 Vs Mawe!

chikakatata

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
220
Reaction score
98
NDUGU WANABODI,

Kuna taarifa kwamba Waziri wa Manbo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernard Membe ame-engage wanasheria wake dhidi ya Ndg. Hussein Bashe, Kada wa Chama Cha Mapinduzi asiye na wadhifa wowote ule, juu ya kumkashifu na kumuita na kumshambulia kwa maneno makali yasiyo saizi ya heshima aliyonayo Waziri membe. Mhe. Membe ameamua kumburuza kortini Ndg Bashe mnamo siku ya Jumatatu ijayo, kwa mujibu ya jopo la wanasheria wake watatu maarufu na mahiri. Ndg. Bashe, siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa Nane Dodoma alituita waandishi wa habari na kutueleza kuwa "...Membe hafai hata kupewa ubalozi wa nyumba kumi kwa kuwa ni muongo, mnafiki na amezoea kuishi kwa kubebwa..."

Itakumbukwa Mhe Membe alikuwa ni mgombea maarufu na mahsusi wa U-NEC wajumbe kumi na akina Bashe na Lowassa walikuwa kwenye jitihada za hali ya juu kuhonga pesa ili asipite katika kinyang'anyiro kile sambamba na uhamasishaji mkubwa waliokuwa wakiufanya pia kutaka Rais JK ambaye pia alikuwa ni mgombea wa Kiti Taifa cha CCM apate kura za Hapana ili kumuaibisha, ikiwa ni pamoja na hoja ya Hussein Bashe na kundi lake kutaka Uenyekiti wa CCM utenganishwe na U-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkutano huu baina ya waandishi wa habari na Ndg Bashe ulichukuliwa kama sehemu ya mkakati madhubuti wa kutaka kuhakikisha Membe anaaibika na anashindwa uchaguzi ule ili kumkatisha tamaa na kumshusha hadhi kama mgombea Urais haswa ukizingatia kuwa Mkutano Mkuu ule ndiyo utakaopitisha jina la mgombea wa Urais wa CCM 2015; kinyume na mipango na fitna zao, pamoja na hela walizohonga aliibuka kidedea akishika nafasi ya sita bila kutoa hongo wala kuzunguka mikoani kutafuta kura, jambo ambalo liliwashangaza sana wanaCCM na wanahabari wengi waliokuwepo Mkutanoni pale - hali ambayo ilidhihirisha kuwa Membe ana umaarufu wa kutosha kushinda URais huku akigombea kwa kufuata misingi yote ya uadilifu. Pia ikizingatiwa kuwa mshindani wake mkubwa Mhe Lowassa aliliogopa kundi la kifo la NEC na kwenda kugombea UNEC jimboni kwake Monduli.
 
Wewe ni mgonjwa wa akili kwa kweli....membe kapitwa hata na shugera ndio unasema mgombea urais bas sema shigera ni rais kabisa
 
Mkuu asante kwa habari ila umeileta kishabiki kweli, umesema H.Bashe aliwaita waandishi wa habari sasa nashindwa kuelewa kama wewe muandishi wa habari unaandika kishabiki namna hiyo tutapataje habari za uhakika? maana umemfagilia kweli MEMBE, poa lakini kila la kheri katika kazi yako jap[o kwa staili hiyo munafanya tuzidi kuwa na maswali mengi juu ya uadilifu wa uandishi wenu.
 
unajuaje kwamba hakuhonga? ucha kutumika vibaya wewe
 
Mkuu asante kwa habari ila umeileta kishabiki kweli, umesema H.Bashe aliwaita waanduishi wa habari sasa nashindwa kuelewa kama wewe muandishi wa habari unaandika kishabiki namna hiyo tutapataje habari za uhakika? maana umemfagilia kweli MEMBE, poa lakini kila la kheri katika kazi yako jap[o kwa staili hiyo munafanya tuzidi kuwa na maswali mengi juu ya uadilifu wa uandishi wenu.


Mkuu umejuaje ka jamaa ni mwandishi wa habari? Afu mbona unamwambia 'uandishi wenu' kwani wako wangapi.
 
Wewe ni mgonjwa wa akili kwa kweli....membe kapitwa hata na shugera ndio unasema mgombea urais bas sema shigera ni rais kabisa

Unamaanisha Martin Shigella ? Unajua alitumia sh ngapi kuwa mjumbe ? hivi nyie watu wa ccm mkoje ? Unalinganishaje watoa rushwa na wasiotoa !
 
ukiweza jaribu kuibalance habari yako ili iweze kujadilika vinginevyo naona kuna ajenda nyingine ktk hoja yako na hivyo kupoteza urari wa kimjadala!
 
Tunasubiri hiyo Jumatatu kuona kama Bashe kweli ataburuzwa mahakamani.

Pamoja na hayo umempakulia sana pilau Membe wakati naye hatofautiani sana na jamaa aliyopo madarakani.
 
Mkuu umejuaje ka jamaa ni mwandishi wa habari? Afu mbona unamwambia 'uandishi wenu' kwani wako wangapi.

Mkuu ukisoma vizuri jamaa amesema "alituita waandishi wa habari" na kusema wako wangapi ni vile waandishi nao wameingia kwenya mtego wa makundi ya CCM, kila anayetaka uongozi ndani ya CCM lazima awe na waandishi wake mfukoni, mifano ni mingi lakini fasta fasta hembu mkumbuke RWEYEMAMU jamaa ni kichwa kwenye uandishi lakini akaisaliti kalamu na karama yake 2005 na malipo yake si unaona alipo sasa?
 
Mwandishi wa habari hii ni mzee wa bahasha za kaki kama Pasco.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
magamba mnagombana nini mtamfanya mke wenu caf kujifunguwa siku si zake
 
Aisee! Hebu huyu mheshimiwa aende mahakamani haraka ili moto mwingine uwake ndani ya CCM. Na ikiwezekana, baada ya yeye kuwasha moto huo, watokee wapumbavu wengine ndani ya chama hicho hicho ambao watajaribu kuuzima moto huo kwa kuumiminia petroli huku wakidhani ni maji.
 
Wewe ni mgonjwa wa akili kwa kweli....membe kapitwa hata na shugera ndio unasema mgombea urais bas sema shigera ni rais kabisa

Ni sababu zipi za msingi zinazopelekea kuamini kuwa mtu hawezi kuwa rais bora wa Tanzania hadi awe member nec ya ccm? ina maana chadema,cuf,tlp,nccr n.k hawawezi kutoa rais bora kwa kuwa hawezi kuwa member wa nec-ccm? na je hakuna mwanaccm yoyote ambae si member wa nec awezaye kuwa rais bora?
 
Back
Top Bottom